- Kuna Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 ambazo zitakwenda kutumika kwenye mashindano haya makubwa
- Sekunde 10 zitatumika kwenye sub na ikitokea mchezaji anayetoka akashindwa kuzitumia adhabu atapewa mrithi wa nafasi yake kwa muda wa dakika moja.
- Mechi 104 zitachezwa bingwa mmoja anatafutwa, timu 48 ambazo zinashiriki mashindano haya
- Juni 11, 2026 mchezo wa ufunguzi utachezwa na fainali ya FIFA Kombe la Dunia 2026 itakuwa Julai 19
Kuna Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 zitaleta mabadiliko kwenye mchezo wa miguu. Sababu kubwa za sheria hizi mpya ni kupunguza kupotea kwa muda na kuongeza haki katika maamuzi. Kuna mengi tutakwenda kushuhudia katika mashindano haya yanayotorajiwa kuwa na ushindani mkubwa kuanzia Juni 11, 2026.
SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 hizi hapa

SOMA HII: Je, Lionel Messi atakosa Kombe la Dunia 2026? Maamuzi mazito yanasubiriwa, kocha Argentina afunguka

Zimebaki siku 5 kuanzia Juni 6, 2026 kabla ya kivumbi kuanza kutimka, tunakuletea Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 ambazo zitakwenda kutumika. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi FIFA, Pieluigi Collina ameweka wazi kuwa baadhi ya mabadiliko tayari yameidhinishwa. Lengo kubwa ni kuhakikisha mchezo unakuwa na kasi na uwazi.
Mapumziko ya kimkakati ya kipa
Moja ya mabadiliko muhimu ni kwenye kuzuia mapumziko ya kimkatati ya kipa. Hapa ni pale ambapo kipa hujilaza chini ya uwanja akidai kuumia. Wakati kipa akiwa amejilaza, wachezaji wengine huelekea kwenye benchi la ufundi kupata maelekezo ya kocha.
FIFA imeamua kwamba ikiwa kipa ataumia na mchezo kusimamishwa, wachezaji wa timu zote hawataruhusiwa kuelekea benchi la ufundi. Jambo ambalo wanapaswa kufanya ni kubaki pale walipo ama kukusanyika katikati ya uwanja kusubiri mchezo kuendelea. Hili ina mlengo kuondoa matumizi ya majeraha kama njia yakupata muda wa kupanga mikakati.
Matumizi ya VAR

Sheria mpya inakwenda kugusa matumizi ya teknolojia ya usaidizi wa Video, (VAR) katika mipira ya adhabu na kona. Awali matukio ya faulo yaliyotokea kabla ya mpira kuchezwa rasmi hayakuchunguzwa na VAR. Hilo limefanyiwa mabadiliko kwa kuwa kulikuwa na malalamiko katika baadhi ya mechi ambazo zilichezwa.Kupitia uamuzi wa kadi ya pili ya njano uliosababisha mchezaji kutolewa uwanjani isipokuwa kadi za njano za kawaida hazitaangaliwa na VAR.
Kuna magoli ambayo yamekuwa yakipatikana bila haki baadhi. Hii ni pale ambapo washambuliaji wanafanya makosa au vizuizi kabla ya mpira kupigwa lakini mchezo unaendelea kama kawaida. IFAB imekubali mabadiliko yanayoruhusu VAR kuchunguza makosa yanayotokea kabla ya mpira kuchezwa. Inamaanisha kwamba iwapo itabainika kulikuwa na faulo kabla ya kona ama mpira wa adhabu kupigwa mwamuzi atakuwa na ruksa kuamuru mpira urudiwe tena.
Sekunde 5 mpira kurushwa
Miongoni mwa mabadiliko yatakayotumika kwenye Kombe la Dunia 2026 ni sheria ya kuhesabu sekunde 5 kwa mipira kurushwa. Ikitokea mchezaji akachelewesha kwa makusudi kuurudisha mpira mchezoni baada ya muda kuisha timu pinzani itapewa faida. Hivyo lengo ni kuona kasi ya mpira inaendelea.
Sekunde 5 kwa mpira wa golikiki
Ikiwa timu A itajaribu kupoteza muda na kuchelewesha kuanza tena mchezo kutakuwa na adhabu. Hapo timu B itapewa haki ya kuanzisha mchezo na mwamuzi kwa kuwapa faida ya kona kama adhabu. Lengo ni kupunguza tabia ya kupoteza muda hasa katika dakika za lala salama.
Sekunde 10 kwa mchezaji anayefanyiwa mabadiliko
Kwenye Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 kuna suala la sekunde 10 kwa mchezaji anayefanyiwa mabadiliko, (sub). Ni sekunde 10 mchezaji anatakuwa kufika nje kwa kupitia njia ya karibu zaidi. Ikitokea akachelewa mchezaji mbadala wake hataruhusiwa kuingia mara moja na timu italazimika kucheza pungufu kwa muda wa dakika moja.
Mchezaji anayepatiwa matibabu ni sekunde 60 nje ya uwanja
Kwenye upande wa matibabu ya majeruhi, mchezaji ambaye atakuwa anapatiwa huduma atalazimika kubaki nje ya uwanja sekunde 60, (dakika 1). Baada ya hapo ataruhusiwa kuingia uwanjani kuendelea kucheza. Isipokuwa majeraha maalumu kama kipa au pale mpinzani amepewa kadi ya njano ama nyekundu.
Kufunika mdomo huku ukizungumza
Mchezaji atakayefunika mdomo wake kwa mkono, jezi au njia nyingine wakati akizungumza au kubishana na mpinzani wake anaweza kuadhibiwa kadi nyekundu. Hatua hii inalenga kuongeza uwazi. Pia kuzuia tabia zinazoweza kuficha mawasiliano ya wachezaji hasa matusi na ubaguzi wa rangi kwenye mpira.
Hitimisho
Sheria 7 FIFA Kombe la Dunia 2026 zinatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika kumtafuta bingwa. Ni ushirikiano wa nchi 3 unaandaa ikiwa ni Marekani, (USA), Canada na Mexico. Mashindano haya hufanyika kila baada ya miaka 4 mara ya mwisho yalifanyika 2022 nchini Qatar. Je nani atatwaa ubingwa? Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa za hivi punde.

