- Mabosi Yanga SC wakutana kwenye kikao kizito makao makuu Jangwani kufanya tathimini
- Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? Sababu zatajwa
- Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC, matokeo ya mchezo wa mwisho NBC Premier League
- Tumekosogezea matokeo ya mechi tatu zilizopita Yanga SC ndani ya ligi
Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? Tetesi zimekuwa zikieleza hivyo. Hii inatokana na mwendo wa timu katika mechi za NBC Premier League. Kwenye mechi tatu mfululizo Yanga SC ilishindwa kupata ushindi.
SOMA HII: Taarifa mpya Depu na Boka wa Yanga SC haifurahishi/ Orodha ya wachezaji majeruhi
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? Sababu hii hapa

Je Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? Tetesi zimekuwa zikieleza kuwa muda wowote huenda akafungashiwa virago. Matokeo ya mechi tatu mfululizo ndani ya NBC Premier League bila matokeo mazuri. Licha ya kushindwa kupata ushindi inatajwa kuna baadhi ya wachezaji hawapewi nafasi.
Taarifa zinaeleza Pedro raia wa Ureno mwenye miaka 50 amekuwa kwenye mwendelezo wa kusuasua katika mechi za karibuni. Katika mechi tatu mfululizo Yanga SC safu ya ushambuliaji imefunga goli moja. Ukuta wa timu hiyo umeruhusu goli moja.
SOMA HII: Mtibwa Sugar watibua mabadiliko Yanga SC / Mhesa na Pacome goal 2025/26 / Highlights, standings

Uchovu wa wachezaji, ubora wa viwanja, kikwazo ushindi Yanga SC
Kocha huyo hivi karibuni aliweka wazi kuwa sababu yakushindwa kupata matokeo ni uchovu wa wachezaji. Aliongeza kwa kubainisha kuwa wamekuwa wakicheza katika viwanja ambavyo sio rafiki jambo. Pedro alibainisha kuwa vipo viwanja vingine ambavyo vilikuwa vizuri na vingine vilikuwa ni vibaya.
“Jambo lingine muhimu ni ubora wa viwanja. Kuna tofauti kubwa unapocheza kwenye uwanja wenye ubora mzuri na ule usio na hali nzuri. Katika baadhi ya michezo ikiwemo wa mwisho, timu zote zilipata ugumu kutokana na hali ya uwanja jambo lililoathiri umakini na umaliziaji.
” Katika michezo yetu ya hivi karibuni mingi imekuwa ya ugenini mara nyingi katika mazingira magumu. Mfano mzuri wa kiwango chetu ugenini ulikuwa mchezo wa Singida Black Stars, ambapo tulicheza kwenye uwanja mzuri uliotuwezesha kucheza soka bora zaidi.
“Ikiwa tunataka kuinua kiwango cha soka ni muhimu pia kuboresha viwanja. Hata hivyo, tunapaswa kuendana na hali na kutafuta njia za kuwazidi wapinzani wetu,” alisema Pedro, Machi 20, 2026 katika mkutano wa Waandishi wa Habari kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika mchezo huo Yanga SC iligawana pointi mojamoja na wenyeji. Mtibwa Sugar walifunga goli dakika ya 90+2 kupitia kwa Ismail Mhesa. Yanga SC walianza kufunga kupitia kwa Pacome.
Mabosi wakutana Jangwani leo kikao kizito

Mabosi wa Yanga SC leo Machi 23, 2026 wamekutana makao makuu ya klabu, mitaa ya Jwangwani, Kariakoo. Agenda kuu ni kufanya tathimini ya timu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa NBC Premier League.
Uongozi wa timu ukiongozwa na Rais Injinia Hersi Said umekutana kwa kikao maalumu. Pia makamu Arafat naye amewasili kwenye kikao hicho. Taarifa zinaeleza kuwa mbali na kujadili mwendo wa timu watamjadili na kocha Pedro ambaye naye yupo kwenye kikao na benchi lake la ufundi.
Matokeo ya mechi 3 za NBC Premier League Yanga SC
Azam FC 0-0 Yanga SC, Machi 15, 2026, Uwanja wa Benjamini Mkapa
TRA United 0-0 Yanga SC, Machi 18, 2026, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC, Machi 21, 2026, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma
SOMA HII: Azam FC 0-0 Yanga SC Dar Derby/ Highlights, standings, statics

Hitimisho
Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? Ni swali ambalo jibu lake halijapatikana bado. Mabosi wa timu hiyo bado hawajatoa taarifa rasmi. Kocha huyo alichukua mikoba ya Romain Folz ambaye alitimuliwa alitangazwa Oktoba 25, 2025.

