- Brazil vs Morocco Utabiri & Preview Kombe la Dunia 2026 inasubiriwa kwa hamu kubwa, hii ni kutokana na ubora wa timu zote mbili.
- Mabingwa hao wa dunia mara 5, Brazil wataanza kampeni yao ya Kundi C katika Kombe la Dunia 2026 kwa kukutana na miamba ya Afrika Morocco.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa MetLife uliopo New Jersey, usiku wa saa 7 kuamkia Jumapili kwa saa za Afrika Mashariki
- Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa 25 Machi 2023 ambapo matokeo yalikuwa Morocco 2-1 Brazil
Mabingwa wa dunia mara tano, Brazil wataanza kampeni yao ya Kundi C katika Kombe la Dunia 2026 kwa kukutana na miamba ya Afrika Morocco.Brazil vs Morocco Utabiri & Preview Kombe la Dunia 2026, unaipa nafasi kubwa Brazili kuibuka na ushindi. Hii ni zaidi ya mechi ya soka, ni vita ya mastaa wakubwa kama Vinicius Jr, Neymar Jr dhidi ya mastaa wa Morocco akiwemo nahodha wao Achraf Hakimi. Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa MetLife uliopo New Jersey, usiku wa saa 7 kuamkia Jumapili kwa saa za Afrika Mashariki. M
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mechi za Kombe la Dunia. Ili kushinda beti mechi ya Ufunguzi kati ya Brazil vs Morocco Afrika kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu Brazil vs Morocco Utabiri & Preview Kombe la Dunia 2026

Brazil
Brazil wataingia katika mchezo huu wakiwa na mipango ya kufuta kumbukumbu ya kuondolewa katika hatua ya robo fainali, kwenye fainali za nchini Qatar miaka minne iliyopita. Morocco wanaofahamika kama Simba wa Atlas Lions wanakabiliwa na mtihani mgumu. Ikumbukwe Fainali zilizopita walipata mafanikio ya kushangaza kwa kufika nusu fainali.
Brazil ndiyo taifa lenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia. Wamecheza mechi nyingi zaidi (114), kushinda mechi nyingi zaidi (74) na kutwaa mataji mengi zaidi (matano), kuliko taifa lolote. Pia ndiyo nchi pekee iliyofuzu fainali zote za Kombe la Dunia tangu mashindano ya kwanza mwaka 1930.
Hata hivyo, mara ya mwisho kushinda ubingwa huo ilikuwa mwaka 2002. Kipindi chao cha miaka 24 bila ubingwa kinafanana kabisa na ukame wao wa kihistoria kati ya mwaka 1970 na 1994, ambao ulihitimishwa nchini Marekani. Brazil walipambana kufuzu mashindano haya mapya yenye timu 48, hii ni baada ya kushinda mechi nane, kutoka sare nne na kupoteza sita katika michezo 18 ya kufuzu. Hii iliwafanya kumaliza nafasi ya tano, na kupata moja ya nafasi sita za moja kwa moja.
Brazil wameshinda mechi zake tatu zilizopita dhidi ya Croatia, Panama na Misri kwa jumla ya mabao 11-4. Brazil wanaingia kwenye pambano hili dhidi ya Morocco, wakiwa nafasi ya tano katika viwango vya FIFA. Tovuti nyingi za ubashiri zinawapa nafasi kubwa ya kusonga mbele kutoka Kundi C.
Morocco
Miaka minne baada ya kuwa taifa la kwanza la Afrika kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia, Morocco wanajiandaa kushiriki mashindano hayo kwa mara ya saba. Morocco ni miongoni mwa timu zinazoweza kuendeleza rekodi ya kufanya maajabu makubwa. Simba wa Atlas wamekuwa taifa lenye nguvu kubwa kisoka katika miaka ya karibuni, wakishinda mechi 33, kutoka sare 10 na kupoteza mara mbili pekee katika michezo 45 tangu mwanzoni mwa mwaka 2023. Kwa sasa wanashika nafasi ya saba duniani mbele ya Uholanzi, Ubelgiji na Ujerumani.
SOMA HII PIA: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Brazil vs Morocco h2h

Katika historia yao, Morocco wanaingia katika mchezo huu wakiwa wamepoteza mechi 2 kati ya 3 walizocheza dhidi ya Brazil. Hata hivyo, walishinda mchezo wao wa mwisho wa kirafiki kati ya mataifa hayo kwa mabao 2-1 mwezi Machi 2023. Je, nani ataandika historia mpya.
Fomu za timu
Brazil: W, D, L, W, W, W
Morocco: W, D, W, W, W, D
Habari za timu na majeruhi
Brazil

Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, Neymar Jr bado anaendelea kuuguza jeraha la misuli ya mguu na hatarajiwi kuwa tayari kwa mchezo huu. Beki wa kulia Wesley pia ameondolewa kwenye Kombe la Dunia, kutokana na jeraha la misuli alilopata katika ushindi dhidi ya Misri. Kiungo Ederson, anayetarajiwa kujiunga na Manchester United, aliitwa kikosini dakika za mwisho na inaelezwa alijaribiwa kucheza nafasi ya beki wa kulia mazoezini. Danilo na Roger Ibanez ni miongoni mwa wachezaji wengine wanaoweza kucheza upande huo wa ulinzi.
Alisson Becker, Gabriel Magalhaes na Bruno Guimaraes wanatarajiwa kuanza kikosini pamoja na Vinicius Junior wa Real Madrid na Raphinha wa Barcelona. Ancelotti pia atafanya uamuzi kati ya Matheus Cunha, Endrick au Igor Thiago kuanza kama mshambuliaji wa kati.
SOMA HII ZAIDI: Sheria mpya za mechi Kombe la Dunia 2026 zashtua! Nini kimebadilishwa?
Morocco

Kwa upande wa Morocco, beki Nayef Aguerd (majeraha ya kinena) na winga Abde Ezzalzouli (goti) watakosa Kombe la Dunia kutokana na majeraha. Nafasi zao zimechukuliwa na Marwane Saadane wa Al Fateh na Amine Sbai wa Angers. Ezzalzouli alipata jeraha hilo katika sare dhidi ya Norway, huku Noussair Mazraoui pia akitolewa kutokana na tatizo la bega.
Nahodha Achraf Hakimi na Brahim Diaz wanatarajiwa kuanza kikosini. Diaz alifunga bao lake la 14 la kimataifa katika mechi 26 dhidi ya Norway, na anaweza kuungana katika safu ya ushambuliaji. Nyota wengine wa ushambuliaji ni pamoja na Ismael Saibari na Bilal El Khannouss.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator
Vikosi vinavyoweza kuanza
Brazil: Alisson; Danilo, Marquinhos, Gabriel, Sandro; Casemiro, Guimaraes; Raphinha, Paqueta, Vinicius Jr; Cunha.
Morocco: Bounou; Hakimi, Diop, Riad, Mazraoui; Amrabat, El Aynaoui, Ounahi; Diaz, Saibari, El Khannouss.
Utabiri wetu na hitimisho
Brazil vs Morocco Utabiri & Preview Kombe la Dunia 2026 ni miongoni mwa ratiba zinazotabiriwa ushindani mkubwa kwenye Kombe la Dunia 2026. Morocco huenda wakatoa ujumbe mzito, na kuongeza matumaini yao ya kuongoza Kundi C iwapo watafanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya Brazil. Ikumbukwe mataifa hayo yanayotofautiana kwa nafasi moja tu, katika viwango vya FIFA hata hivyo Brazil wana nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

