Msimamo wa Ligi KuuMsimamo wa Ligi Kuu
  • Ligi Kuu ya NBC imeendelea tena leo Jumatano kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja tofauti.
  • Simba SC walikuwa wageni wa KMC kwenye Uwanja wa KMC Complex, huku Singida Black Stars wakiikaribisha Fountain Gate pale Azam Complex.
  • Mechi hizi zimebadili kabisa msimamo wa Ligi Kuu Bara, ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku Singida Black Stars nao wakishinda bao 1-0.
  • Makala hii inakuchambulia hali ya msimamo na dondoo muhimu mara baada ya mechi hizi.

Ligi Kuu ya NBC imeendelea tena leo Jumatano kwa michezo miwili kupigwa. Simba SC walikuwa wageni wa KMC kwenye Uwanja wa KMC Complex, huku Singida Black Stars wakiikaribisha Fountain Gate pale Azam Complex. Mechi hizi zimebadili msimamo wa Ligi Kuu Bara NBC, ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku Singida Black Stars nao wakiitandika Fountain Gate bao 1-0. Makala hii inakuchambulia hali ya msimamo, na dondoo muhimu mara baada ya mechi hizi.

SOMA HII ZAIDI: Umeona msimamo wa Ligi Kuu NBC: Takwimu za Yanga SC, Simba SC, JKT zashtua!

Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

aviator

Kuhusu msimamo wa Ligi Kuu Bara

Msimamo wa ligi Kuu NBC mpaka sasa, unadhihirisha kuwa msimu huu wa 2025/26 umeanza kwa ushindani mkali. Timu nyingi zimejipanga vizuri kushindana kwa nguvu zote. Mpaka baada ya mechi za leo timu ya JKT Tanzania, imeendelea kung’angania msimamo, huku timu kongwe za Yanga SC na Simba SC zikija kwa kasi.

JKT Tanzania vinara

Kikosi cha JKT Tanzania
Kikosi cha JKT Tanzania

JKT Tanzania ndio inaongoza msimamo, baada ya kukusanya pointi 27 katika michezo 15 waliyocheza. Kwa Daraja la timu yao unaweza kusema hii ni hatua kubwa, timu hiyo imeendelea kushikilia usukani kwa muda mrefu sasa. Changamoto kubwa kwao ni kuwa wamecheza michezo mingi zaidi, wakiwa na mechi 15, yaani 7 zaidi ya timu za Simba na Yanga na Singida ambao wamecheza mechi chache zaidi.

Pamba Jiji wanakimbiza mwizi kimyakimya

Tangu kuanza kwa msimu huu, Pamba Jiji imetoa ishara kuwa wanaweza kuingia katika mzunguko wa kushindania nafasi za juu. Mpaka sasa Pamba Jiji wako nafasi ya 2 na pointi zao 23 walizokusanya katika michezo 14. Nao ni miongoni mwa timu ambazo zimekaa nafasi za juu kwa muda mrefu. Hii inawafanya kuonekana wanakimbiza mwizi kimyakimya.

SOMA HII ZAIDI: Umeona msimamo wa Ligi Kuu NBC: Takwimu za Yanga SC, Simba SC, JKT zashtua!

Simba SC na Yanga SC gari limewaka

Libase Gueye - Simba SC
Libase Gueye – Simba SC

Vigogo wawili wa soka nchini Simba SC na Yanga SC zinaonekana kuzidi kuimarika baada ya kuanza msimu kwa kusuasua na kubanwa na ratiba ya mashindano ya kimataifa. Kila timu sasa inazidi kuweka nguvu kushinda mechi zake. Yanga SC mpaka sasa wanakamatia nafasi ya tatu na pointi zao 22, huku Simba wao wakikamatia nafasi ya 6 na pointi zao 19. Ikumbukwe timu hizi zimecheza mechi 8 tu.

Inatabiriwa msimamo kuwa na mabadiliko makubwa

Kutokana na uhalisia kuwa kuwa mechi ni chache ambazo zimechezwa msimu huu, hii ina maana msimamo wa Ligi Kuu Bara NBC unaweza kubadilika sana. Ni uwezekano mkubwa kuona mabadiliko makubwa. Mabadiliko haya yanatarajiwa kwa timu ambazo zina mechi nyingi za viporo.

KMC hali yao ni tete

Kikosi cha KMC wanapumulia mashine msimu huu kwani wameambulia pointi 8 tu, katika michezo 15 waliyocheza mpaka sasa. Takwimu hizo zinawafanya kuwa timu ya mwisho kwenye msimamo. Hii ni wazi inawasha kengele kwa mabosi wa timu. Tayari kumeripotiwa uwezekano wa mabadiliko ya benchi lao la ufundi.

SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 hii hapa | Mechi za Dabi, kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani

Hitimisho

Msimamo wa Ligi Kuu
Msimamo wa Ligi Kuu

Kwa kuangalia msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, utaona kuwa msimu huu wa 2025/26 unaashiria ligi itakuwa na ushindani mkubwa. Ikumbukwe Wananchi Yanga SC ndio watetezi wa kombe hili kwa mara nne mfululizo. Mpaka sasa timu kama JKT Tanzania, Young Africans, Simba, Pamba Jiji na Mashujaa FC zinaonekana kuonesha nguvu ya kushindana ubingwa. Hata hivyo, bado ni awamu ndogo ya ligi imechezwa. Hivyo mafanikio ya sasa hayahakikishi chochote ila inaweza kutoa dondoo za awali.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.