England vs Croatia FIFA Kombe la Dunia 2026England
  • Timu zina deni bado England vs Croatia FIFA Kombe la Dunia 2026, Juni 17, 2026
  • H2H mechi 11, ushindi England mara 6, Croatia mara 3 huku wakitoshana nguvu mara 2
  • SportPesa Blog imekuletea takwimu, muda wa mchezo kwa saa Afrika Mashariki na utabiri

England vs Croatia FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mechi ya kundi L itakayochezwa Uwanja wa AT & T, mji wa Arlington, USA. Makala hii inakuletea England vs Croatia prediction, muda wa mechi saa za Afrika Mashariki, team news, lineups, H2H, odds za SportPesa na live score updates. Timu hizi bado zina deni la kihistoria halijalipwa tangu nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018 mjini Moscow, England ni fursa kufuta kumbukumbu za kuondolewa na Croatia miaka minne iliyopita.

Ijue ratiba kamili ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Iraq vs Norway, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa, bashiri kwa uwajibikaji.

England
England vs Croatia, odds zilizoboreshwa

Updated: England vs Croatia team news, lineups, kick-off time, H2H na odds kbla ya mchezo wa kundi L Kombe la Dunia 2026.

KipengeleMaelezo
MechiEngland vs Croatia
MashindanoFIFA World Cup 2026
KundiKundi L
TareheJuni 17, 2026
UwanjaAT & T Stadium
Muda (EAT)Saa 9:00 alasiri
Betting PlatformSportPesa

Kundi L linaundwa na England, Croatia, Ghana na Panama, na mchezo huu wa ufunguzi kati ya timu mbili zenye uzoefu mkubwa zaidi kwenye kundi hilo una umuhimu mkubwa. Ushindi kwa upande wowote unaweza kuwapa udhibiti wa kundi tangu mwanzo, huku kichapo kikimaanisha kulazimika kupambana kufidia pengo hilo katika mazingira magumu ya joto kali la majira ya kiangazi nchini Marekani.

England vs Croatia taarifa muhimu za mechi

UBAO umesoma Ubelgiji 1-1 Misri katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa FIFA Kombe la Dunia hatua ya makundi ikiwa ni Kundi G usiku wa Juni 15, 2026.

Ni Emam Ashour alianza kufunga katika dakika ya 20 goli ambalo lilidumu mpaka dakika ya 66 na kijana huyo alifunga bonge moja ya goli akiwa nje ya 18 likiwanyanyua mashabiki wa Misri.

Kuingia kwa mshambuliaji nyota wa Ubelgiji, Romelu Lukaku dakika ya 65 kulibadilisha usomaji wa matokeo ambapo alisababisha Misri kujifunga dakika ya 66 kupitia kwa Mohamed Hany.
England vs Croatia

Mabingwa wanarejea kazini na mchezo wao huu hapa usome: Argentina vs Algeria FIFA Kombe la Dunia 2026: Wachezaji muhimu, muda, h2h, utabiri | SportPesa Blog

WhatsApp Image ---------- at --------

Croatia ilipoifunga England kwa mabao 2-1 nusu fainali ya Kombe la Dunia 2018 mjini Moscow ni deni kwa England. Kikosi cha Gareth Southgate hakikuweza kuondoa kumbukumbu ya kipigo hicho, huku Luka Modrić, Ivan Perišić na wenzake wakiiandikia Croatia moja ya kurasa za dhahabu katika historia yao ya soka.

England chini ya kocha Thomas Tuchel inaonekana kuwa timu yenye mpangilio wa hali ya juu, nidhamu ya kiufundi na umakini mkubwa kuliko ilivyokuwa katika enzi za hivi karibuni chini ya Southgate. Mfumo wa 4-2-3-1 uliotumika kwenye mechi za kufuzu unaweka viungo wawili wa ulinzi mbele ya mabeki, huku Jude Bellingham akipewa uhuru wa kushinikiza mbele na kuingia eneo la hatari kwa kuchelewa.

Takwimu za kufuzu zinaonyesha ubora wao: ushindi mechi 8, mabao 22 ya kufunga na kutoruhusu bao lolote katika kampeni nzima ya hatua ya makundi ya UEFA. Croatia italazimika kufanya kazi kubwa kuvunja uimara wa safu ya ulinzi ya England mapema kwenye mchezo huu.

Kwa upande mwingine, Croatia ya Zlatko Dalić inaingia kwenye mashindano haya ikiwa ni timu inayojulikana kwa kuzidi matarajio katika majukwaa makubwa, lakini pia ikiwa kwenye kipindi cha mpito wa kizazi huku ikikabiliwa na presha kubwa. Luka Modrić anaelekea kwenye kile kinachoonekana kuwa Kombe lake la Dunia la mwisho akiwa na umri wa miaka 40. Ingawa mchango wake katika kudhibiti kasi na mwelekeo wa mchezo wa Croatia bado hauna mbadala, mahitaji makubwa ya kimwili ya mfumo wa kushinikiza kwa nguvu katika joto la Texas yanaweza kuwa changamoto kubwa kwake na kwa timu yake.

Fomu ya England kabla ya mechi

TareheMechiUwanjaMashindanoMatokeo
Juni 2026England vs Costa RicaUwanja wa NeutraliKirafiki3–0
Juni 2026England vs New ZealandUwanja wa NeutraliKirafiki1–0
Machi 2026England vs JapanNyumbaniKirafiki0–1
Machi 2026England vs UruguayNyumbaniKirafiki1–1
Novemba 2025Albania vs EnglandUgeniniKufuzu Kombe la Dunia0–2

Fomu ya Croatia kabla ya mechi

TareheMechiUwanjaMashindanoMatokeo
Juni 2026Croatia vs SloveniaNyumbaniKirafiki2–1
Juni 2026Croatia vs BelgiumNyumbaniKirafiki0–2
Machi 2026Croatia vs BrazilUwanja wa NeutraliKirafiki1–3
Machi 2026Croatia vs ColombiaUwanja wa NeutraliKirafiki2–1
Novemba 2025Montenegro vs CroatiaUgeniniKufuzu Kombe la Dunia2–3

England vs Croatia H2H

TareheMashindanoMechiMatokeo
13.06.2021EUREngland vs Croatia1–0
18.11.2018UNLEngland vs Croatia2–1
12.10.2018UNLCroatia vs England0–0
11.07.2018WC (AET)Croatia vs England2–1
09.09.2009WCEngland vs Croatia5–1
10.09.2008WCCroatia vs England1–4
21.11.2007EUREngland vs Croatia2–3
11.10.2006EURCroatia vs England2–0
21.06.2004EURCroatia vs England2–4
20.08.2003FIEngland vs Croatia3–1
24.04.1996FIEngland vs Croatia0–0

Timu hizi zimekutana kwenye mechi 11. Ushindi kwa England mechi 6, Croatia mechi 3 ushindi. Wametoshana nguvu katika mechi 2.

Taarifa ya kikosi cha England

England vs Croatia FIFA Kombe la Dunia 2026
Timu ya taifa ya England.

Utambue utabiri na odds za mchezo wa Iraq vs Norway: Iraq vs Norway prediction: utabiri, muda, vikosi, h2h, live score, odds

England inaingia kwenye mashindano haya ikiwa imetangaza kikosi chake kamili bila kuwa na majeraha makubwa. Nahodha Harry Kane anawasili akiwa katika hali bora kabisa, huku akieleza wazi kuwa anajisikia kuwa katika kiwango chake cha juu zaidi baada ya msimu mzuri katika soka la klabu. Jude Bellingham naye anakuja akiwa na morali kubwa baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa Real Madrid.

Declan Rice na Bukayo Saka wote wako fiti na wanatarajiwa kuanza katika kikosi cha kwanza. Mjadala mkubwa wa uteuzi wa kikosi unaonekana kuwa katika nafasi ya mabeki wa kati, ambapo John Stones, Marc Guehi na Ezri Konsa wanapambana kuwania nafasi za kuanza. Upande wa kushoto wa ushambuliaji pia unampa Thomas Tuchel chaguo kadhaa, akiwemo Anthony Gordon pamoja na Noni Madueke.

Taarifa ya kikosi cha Croatia

Croatia ina wasiwasi mmoja mkubwa kuhusu hali ya Luka Modrić. Kiungo huyo mkongwe alipata jeraha la kuvunjika mfupa wa shavu kabla ya mashindano kuanza, lakini tayari amethibitishwa kuwemo katika kikosi cha Kombe la Dunia 2026 na anatarajiwa kucheza.

Swali kubwa ni kama Modrić ataanza moja kwa moja katika mchezo huu wa ufunguzi au kama kocha Zlatko Dalić atachagua kumtumia taratibu ili kumlinda kwa michezo ijayo ya mashindano.

Joško Gvardiol, beki wa kati wa Manchester City na mmoja wa mabeki bora barani Ulaya kwa sasa, yuko katika hali nzuri na ni chaguo la uhakika katika kikosi cha kwanza. Dominik Livaković ataendelea kuwa kipa namba moja wa Croatia, huku Mateo Kovačić akiwa tayari kuiongoza safu ya kiungo.

Vikosi Vinavyotarajiwa Kuanza

England (4-2-3-1)

Pickford; James, Stones, Guehi, Livramento; Rice, Mainoo; Saka, Bellingham, Gordon; Kane (Nahodha).

Croatia (4-2-3-1)

Livaković; Stanišić, Šutalo, Gvardiol, Pongračić; Kovačić, Mario Pašalić; Vlašić, Modrić (Nahodha), Perišić; Kramarić.

Jinsi ya kuangalia (How to watch) England vs Croatia

Mashabiki wanaweza kufuatiliaEngland vs Croatia kupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Prediction

England vs Croatia prediction ni upande wa England ambayo imepata ushindi mara 6 dhidi ya wapinzani wao. Magoli yatakayofungwa sio mengi kutokana na ushindani uliopo. England 2-1 Croatia. Haya ni maoni sio matokeo kamili.

Share this: