- Pedro Goncalves afutwa kazi Yanga SC rasmi Mei 6, 2026
- Mrithi wa mikoba yake ni Abdihamid Moalin na kocha Patrick Mabedi
- Yanga SC inaachana na Pedro mwenye miaka 50 ikiwa inaongoza ligi ya NBC Premier League
Pedro Goncalves afutwa kazi Yanga SC rasmi leo Mei 6, 2026. Pedro alikuwa ni Kocha Mkuu wa Yanga SC ambaye alichukua mikoba ya Romain Folz. Mchezo wa mwisho kukaa benchi ubao wa Uwanja wa KMC Complex umesoma KMC FC 0-1 Yanga SC.
SOMA HII: Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? | Mabosi wakutana kufanya tathimini
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Pedro Goncalves afutwa kazi Yanga SC

Haraka mno Pedro Goncalves afutwa kazi Yanga SC muda mfupi baada ya mchezo wa 21 ndani ya NBC Premier League. Katika mchezo wa leo alishuhudia wachezaji wakipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya KMC FC wakiwa ugenini.
Pedro raia wa Ureno ana umri wa miaka 50. Ni muumini katika kucheza kwa kushambulia na kujilinda kwenye kusaka ushindi. Kocha huyo amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Angola kwa sasa yupo huru kujiunga na timu nyingine.
Goli la ushindi limefungwa na Allan Okello mwenye miaka 25 huyu ni raia wa Uganda. Mbali na kufunga amechaguliwa kuwa Man of the Match katika mchezo huo. Unakuwa ni mchezo wake wa mwisho kuanza kikosi cha kwanza chini ya Pedro.
SOMA HII: Yanga SC itafungwa na nani 2025/26 NBC Premier League? | Matokeo na msimamo | SportPesa Blog

Taarifa kutoka Yanga SC kuhusu Pedro

“Uongozi wa Klabu ya Yanga SC unapenda kuutarifu umma kuwa umemfuta kazi Kocha Mkuu Pedro Goncalves. Uongozo unamshukuru kocha Pedro Goncalves kwa mchango wake alioutoa ndani ya klabu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.
“Katika kipindi hiki kikosi kitakuwa chini ya uongozi wa kocha Abdihamid Moalin na kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mtendaji Mkuu.
SOMA HII: Steve Barker ameshinda taji la kwanza Simba SC | Tuzo, takwimu | SportPesa Blog
Hitimisho
Pedro Goncalves afutwa kazi Yanga SC na mchezo wake uliopita alivuna pointi moja kwa kufungana 2-2 Simba SC. Huyu alikuwa ni mrithi mikoba ya Romain Folz ambaye naye alifutwa kazi. Kocha huyo alipoteza fainali ya Muungano Cup kwa kufungwa goli 1-0 Simba SC, New Amaan Complex.

