
Taarifa kuhusu Bacca,Kangwanda na Maxi Nzengeli ipo hivi | SportPesa Blog
- Yanga SC imetoa taarifa kuhusu Bacca, Kangwanda na Maxi Nzengeli ambao maendeleo yao.
- Kangwanda alipata maumivu akiwa katika timu ya taifa ya Zambia anatarajiwa kurejea uwanjani hivi karibuni.
- Polisi Tanzania vs Yanga SC ni mchezo ujao kwenye ratiba ya NBC Premier League.
Klabu ya Yanga SC imetoa taarifa kuhusu Bacca, Kangwanda na Maxi Nzengeli. Taarifa hizi zinakuja wakati timu ikiendelea na maandalizi yake kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano mengine.Wachezaji wawili walipata maumivu wakiwa katika majukumu ya taifa isipokuwa Maxi alipata maumivu katika uwanja wa mazoezi.
SOMA HII PIA:Maxi Nzengeli: Wasifu Kamili wa Kiungo Mshambuliaji wa Yanga SC
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege
Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.
Taarifa kuhusu Bacca, Kangwanda na Maxi Nzengeli
Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC ametoa taarifa kuhusu Bacca, Kangwanda na Maxi Nzengeli akibainisha kwamba wanaendelea vizuri.Timu hiyo imeweka kambi Zanzibar ikiendelea na maandalizi kwa mechi zijazo za kitaifa na kimataifa.Bacca alipata maumivu akiwa na timu ya taifa ya Tanzania na Kangwanda alipata maumivu akiwa na timu ya taifa ya Zambia.
Kuhusu Bacca, taarifa kutoka Yanga SC zinaeleza kuwa anaendelea vizuri na matibabu yake. Klabu haijatoa tarehe kamili ya kurejea kwake uwanjani, lakini imethibitisha kuwa maendeleo yake ni mazuri na anafanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari.
“Albert Kangwada na Ibrahim Bacca walipata maumivu kwenye majukumu yao tunamshukuru Mungu wanaendelea vizuri.Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari wa timu ambazo wapo wametuambia wanaendelea vizuri.Kangandwa alipata maumivu ya misuli kidogo hivyo atarejea kwenye ubora hivi karibuni na ataungana na timu,” alisema Kamwe.
SOMA HII PIA:Beki Ibrahim Bacca wa Yanga SC amefungiwa mechi 5 na TPLB
Maxi nzengeli na mustakabali wake
Maxi Nzengeli, kiungo mshambuliaji mwingine wa Yanga, pia anafanyiwa tathmini ya kina kuhusu hali yake. Taarifa zinaeleza kuwa atakuwa nje kwa muda kutokana na kutokuwa fiti.Nyota huyu amekuwa imara kwenye eneo la kiungo kutokana na jitihada zake kutimiza majukumu ndani ya uwanja.
Athari kwa kikosi cha Yanga SC
Kukosekana kwa wachezaji hawa muhimu kunaweza kuathiri mipango ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Lakini Yanga SC ina kikosi kipana chenye wachezaji wenye uwezo wa kuziba nafasi hizo. Timu inaendelea kujifua vikali kuhakikisha inabaki imara katika mashindano yote.
Fadlu ameweka wazi kuwa wana mechi ngumu mbele yao watapambana kufanya vizuri.Kuhusu mechi za CAF wanatambua umuhimu wake watapambana kupata matokeo chanya.Amewaomba mashabiki kuwapa ushirikiano katika kila mechi.
“Tuna mechi ngumu ambazo zipo kwenye ratiba hilo tunalitambua.Kikubwa ambacho tunafanya ni maandalizi mazuri.Ninaona wachezaji wanajituma na kufanya vizuri hivyo kazi bado inaendelea,”.
Hitimisho
Yanga SC inaendelea kufuatilia kwa karibu hali za afya za Bacca, Kangwanda na Maxi Nzengeli. Wachezaji hawa wanatarajiwa kujiunga na timu mara baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa.Mchezo ujao kwa ni Polisi Tanzania vs Yanga SC, Uwanja wa Ushririka, Mosho, Novemba 20, 2026.


