Yanga SC wanaanza mabadiliko leoAli Kamwe
  • Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves, ni taarifa iliyotarajiwa, lakini imeshtua wengi.
  • Hii ni kutokana na mwenendo na takwimu za timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara (NBC Premier League).
  • Je, matokeo ya mechi 3 hizi; Yanga SC 0-0 Simba SC Machi 1, 2026, Yanga SC 0-1 Simba SC Aprili 29,2026 na Simba SC 2-2 Yanga SC Mei 3, 2026 yamechangia?
  • Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe wametaja na kueleza sababu 4 za kumfukuza kazi kocha Pedro.

Baada ya jana Jumatano 6/5/2026 Uongozi wa Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves, hatimaye leo Alhamisi uongozi wa timu hiyo umetaja sababu 4 zilizopelekea uamuzi huo. Ikumbukwe, Pedro alipokea mikoba ya kuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC baada ya kuondoshwa kwa kocha, Romain Folz. Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe wametaja na kueleza sababu mbalimbali za kumfukuza kazi kocha Pedro. Makala hii inachambua kwa ufupi sababu hizo.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu Bara ‘NBC Premier League’ 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.

Taarifa ya Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves

TAARIFA YA YANGA SC KWA UMMA
TAARIFA YA YANGA SC KWA UMMA

Muda mfupi baada ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC walitoa taarifa kwa Umma kutoka Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa klabu, Andre Mtine iliyoeleza: “Uongozi wa klabu ya Yanga SC unapenda kuutarifu Umma kuwa umemfuta kazi Kocha Mkuu Pedro Goncalves. Uongozi unamshukuru kocha Pedro Goncalves kwa mchango wake alioutoa ndani ya klabu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo. Katika kipindi hiki kikosi kitakuwa chini ya uongozi wa kocha Abdihamid Moalin na kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.”

SOMA HII PIA: Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? | Mabosi wakutana kufanya tathimini

Hizi hapa sababu 4 za kumfukuza kocha Pedro Goncalves kutoka kwa Ali Kmawe

Akizungumzia uamuzi huo wa Uongozi wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema: “Nimepigiwa simu nyingi, nimepata meseji nyingi. Waandishi wa habari wamekuwa wakiuliza, timu tumeona inaongoza Ligi kwa peno la pointi 5.

“Mmefunga magoli mengi zaidi, mmefungwa magoli machache zaidi, na kama haitoshi Yanga ni unbeaten mpaka sasa hivi ni kitu gani kimefanya mmemuondoa kocha Pedro Goncalves? Zipo sababu kadhaa kama ifuatavyo;

1. Tathimini ya uongozi

Yanga SC itafungwa na nani 2025/26
Dube na De Reuck

Kamwe amesema: “Uongozi umefanya tathmini ya mwenendo wa timu, mwenendo wa timu kama Yanga sio matokeo peke yake, sio idadi ya pointi peke yake, sio idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa peke yake. Ukisikia mwenendo wa timu kama Yanga SC unakusanya mambo mengi sana ndani yake. kuna ‘performance analysis’ yaani sawa tumeshinda, ila tumeshindaje shindaje?

“Kweli tunashinda, lakini tunashinda huku mioyo inadunda, Viongozi wamefanya tathmini na wamegundua kwamba mwenendo wa timu hauridhishi. Hii imeonekana katika baadhi ya michezo ambayo tumecheza. Uongozi ukaona uchukue hatua.”

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

2. ‘Team Management’

Kocha Pedro Goncalves
Kocha Pedro Goncalves

Kamwe aliendelea kusema: “Eneo jingine ambalo limefanya tufikie uamuzi huu ni namna ambavyo kocha alikuwa akiiongoza timu. Vitu kama ari ya timu, mbinu za kiufundi na vingine viliangaliwa, ikaonekana kunahitaji mabadiliko. Tathimi nii ilifanyika kwa ujumla.”

3. Maslahi mapana ya timu

“Yanga SC ni timu ambayo inaamini katika mafanikio, wapo ambao wameanza kusema tumefukuza makocha wengi ndani ya muda mfupi. Lakini nataka niwajibu kuwa, haijalishi ni makucha wangapi wataondoka, uongozi wa Yanga SC hautasita kumfuta kocha kazi ikiwa tu ni kwa maslahi ya timu. Uongozi unaangalia mafanikio yako wapi? Makombe yako wapi?”

SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto | Mechi 5 NBC Premier League ugenini | Msimamo, matokeo

4. Matokeo dhidi ya Simba SC

Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves
Chama akifunga bao vs Yanga SC

“Ukiangalia watani wetu kwa sasa wanaonekana kuwa na furaha, timu kubwa kama Yanga SC sio ya kusubiri ufungwe ndo usawazishe. Sisi tunapaswa kunusa hatari na kuwa wa kwanza kuiondoa, ikiwezekana sisi tufunge mpinzani asawazishe,” amesema Ali Kamwe. Ikumbukwe Yanga SC chini ya kocha, Goncalves katika mechi zao tatu zilizopita matokeo yalikuwa Yanga SC 0-0 Simba SC Machi 1, 2026, Yanga SC 0-1 Simba SC Aprili 29,2026 na Simba SC 2-2 Yanga SC Mei 3, 2026.

Nani kocha mkuu mpya Yanga SC?

Yanga SC Abdihamid Moalin
Source: Instagram.com

Kuhusiana na swali hili, Ali Kamwe amesema: “Baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC, Pedro Goncalves kufutwa kazi. Makocha, Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi watafanya kazi kama ‘Co-Headcoaches’ yaani wote wawili watakuwa makocha wakuu wa timu yetu. Kocha msaidizi atasalia, Matthew Silva ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Pedro.”

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC vs Simba SC uso kwa uso Fainali Muungano Cup 2026 | h2h, Ratiba, Matokeo, Takwimu

Hitimisho

Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves kumefungua ukurasa mpya kwa makocha, Moalin na Mabedi. Makocha hao kila mmoja kwa nyakati tofauti, waliwahi kuiongoza Yanga SC kwa mafanikio. Swali ni je, uamuzi wa Yanga SC kumfukuza kocha Pedro Goncalves utaleta matokeo gani kwenye timu, hasa wakati huu wakipambana kutetea ubingwa wao?

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.