Polisi Tanzania vs Yanga SCShalulile (-)Shalulile (-)

Polisi Tanzania vs Yanga SC
Anuary Jabir mshambuliaji wa Polisi Tanzania

Polisi Tanzania vs Yanga SC | Azam FC vs Singida Black Stars | NBC Premier 20/11/2026

  • Burudani zinarejea ndani ya NBC Premier League huku Polisi Tanzania vs Yanga SC likiwa ni pambano la mapema saa 10:00 jioni, 20/11/2026.
  • Azam FC watakuwa Uwanja wa Azam Complex saa 3:00 usiku, Namungo FC vs Mbeya City saa 12:30 jioni.
  • Vinara wa ligi Simba SC mchezo wao unaofuata unatarajiwa kupigwa Novemba 21, 2026 itakuwa dhidi ya JKT Tanzania.
  • Makala haya imekuletea ratiba ya mechi kali za NBC Premier League zitakazochezwa Novemba 20/2026

Polisi Tanzania vs Yanga SC ni ratiba ya mchezo ujao NBC Premier League 20/11/2026.Burudani ya ligi inarejea mara baada ya kusimama kwa muda kutokana na ratiba za FIFA.Mbali na mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni, Uwanja wa Moshi kuna mechi nyingine mbili kazi zaidi zitapigwa.

Namungo FC vs Mbeya City, saa 12:30 jioni, Uwanja wa Majaliwa. Azam FC vs Singida Black Stars saa 3:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex wababe hawa wakiwa kazini kusaka pointi 3 muhimu.

SOMA HII PIA:Rasmi Fadlu Davids ni kocha mpya Yanga SC 2026/27 | SportPesa Blog

Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Polisi Tanzania vs Yanga SC na ratiba zijazo NBC Premier League

Mechi Muda Uwanja Mkoa / Jiji
Polisi Tanzania vs Yanga SC Saa 10:00 Jioni Uwanja wa Ushirika Moshi
Namungo FC vs Mbeya City Saa 12:30 Jioni Uwanja wa Majaliwa Lindi (Ruangwa)
Azam FC vs Singida Black Stars Saa 3:00 Usiku Uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam

Msimamo wa NBC Premier League

Simba SC ni vinara wakiwa na pointi 30, Yanga SC nafasi ya pili wana pointi 25.Azam FC nafasi ya 3 wakiwa na pointi 23, JKT Tanzania nafasi ya 4 wana pointi 17 na Dodoma Jiji FC nafasi ya 5 wakiwa na pointi 16.

Polisi Tanzania vs Yanga SC NBC Premier League
NBC Premier League msimamo

SOMA HII PIA:Hizi hapa mechi 3 za kwanza za Kocha Fadlu Davis Yanga SC: 2 ni za Ligi Kuu NBC na moja ni dhidi ya Waarabu MC Alger kutoka Algeria

JKT vs Simba SC mechi inayofuata

Vinara wa ligi mchezo wao ujao watakuwa ugenini.Ni JKT Tanzania vs Simba SC unatarajiwa kupigwa Novemba 21, 2026.Wababe hawa watakuwa kazini kusaka pointi 3 muhimu.

Ikumbukwe kwamba Simba SC haijapoteza mchezo wowote ndani ya NBC Premier League.Matokeo ya mchezo uliopita ilikuwa Simba SC 3-2 Namungo FC, Uwanja wa Uhuru.Wanakaribishwa na JKT Tanzania iliyopoteza mechi 4.

Hitimisho

Polisi Tanzania vs Yanga SC Novemba 20, 2026 ni mwendelezo wa burudani ndani ya NBC Premier League.Huu ni mchezo unaosubirwa kwa shauku kubwa kwa kuwa Yanga SC watashuhudia mbinu za kocha mpya Fadlu Davids.Polisi Tanzania watashuhudia timu yao ikiwa Moshi ikitumia Uwanja wa Uhirika kwa mechi za nyumbani.

Share this: