Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoliOkelo (-)
  • Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli Muungano Cup fainali 2026, Uwanja wa New Amaan Complex
  • Kariakoo Dabi kutoka ligi namba 6 kwa ubora Afrika
  • Yanga SC kuwakocha wawili Zimbwe Jr na Buba Jammeh

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli Muungano Cup fainali ipo pande zote mbili. Mchezo unatarajiwa kupigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Aprili 29, 2026. Prince Dube kutoka kwa mabingwa watetezi na Seleman Mwalimu ambaye ni mnyama watakuwa kwenye vita saa 2:15 usiku.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC uso kwa uso Fainali Muungano Cup 2026 | h2h, Ratiba, Matokeo, Takwimu

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli, nani atashinda?

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli
Prince Dube kinara wa ufungaji Muungano Cup 2026.

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli inatarajiwa kuwa vitani kusaka ushindi. Dube anaongoza katika wafungaji akiwa nayo matatu kwa Yanga SC. Seleman yeye amefunga magoli mawili upande wa Simba SC.

Wenyeji watakosa huduma za wachezaji wawili, Zimbwe Jr na Buba Jammeh. Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Pedro Goncalves amebainisha hawa hawapo fiti. Licha ya kukosekana wachezaji hao Yanga SC wapo kamili kwa Kariakoo Dabi kutoka ligi namba 6 kwa ubora Afrika.

Mitambo ya magoli Yanga SC

MchezajiMagoliTimu alizofungaAsistiTimu alizotoa asisti
Prince Dube3Muembe Makumbi (2), Azam FC (1)1Azam FC
Maxi Nzengeli1Azam FC0
Shekhan Khamis2Muembe Makumbi (2)0
Allen Okello02Muembe Makumbi, Azam FC

Kinara wa ufungaji ni Prince Dube akifunga magoli mawili. Kwenye upande wa Asisti Okelo anaongoza akiwa nazo mbili. Juma mabingwa watetezi wamefunga magoli 6 katika mechi mbili.

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Mitambo ya magoli Simba SC

MchezajiMagoliTimu alizofungaAsistiTimu alizotoa asisti
Seleman Mwalimu2Mafunzo FC (1), Mlandege FC (1)0
Neo Maema1Mlandege FC0
Anicet Oura1Mlandege FC1Mlandege FC
Clatous Chama02Mlandege FC

Simba SC kinara wa ufungaji ni Seleman Mwalimu akiwa nayo magoli mawili. Mkali wa kutengeneza pasi za mwisho ni Clatous Chama akiwa nazo mbili. Baada ya mechi mbili, mnyama amefunga magoli manne ndani ya dakika 180.

Fainali inatarajiwa kuwakutanisha wawili hawa ndani ya New Amaan Complex. Steve Berkar anakiongoza kikosi cha Simba SC. Mbinu zake zitapambana na Pedro Goncalves mchezo wa fainali.

Matokeo Muungano Cup 2026

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Simba SC.
TimuTareheMechiHatuaMatokeo
Yanga SCAprili 21, 2026Yanga SC vs Muembe MakumbiRobo fainaliYanga SC 4-0 Muembe Makumbi
Aprili 25, 2026Yanga SC vs Azam FCNusu fainaliYanga SC 2-1 Azam FC
Azam FCAprili 22, 2026KVZ vs Azam FCRobo fainaliKVZ 0-2 Azam FC
Aprili 25, 2026Yanga SC vs Azam FCNusu fainaliYanga SC 2-1 Azam FC
Simba SCAprili 23, 2026Simba SC vs Mafunzo SCRobo fainaliSimba SC 1-0 Mafunzo SC
Aprili 26, 2026Mlandege FC vs Simba SCNusu fainaliMlandege FC 0-3 Simba SC
Mlandege FCAprili 23, 2026Mlandege FC vs Singida Black StarsRobo fainaliMlandege FC 2-1 Singida Black Stars
Aprili 26, 2026Mlandege FC vs Simba SCNusu fainaliMlandege FC 0-3 Simba SC

SOMA HII: Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) Muungano Cup 2026 | Highlights, magoli, H2H| Kisasi kimelipwa

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli inatarajiwa kuwa kazini. Mabingwa watetezi watakabiliana na mnyama. Hii ni Kariakoo Dabi ndani ya Zanzibar endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa matokeo na taarifa zaidi.

Share this: