- Karibu tena nyumbani! Ujumbe wa Yanga SC kwa kocha atakayefanya kazi na Pedro Goncalves
- Kocha mpya Yanga SC Abdihamid Moalin ametangazwa kurejea Jangwani, uzoefu na makombe
- Maazimio ya mabingwa watetezi kuleta mapinduzi mzunguko wa pili 2025/26
- Ripoti yawataja wachezaji 8 majeruhi tengemeo akiwemo Clement Mzize, Depu, Prince Dube
Kocha mpya Yanga SC Abdihamid Moalin ametangazwa rasmi kurejea nyumbani akiwa ni msaidizi. Kocha ana mafanikio kwa kutwaa ubingwa wa NBC ana uzoefu katika soka la Bongo. Timu ya kwanza kumleta ndani ya ligi ni Azam FC. Atashirikiana na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves mzunguko wa pili.
SOMA HII: Kocha mpya Yanga SC huyu hapa, kuiwahi mechi ya Yanga SC vs Silver Strikers Jumamosi?
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Umecheza na hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kocha mpya Yanga SC Abdihamid Moalin kwa nini amerejea?

Uongozi umetangaza ujio wa Kocha mpya Yanga SC Abdihamid Moalin kurejea kwa mara nyingine. Sababu kubwa ni tathimini ambayo wameifanya kwa mechi za mzunguko wa kwanza 2025/26. Katika kikao rasmi cha Machi 23,2026 kiliamua hayo yote.
Kwenye kikao hicho kiliongozwa na Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said. Viongozi wengine walikuwepo Makamu wa Rais Arafat, Meneja wa Idara ya Habari Ali Kamwe. Ni makao makuu Jangwani, maamuzi hayo yalifanyika.
Mafanikio ya Moalin

Abdihamid Moalin ni kocha msaidizi ambaye atakuwa benchi akisaidina na kocha Pedro Goncalves. Moalin amewahi kufanya kazi Yanga SC 2024/25 chini ya Kocha Mkuu, Sead Ramovic na Miloud Hamdi na alipata mafanikio ya kushinda taji la ligi ya NBC 2024/25. Wakati huo ndani ya Yanga SC alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Ufundi.
Taji jingine ambalo alitwaa akiwa na Yanga SC ni CRDB Federation Cup 2025 na Muungano 2025. Hivyo ni miongoni mwa makocha ambao wanambinu za ushindi. Wananchi ni mabingwa watetezi wa taji la NBC Premier League.
Uzoefu na ligi ya Bongo
Abdihamid Moalin ameinoa Azam FC msimu wa 2021/22, kisha akainoa KMC FC 2024/25 na kupewa majukumu ndani ya kikosi cha Yanga SC 2024/25, anarejea kwa mara nyingine 2025/26.
Ni raia wa Marekani
Moalin ni raia wa Somalia kiasili akiwa na uraia wa Marekani. Wakati anakuja Azam FC alitokea Marekani. Alipokuja Azam FC alianza majukumu kwenye eneo la Mkurugenzi wa Ufundi Azam FC kisha akapewa majukumu kuinoa Azam FC.
Maamuzi ya uongozi Yanga SC haya hapa
Taarifa rasmi kutoka Yanga SC imeeleza kuwa uongozi mara baada ya kukutana Machi 23 2026 katika kikao cha tathimini ya mzunguko wa kwanza wamekuja na maazimio kuhakikisha wanaendelea kupambana mzunguko wa pili.
SOMA HII: Pedro Goncalves kufukuzwa Yanga SC? | Mabosi wakutana kufanya tathimini

Pedro Goncalves akabidhi ripoti

Kwenye kikao hicho uongozi ulipokea ripoti kutoka kwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves. Ripoti ilionyesha takwimu nzuri kwa mzunguko wa kwanza. Yanga SC imecheza mechi 16, ushindi mechi 11, sare 5 na haijapoteza mchezo.
Yanga SC ni timu namba moja kufunga magoli mengi ambayo ni 32 na imeruhusu magoli 3 kufungwa. Ripoti imebainisha changamoto zifuatazo:-
1. Ratiba ndani ya siku 21 timu ilicheza mechi 7 mfululizo, 6 NBC Premier League na moja mchezo wa CRDB Federation Cup. Timu hiyo ilisafiri umbali wa kilomita 4,462 kwa mechi za ugenini.
2. Timu ina wachezaji 8 muhimu ambao wamepata majeraha akiwemo Khomein Aboubakar. Clement Mzize, Dickson Job, Ibrahim Bacca. Chadrack Boka, Edmund John, Prince Dube na Laurindo Maria, ‘Depu’.
SOMA HII: Usajili wa Yanga SC orodha ya wapya 11 msimu wa 2025/26 | Rekodi, magoli na timu walizotoka

Hitimisho
Kocha mpya Yanga SC Abdihamid Moalin CV yake inaonyesha uzoefu alionao na soka la Tanzania. Kurejea kwa mara nyingine kutakuwa na matokeo chanya? Ni swali ambalo litajibiwa kwa vitendo kwenye mechi zijazo za ushindani.

