- Mlandege FC vs Simba SC ni kisasi! Ni zaidi ya mechi ya Nusu Fainali ya pili ya Muungano Cup 2026.
- Ikumbukwe hatua ya Nusu Fainali ya Muungano Cup 2026 itafikia tamati kesho Jumapili 26/4/2026, katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.
- Mshindi wa mechi hii atavaana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine inayochezwa leo Jumamosi kati ya Yanga SC vs Azam FC.
- Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana ubao wa matokeo ulisoma Mlandege FC 1-0 Simba SC 13/1/2024 katika mchezo wa Fainali ya Mapinduzi Cup.
Hatua ya Nusu Fainali ya Muungano Cup 2026 itafikia tamati kesho rasmi kesho Jumapili. Katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, itapigwa mechi kali ya kisasi! Ni Mlandege FC vs Simba SC Nusu Fainali ya pili ya mashindano haya. Mshindi wa mechi hii atavaana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine inayochezwa leo Jumamosi kati ya Yanga SC vs Azam FC. Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana ubao wa matokeo ulisoma Mlandege FC 1-0 Simba SC 13/1/2024 katika mchezo wa Fainali ya Mapinduzi Cup.
Endelea kufuatilia mwenendo ya mashindano ya Muungano Cup 2026 na mashindano mengine, na uweke ubashiri wako kupitia mechi za Odds kubwa kwa kubonyeza wino huu wa bluu SportPesa.
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu mechi ya Mlandege FC vs Simba SC

Mechi ya Mlandege FC vs Simba SC itapigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kesho Jumapili 26/4/2026. Mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa 2:15 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki. Mchezo huu ni wa mfumo wa mtoano, hivyo lazima mshindi apatikane ndani ya dakika 90, za nyongeza au katika changamoto za mikwaju ya Penalti. Mshindi wa jumla atakuwa amefuzu kucheza fainali ambayo inatarajiwa kupigwa 29/4/2026.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Azam FC: Muungano Cup 2026 Nusu Fainali yamoto, Ratiba, h2h, matokeo
Mlandege FC vs Simba SC h2h

Katika miaka ya hivi karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 5, mechi hizo zikiwa ni za Mashindano ya Kombe la Mapinduzi. Katika michezo hiyo mitano Simba SC wameshinda mechi 2, na Mlandege FC wameshinda mechi 2. Mchezo 1 uliosalia uliisha kwa matokeo ya Suluhu. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mchezo huu ni mgumu kwa timu zote mbili, na wa kisasi kwa kuwa Simba SC amepoteza mechi 2 mfululizo mbele ya Mlandege FC.
Takwimu hizi zimerahisishwa kupitia Jedwali hili hapa chini;
| Tarehe | Mashindano | Matokeo |
|---|---|---|
| 13 Januari 2024 | Fainali ya Kombe la Mapinduzi | Mlandege 1 – 0 Simba |
| 3 Januari 2023 | Kombe la Mapinduzi | Mlandege 1 – 0 Simba |
| 7 Januari 2022 | Kombe la Mapinduzi | Simba 0 – 0 Mlandege |
| 17 Oktoba 2020 | Mechi ya Kirafiki ya Klabu | Simba 3 – 1 Mlandege |
| 9 Januari 2019 | Kombe la Mapinduzi | Simba 1 – 0 Mlandege |
Safari ya Mlandege FC kutinga Nusu Fainali Muungano Cup 2026
Mlandege FC ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, wameingia Nusu Fainali baada ya kuicharaza Singida BS 2-1. Mchezo huo wa Robo Fainali ulipigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar Alhamisi ya Aprili 23/42026. Mbwana Samatta na Mussa Mbappe walifunga mabao ya Mlandege FC, huku Daudi Mishamo akifunga bao la Singida Black Stars FC. Ikiwa Mlandege wataichapa Simba SC katika mchezo huu, itakuwa mchezo wa 3 mfululizo Simba SC wanapoteza mbele ya Mlandege FC.
SOMA HII ZAIDI: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali
Safari ya Simba SC kutinga Nusu Fainali Muungano Cup 2026

Simba SC imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuiondosha Mafunzo SC, katika mchezo wa Robo Fainali. Katika mchezo huo wa Nusu Fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, bao pekee la Simba SC lilifungwa na mshambuliaji, Selemani Mwalimu. Ikiwa Simba SC itafuzu kucheza Fainali itavaana na mshindi kati ya Yanga SC vs Azam FC.
Mlandege FC vs Simba SC ni vita ya kisasi na heshima
Mlandege FC vs Simba SC licha ya kuwa ni mchezo wa kusaka nafasi ya Kwenda Fainali, lakini pia umebeba thamani ya vita ya heshima na kisasi kwa timu zote mbili. Mechi hii inakutanisha wababe, ambao katika mechi 5 zilizopita kila timu imemduwaza mpinzani wake na kuwafunga mara 2. Ikumbukwe Simba SC haijapata ushindi wowote dhidi ya Mlandege katika mechi 3 mfululizo, wamefungwa mara 2 na sare moja hivyo hii ni nafasi kwao kurudisha heshima.
SOMA HII ZAIDI: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo
Hitimisho

Mlandege FC vs Simba SC ni wazi utakuwa mchezo mgumu, kwa uthibitisho wa takwimu. Simba SC watakuwa na deni kubwa zaidi hasa kwa kuwa hawajaonja Ladha ya ushindi kwa Mlandege katika mechi 3 zilizopita mfululizo. Ubora wa timu zote mbili hasa ukizingatia Mlandege ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Zanzibar, unafanya mchezo huu usubiriwe kwa hamu kubwa.

