Ali KamweAli Kamwe
  • Yanga SC yapigwa faini nzito na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kwa matukio ya uvunjifu wa kanuni kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Simba SC.
  • Katika mchezo huo ulioisha kwa matokeo ya sare ya Simba SC 2-2 Yanga SC, matukio mbalimbali ya uvunjifu wa kanuni yaliripotiwa, na kupelekea adhabu hiyo.
  • Ikumbukwe mchezo huo namba 169 wa Ligi Kuu Bara, ulipigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
  • Uongozi wa Yanga SC nao umejibu mapigo, kwa kuanzisha harambee ya kuchangia kulipa faini hiyo.

Yanga SC yapigwa faini nzito na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kufuatia matukio ya uvunjifu wa kanuni yaliyotokea kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Simba SC. Ikumbukwe mchezo huo namba 169 wa Ligi Kuu Bara, ulipigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Katika mchezo huo ulioisha kwa matokeo ya sare ya Simba SC 2-2 Yanga SC, matukio mbalimbali ya uvunjifu wa kanuni yaliripotiwa, na kupelekea adhabu hiyo. Uongozi wa Yanga SC nao umejibu kwa kuanzisha harambee ya kuchangia kulipa faini hiyo.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.

Taarifa ya TPLB kuhusu Yanga SC kupigwa faini

Nyumba waliyotumia Yanga SC
Nyumba waliyotumia Yanga SC

Uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), leo Jumatatu 11/5/2026 umetoa taarifa ifuatayo;

“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,

“Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Mei 9, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC

Mechi Namba 169: Simba SC 2-2 Young Africans

“Klabu ya Young Africans imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam kuelekea mchezo tajwa hapo juu Mei 3, 2026. Young Africans iliwasili uwanjani saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri, jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

“Young Africans imetozwa faini ya Sh. 30,000,000 (milioni thelathini), kwa kosa la wachezaji na maofisa wake wa ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvulia kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Badala yake walitumia nyumba iliyo nje ya uwanja upande wa pili wa Barabara, kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 27:7 ya Ligi Kuu kuhusu Vyombo vya Maamuzi.”

SOMA HII PIA: Yanga SC na maajabu 2025/26 | Matokeo ya hivi punde, wafungaji na msimamo NBC Premier League

Meneja naye apigwa rungu

Meneja Yanga SC
Meneja Yanga SC

Taarifa hiyo imemtia hatiani Meneja Habari na mawasiliano wa Yanga SC, Walter Harson ambapo imeeleza: “Meneja wa Klabu ya Young Africans Walter Harson amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja), kwa kosa la kumsukuma mchezaji wa Simba Clatous Chama kwenye mchezo tajwa hapo juu. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha na Maofisa Wengine wa Ufundi.”

Shabiki naye afungiwa kuingia uwanjani Mwaka mzima

Taarifa ya Bodi ya Ligi pia imemtia hatiani na kumfungia aliyetambuliwa kama shabiki wa klabu hiyo ambapo taarifa ilieleza: “Shabiki wa klabu ya Young Africans aliyetambulika kwa jina la Mohamed Ally Mposo, ambaye amekuwa akiambatana na maofisa wa ufundi wa klabu hiyo amefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12. Adhabu hii kwa kosa la kuingia kwenye eneo la kuchezea wakati wa mapumziko, na kumwaga vimiminika kitendo kilichotafsiriwa kama imani za kishirikina. Adhabu hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 47:2 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.”

SOMA HII ZAIDI: Jonathan Sowah na Allasane Kante wa Simba SC wafungiwa mechi 5/ Yanga SC wapigwa rungu na TPLB

Yanga SC yapigwa faini, Ali Kamwe ajibu mapigo na harambee ya ‘Jumba la Maajabu’

Simba SC 2-2 Yanga SC
Tukio la Gueye

Wakati Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ikitoa adhabu hizo, uongozi wa klabu ya Yanga SC umejibu mapigo. Hii ni baada ya Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe kuongoza harambee ya kulipa fedha hizo ambayo wameipa jina la Jumba la Maajabu. Harambee hiyo inalenga kuchangisha fedha za kulipa adhabu ya faini iliyotolewa.

Hitimisho

TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA

Yanga SC kupigwa faini inaonyesha uthabiti wa uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), kusimamia miongozo ya kikanuni kwa timu zote. Yanga SC na Simba SC mara nyingi wamekuwa vinara wa uvunjifu wa kanuni hizi za ligi, kwa kisingizio cha imani zisizo za kimichezo. Ifike wakati viongozi wa timu zetu waendeshe soka kisasa, na kuachana na Imani zisizo za kisoka.

SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto | Mechi 5 NBC Premier League ugenini | Msimamo, matokeo

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.