Yanga SC vs Singida Black StarsMoallins na Patrick
  • Yanga SC (3) vs Coastal Union (0) NBC Premier League Mei 9, 2026 Uwanja wa KMC Complex
  • Moallins kufanya maboresho zaidi kwa kikosi kuelekea mechi zijazo za ushindani
  • Allan Okello kiungo mshambuliaji raia wa Uganda afunga magoli mawili na kutwaa tuzo
  • Yanga SC Unbeaten mechi 22

Yanga SC (3) vs Coastal Union (0) ni matokeo ya mchezo wa NBC Premier League, Mei 9,2026. Ahamid Moallins na Patrick Mabedi ni mara ya kwanza kuongoza kikosi baada ya kurithi mikoba ya Pedro Goncalves. Allan Okello raia wa Uganda alifunga magoli mawili dakika ya 17 na 62, Maxi Nzengeli alifunga goli moja dakika ya 64. Ushindi huo unawafanya mabingwa hao watetezi kuzidi kuwa kileleni na pointi 54.

SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Yanga SC (3) vs Coastal Union (0) Moallins kufanya maboresho zaidi

Yanga SC (3) vs Coastal Union (0)
Allan Okello

Licha ya Yanga SC (3) vs Coastal Union (0) mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Moallins amesema atafanya maboresho zaidi. Wananchi wanafikisha jumla ya mechi 22 bila kupoteza wakiwaacha watani zao wa jadi kwa tofauti ya pointi 5. Kocha huyo ameongeza kwamba kila mchezaji anafanya kazi nzuri uwanjani.

“Nimefurahishwa na uwezo wa wachezaji katika dakika zote 90. Kuna maboresho ambayo yanapaswa kufanyika hilo tutafanyia kazi. Bado tuna mechi nyingi zakucheza hivyo tutakuwa na muda katika uwanja wa mazoezi,” alisema Moallins.

SOMA HII: Yanga SC bado ipo kazini, ratiba ya NBC Premier League, msimamo wa 5 bora

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Allan Okello atwaa tuzo ya Man of the Match

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Allan Okello atwaa tuzo ya Man of the Match kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Hii inakuwa tuzo yake ya pili kuitwaa ndani ya Mei. Alianza kwenye mchezo dhidi ya KMC FC uliochezwa Mei 6, 2026.

Katika mchezo dhidi ya wakusanya mapato, Allan Okello raia wa Uganda alifunga goli pekee la ushindi dakika ya 65. Mchezo dhidi ya Coastal Union alifunga magoli mawili. Kwenye mechi mbili nyota huyo kafunga jumla ya magoli matatu akitwaa tuzo mbili mfululizo ndani ya NBC Premier League.

Unbeaten ya Yanga SC bado inadunda

Yanga SC (3) vs Coastal Union (0)
Wachezaji wa Yanga SC.

Unbeaten ya mabingwa watetezi inaendelea kudunda mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Coastal Union. Huu ni mchezo wa 22 kwa Yanga SC 2025/26 kucheza bila kupoteza. Ni mechi 6 walipata sare huku wakishinda mara 16 wanaogoza ligi wakiwa na pointi 49.

Azam FC ilikuwa inakimbizana na Yanga SC mwanzo wa msimu. Rekodi hiyo ilivunjwa na TRA United ilipopata ushindi wa magoli 4-1 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Wananchi wanaongoza ligi wakiwa na rekodi tamu yakutopoteza pointi tatu uwanjani.

SOMA HII: Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini | Taarifa mpya kuhusu Depu, ratiba 2025/26

Hitimisho

Yanga SC (3) vs Coastal Union (0) rekodi nyingine inaandikwa KMC Complex kwa star boy Allan Okello kufunga magoli mawili. Timu hiyo inazidi kuongeza kasi kuutetea ubingwa wake. Mchezo ujao itakuwa ni Dodoma Jiji FC vs Yanga SC ugenini. Je rekodi itaendelea kudunda?

Share this: