- Ni Yanga SC vs Azam FC moto utawaka Jumamosi hii ya 25/4/2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
- Huu ni mchezo mkali wa Nusu Fainali ya kwanza, ya mashindano ya Muungano Cup 2026, ambao unajulikana kama ‘Dar es Salaam Derby’.
- Ikumbukwe Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuifunga Muembe Makumbi City 4-0 katika Robo Fainali, huku Azam FC ikiicharaza KVZ FC mabao 2-0.
- Hizi hapa dondoo muhimu kuelekea mchezo huo.
Yanga SC vs Azam FC moto utawaka Jumamosi hii ya 25/4/2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Ni katika mchezo mkali wa Nusu Fainali ya kwanza, ya mashindano ya Muungano Cup 2026, ambao unajulikana kama ‘Dar es Salaam Derby’. Ikumbukwe Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuifunga Muembe Makumbi City 4-0 katika Robo Fainali, huku Azam FC ikiicharaza KVZ FC mabao 2-0. Hizi hapa dondoo muhimu kuelekea mchezo huo.
SOMA HII PIA: Yanga SC bingwa NMB Mapinduzi Cup 2026 kwa penati 5-4 Azam FC/ Highligts, stats
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu mechi ya Yanga SC vs Azam FC

Mechi hii itapigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa 2:15 usiku, kwa saa za Afrika Mashariki. Kwa kuwa mchezo huu ni wa mfumo wa mtoano, ni lazima mshindi apatikane ambapo mshindi wa jumla atakuwa amefuzu kucheza fainali. Katika Fainali hiyo watakutana na mshindi wa mechi ya Mlandege FC vs Simba SC / Mafunzo SC.
Endelea kufuatilia mwenendo ya mashindano ya Muungano Cup 2026 na mashindano mengine,na uweke ubashiri wako kupitia mechi za Odds kubwa kwa kubonyeza wino huu wa bluu SportPesa.
Yanga SC vs Azam FC h2h
Katika miaka ya hivi karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 13, mingi kati ya michezo hii ikiwa ni ya Ligi Kuu ya NBC. Yanga SC wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 7. Azam FC wao wamefanikiwa kushinda mechi 3 tu, huku mechi 3 zilizosalia zikiisha kwa sare. Mara ya mwisho kukutana ilikuwa Machi 15, 2026 mchezo ukiisha Suluhu.
Baadhi ya matokeo ya mechi zilizopita za Yanga SC vs Azam FC ;

10 April 2025 Azam FC 1-2 Yanga SC
2 Nov 2024 Yanga SC 0-1 Azam FC
17 March 2024 Azam FC 2-1 Yanga SC
23 Oct 2023 Yanga SC 3-2 Azam FC
25 Dec 2022 Azam FC 2-3 Yanga SC
6 Sep 2022 Yanga SC 2-2 Azam FC
6 April 2022 Azam FC 1-2 Yanga SC
SOMA HII ZAIDI: Dabi ya Kariakoo Yanga SC vs Simba SC ni Machi Mosi 2026/ NBC Premier League ratiba
Yanga SC vs Azam FC ni vita ya heshima na rekodi

Mchezo huu sio tu, ni vita ya kusaka tiketi ya Kwenda Fainali, bali ni vita ya heshima, historia na ubabe. Mechi hii inakutanisha wababe, ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya soka la Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni. Yanga SC wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na ari ya kujiamini, hasa kutokana na uzoefu mkubwa wa kikosi chao na wachezaji bora hasa safu yao imara ya ushambuliaji. Azam FC wao watakuwa na dhamira ya kufuta uteja kwa Yanga SC, lakini pia kujiweka katika nafasi ya kushinda ubingwa.
Timu zote mbili zinatambua kuwa ushindi katika mchezo huo utawapa nafasi ya kutwaa kombe, Pamoja na fahari ya moja ya dabi zenye ushindani mkubwa nchini. Hii inaweza kuzaa moja kati ya fainali mbili kubwa, zinazotarajiwa kwa hamu kubwa. Dabi ya Kariakoo yaani Yanga vs Simba au Dabi ya Mzizima yaani Simba SC vs Azam FC. Mechi hizi huwa na ushindani mkubwa, huku Azam wakijaribu kuvunja ubabe wa timu kongwe.
Ikiwa Azam FC, watafika fainali, itakuwa hatua muhimu ya kuthibitisha ubora wao dhidi ya vigogo wa soka la Tanzania. Uwezekano wa mechi hizi kubwa unafanya mashindano ya Muungano Cup 2026 kuwa miongoni mwa mashindano yenye msisimko mkubwa msimu huu. Mashabiki wanatarajia burudani ya hali ya juu, yenye ushindani mkali na hisia kali za soka.
SOMA HII PIA: Azam FC 0-0 Yanga SC Dar Derby/ Highlights, standings, statics
Hitimisho

Yanga SC vs Azam FC ni mchezo mgumu. Haijalishi ni katika hatua gani, au mashindano gani timu hizo zinakutana. Ubora wa timu zote mbili, unafanya mchezo huu usubiriwe kwa hamu kubwa. Ikumbukwe timu hizi zitakutana tena katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Bara mwezi Mei, mwaka huu.

