Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0)Abraham Morice
  • Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0) NBC Premier League, KMC Complex
  • Clatous Chama Man of the Match
  • Seleman Mwalimu akosa penati dakika ya 10 na kufunga goli dakika ya 43

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0) ni matokeo rasmi ya NBC Premier League Mei 11, 2026. Magoli yamefungwa na Morice Abraham dakika ya 27, Clatous Chama dakika ya 41, Seleman Mwalimu dakika ya 43 na Ismail Traore dakika ya 61. Ushindi huo unamfanya mnyama kufikisha pointi 49 nafasi ya pili kwenye msimamo.

SOMA HII: Usajili wa Simba SC dirisha dogo 2025/26 balaa! Gueye, Kibabage, Loemba

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako sasa, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0) NBC Premier League

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0)
Simba SC vs Tanzania Prisons

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0) mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Mwenge. Hii ni mara ya kwanza ndani ya msimu mnyama kucheza hapo awali alikuwa anatumia Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo, Mbweni. Ikumbukwe kwamba hata mchezo wa Kariakoo Dabi, Mei 3 ulipigwa huko matokeo yakiwa Simba SC 2-2 Yanga SC.

Mchezo uliopita kwa Simba SC ilipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya JKT Tanzania. Mfungaji alikuwa ni Clatous Chama na alichaguliwa kuwa Man of the Match. Mchezo wa kwanza kucheza wakiwa KMC Complex wamepata ushindi wa magoli 4-0 Tanzania Prisons.

Seleman Mwalimu alikosa penati dakika ya 10 iliyosababishwa na Anthony Mligo. Mshambuliaji huyo alipewa jukumu hilo licha ya kumpoteza mlinda mlango Mussa Mbissa alipaisha mpira. Dakika ya 43 alifunga goli moja hali iliyopeleka dakika 45 za mwanzo ubao kusoma Simba SC 3-0 Tanzania Prisons.

SOMA HII: Simba SC 2-2 Yanga SC: Matukio 6 ya ajabu yaliyotokea, NBC Premier League, matokeo na Takwimu | SportPesa Blog

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Clatous Chama Man of the Match KMC Complex

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0)
Chama Clatous

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama ametwaa tuzo ya Man of the Match mara baada ya mchezo. Mwamba wa Lusaka alifunga goli moja katika mchezo huo alikuwa kwenye ubora. Inakuwa ni tuzo yake ya tatu mfululizo kwenye mechi za Mei.

Alianza kukusanya tuzo Simba SC 2-2 Yanga SC, hapa alifunga goli moja na pasi moja ya goli. Simba SC 1-0 JKT Tanzania alifunga goli la ushindi. Simba SC 4-0 Tanzania Prisons alifunga goli moja na kutoa pasi moja ya goli kwa Traore kupitia pigo la kona.

Katika mechi 3 ambazo ni dakika 270, Chama amefunga magoli matatu na pasi mbili za magoli kati ya 7 ambayo yamefungwa. Mchezaji huyo amekuwa kwenye ubora mechi za mzunguko wa pili. Ikumbukwe kwamba ni ingizo jipya katika dirisha dogo akitokea Singida Black Stars.

Ahmed Ally amchambua Clatous Chama

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema Chama ni mchezaji mwenye ubora mkubwa. Aliongeza kuwa mara baada yakufunga dhidi ya Yanga SC amezidi kuwachanganya wengi. Alibainisha kuwa magoli anayofunga yanawachanganya mpaka FIFA.

“Clatous Chama anatuchanganya kabisa kwenye kila mechi. Sio Simba SC pekee bali mpaka FIFA anawachanganya kutokana na uwezo wake. Anafunga magoli mazuri yanayofurahisha. Tunaamini ataendelea kuwa kwenye ubora huu mechi zote,” alisema Ahmed.

SOMA HII: Kariakoo Dabi-Goli la Clatous Chama gumzo kubwa | Ahmed Ally atamba | SportPesa Blog

Hitimisho

Simba SC (4) vs Tanzania Prisons (0) pointi tatu zinabaki unyamani. Matokeo haya yanaendeleza mbio za kuwania ubingwa uliopo mikononi mwa Yanga SC. Tofauti ni pointi 5 kwa wababe hawa wawili kila mmoja akicheza mechi 22. Endelea kufuatilia blog ya SportPesa kwa matokeo na taarifa zaidi.

Share this: