- KMC FC 0-1 Yanga SC NBC Premier League 2025/26, Uwanja wa KMC Complex
- Allan Okello raia wa Uganda afunga goli la ushindi na kuwa Man of the Match
- Pedro Goncalves fukuto la kufutwa kazi linaendelea kumuandama
KMC FC 0-1 Yanga SC NBC Premier League matokeo rasmi mchezo wa leo Mei 6. 2026, Uwanja wa KMC Complex. Goli la ushindi limefungwa na Allen Okello dakika ya 65. Wananchi wameendeleza ubabe mbele ya wakusanya mapato baada ya mzunguko wa kwanza kupata ushindi wa magoli 4-1.
SOMA HII:Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

KMC FC 0-1 Yanga SC NBC Premier League

Mwisho wa dakika 90 KMC FC 0-1 Yanga SC NBC Premier League. Dakika 45 za mwanzo wababe hawa wawili hakuna aliyepata goli ilikuwa 0-0. Ushindi huu unaiongezea ufalme Yanga SC nafasi ya kwanza ikifikisha pointi 51.
Okello amechaguliwa kuwa Man of the Match mara baada ya mchezo. Kiungo huyo raia wa Uganda amekuwa kwenye kiwango bora katika mechi za hivi karibu. Leo alianza kikosi cha kwanza na alitumia dakika 90 nafasi yake ilichukuliwa na Sure Boy.
Matokeo haya yanazidi kuididimiza KMC FC katika msimamo ikiwa mkiani. Pointi zake 9 baada ya mechi 21 imepata ushindi kwenye mechi mbili pekee. Huu unakuwa mchezo wa 16 kupoteza ndani ya NBC Premier League.
SOMA HII: Kariakoo Dabi-Goli la Clatous Chama gumzo kubwa | Ahmed Ally atamba | SportPesa Blog

Pedro Goncalves akalia kuti kavu
Mara baada ya mchezo mashabiki walikuwa wakimzomea Kocha Mkuu, Pedro Goncalves. Hii inatokana na kile walichodai kutofurahishwa na matokeo ya timu hiyo. Licha ya ushindi bado walikuwa wakimtaka awaachie timu yao wakimfuata rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said.
| Takwimu | KMC FC | Yanga SC |
|---|---|---|
| Umiliki wa mpira (%) | 43 | 57 |
| Magoli | 0 | 1 |
| Kona | 1 | 6 |
| Kadi za njano | 1 | 1 |
| Kadi nyekundu | 0 | 0 |
| Mashuti yaliyolenga lango | 3 | 6 |
| Mashuti yasiyolenga lango | 1 | 6 |
Yanga SC kwenye mchezo wa leo wamekuwa na umiliki mkubwa ndani ya dakika 90. Walifanya mashambulizi mengi zaidi na kupata goli 1. KMC FC walicheza kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.
SOMA HII: Wachezaji wanne wa Yanga SC warejea kazini | Taarifa mpya kuhusu Depu, ratiba 2025/26
Hitimisho
KMC FC 0-1 Yanga SC NBC Premier League dakika 90 zimekamilika ushindi ukienda kwa wageni. Pedro Goncalves alianza kwa mbinu ya 4-4-2 na KMC FC walikuwa na mpago kazi wa 4-3-3. Wakusanya mapato wamepoteza nje ndani mbele ya mabingwa watetezi msimu wa 2025/26.

