
Yanga SC 3-1 KVZ Mchezo wa Kirafiki Zanzibar | Highlights | SportPesa Blog
- FT:Yanga SC 3-1 KVZ ya Zanzibar mchezo wa kirafiki uliochezwa Novemba 14, 2026.
- Fadlu Davids mrithi wa mikoba ya Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini amenanza kazi kwa ushindi.
- Aziz Ki kiungo wa Yanga SC amekuwa mpishi katika mchezo huo akitoa asisti 3 zote zikileta mabao.
Ni Yanga SC 3-1 KVZ ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki kazi imeanza kwa kocha mpya Fadlu Davids.Huu ni mchezo wa kwanza kwa mrithi wa mikoba ya Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini aliyefutwa kazi Jangwani hivi karibuni.Novemba 7,2026 usiku wa manane,Fadlu alitua Bongo na kuanza kazi kulipopambazuka yupo na timu Zanzibar ilipoweka kambi kujifua na mechi za kitaifa na kimataifa.
Yanga SC 3-1 KVZ wafungaji wa mabao
Novemba 14, 2026 matokeo rasmi ilikuwa Yanga SC 3-1 KVZ ya Zanzibar ikiwa ni kete ya kwanza kwa Fadlu Davids.Wafungaji wa mabao ya Yanga SC walikuwa ni CheikToure alifunga mabao mawili na Edmund John alifunga bao moja.Asisti zote tatu zilitoka kwa kiungo mshambuliaji Aziz Ki.
Mchezo huu wa kirafiki ulikuwa sehemu ya maandalizi ya Yanga SC kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) na mashindano mengine ya kimataifa. Mchezo ujao kwa Yanga SC unatarajiwa kupigwa Novemba 20, 2026, Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi itakuwa Polisi Tanzania vs Yanga SC, NBC Premier League Uwanja wa Ushirika Moshi.
Kwenye anga la kimataifa, CAF Champions League Fadlu kete ya kwanza atakuwa nyumbani. Yanga SC vs MC Alger ya Algeria unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Dar, Novemba 28, 2026. Hivyo maandalizi ya kikosi yanaendelea kwa sasa.
Maandalizi kuelekea msimu mpya
Yanga SC inaendelea na kambi yake ya maandalizi Zanzibar ikitarajiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Mashabiki wanatarajia kuona timu yao ikifanya vizuri na kutetea mataji yao.Ni wazi kuwa Yanga SC ni mabingwa watetezi wa NBC Premier League.
Miongoni mwa wachezaji ambao wapo na kikosi Zanzibar mbali na Aziz Ki yupo Clement Mzize ambaye ni mshambuliaji.Dickson Job huyu ni nahodha msaidizi na beki wa kati.Aboutwalib Mshery mlinda mlango.
Hitimisho
Yanga SC 3-1 KVZ ya Zanzibar ni mwanzo mzuri kwa benchi jipya laufundi. Fadlu amebainisha kuwa amewaona vijana wakipambana katika mechi anaamini watazidi kuwa imara.Mchezo ujao kwenye ligi kwa Yanga SC itakuwa ugenini dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Ushirika, Moshi.

