Simba SC vs Yanga SC kupigwa Uwanja wa Meja IsamuhyoLibese G
  • Simba SC vs Yanga SC joto linazidi kupanda, kuelekea mchezo mkali wa Kariakoo Dabi a Ligi Kuu Bara (NBC Premier League).
  • Mchezo huu utapigwa tarehe 3/5/2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Machi 1, 2026 ambapo ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisomeka Yanga SC 0-0 Simba SC.
  • Mashabiki wa kila timu wanatambiana ubora wa vikosi vyao, ila kwa msingi wa Takwimu hawa ni wachezaji 10 hatari kuelekea Mei 3, 2026, kuanzia kwa Pacome, Okello mpaka Gueye, Oura na Mpanzu

Joto linazidi kupanda kuelekea mchezo mkali wa Kariakoo Dabi a Ligi Kuu Bara (NBC Premier League). Ni Simba SC vs Yanga SC mchezo utakaopigwa tarehe 3/5/2026, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam. Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Machi 1, 2026 ambapo ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisomeka Yanga SC 0-0 Simba SC. Mashabiki wa kila timu wameendelea kutambiana ubora wa vikosi vyao, na kwa msingi wa Takwimu za Ligi Kuu Bara, makala hii inakuletea wachezaji 10 hatari n awa kuchungwa kuelekea Mei 3, 2026.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya NBC Premier League 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge
Paisha kindege uvune mpaka Milioni 800

Wachezaji hatari kuelekea mechi ya Simba SC vs Yanga SC

Kutoka Simba SC

Elie Mpanzu

Muungano Cup 2026
Elie Mpanzu

Nyota wa kimataifa wa Simba SC raia wa DR Congo, mwenye umri wa miaka 24 tu, akiwa ni kipenzi kikubwa cha Wanasimba. Anaichezea Simba SC kwa msimu wa 2 baada ya kujiunga nayo msimu wa 2024/2025. Licha ya kuanza vibaya msimu huu kutokana na kile alichokieleza kuwa ni changamoto za kifamilia, Nyota huyo ameanza kuwaka. Mpanzu msimu huu amehusika kwenye mabao 8, akifunga mabao 3 na kuasisti mara 5.

Anicet Oura

Huyu ni kiungo wa kimataifa wa Simba SC kutokea Ivory Coast, ambaye alikamilisha usajili wake Simba SC 26/1/2026. Kwa kipindi kifupi ndani ya Ligi Kuu Bara, Oura amejitambulisha kama mchezaji hatari na mwenye Uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi. Akiwa na siku chache kikosini, Oura tayari amehusika kwenye mabao 5 ya Simba SC akifunga mabao 3 na kuasisti mara 2, ni wazi Wananchi wanapaswa kumchunga.

SOMA HII PIA: Dabi ya Kariakoo kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo Mei 3, 2026 | TPLB wataja sababu

Libasse Gueye

Libase na Oura
Libase na Oura

Usajili mpya kutoka nchini Senegal, akiwa na umri wa miaka 22 tu, tayari ameitikisa Ligi ya Tanzania Bara (NBC Premier League). Gueye alijiunga na Simba SC rasmi Januari 17, 2026 na kusaini mkataba wa miaka 2 akitokea Teungueth FC. Silaha yake kubwa ni kasi, na mguu wake wa kushoto wenye maajabu ya chenga. Tangu ajiunge na Simba SC ameifungia timu hiyo mabao 4 muhimu na aliwatesa sana Yanga SC kwenye mchezo wa kwanza.

Selemani Mwalimu

Amejiunga na Simba msimu huu akitokea timu ya Wydad Casablanca kwa mkopo, ambapo takwimu zake sio haba. Mwalimu mpaka sasa amefanikiwa kuifungia Simba SC mabao 6, idadi inayomfanya kuwa kinara wa mabao ndani ya kikosi cha timu hiyo. Katika mchezo wa awali uliopigwa 1/3/2026 Mwalimu aliifungia Simba SC bao ambalo lilikataliwa na Mwamuzi kwa madai ya kuotea, huku baada ya mapitio bao hilo likaonekana lilikataliwa kimakosa. Yanga wanapaswa kumchunga.

SOMA HII ZAIDI: Kiungo wa Yanga SC Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC | Afungiwa mechi 3 na TPLB

Clatous Chama

Clatous Chama
Chama Clatous

Anaujua vizuri mchezo wa Kariakoo Dabi, huyu ni miongoni mwa Nyota wachache ambao wamecheza kwa mafanikio makubwa katika timu za Yanga SC na Simba SC kwa vipindi tofauti. Chama amerudi Simba SC msimu huu, akitokea Jangwani ambapo mpaka sasa amehusika kwenye mabao 5, akifunga mabao 3 na kuasisti mara 2.

Mastaa hatari wa Yanga SC

Prince dube

Kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga SC. Raia huyu wa Zimbabwe ameonekana kuwa hatari tangu aliporejea kutoka kwenye majeraha. Mpaka sasa amehusika kwenye mabao 10 ya Yanga, akifunga mabao 8 na kuasisti mara 2. Ikiwa Simba wanataka pointi 3 wana kazi ya kufanya kwa Dube.

Zouzoua Pacome

Pacome Yanga SC
Pacome Yanga SC

Anatajwa kuwa ndiye injini ya Yanga SC kwa sasa, akichukua majukumu hayo tangu Aziz Ki alipoondoka. Pacome msimu huu amehesika kwenye mabao 10 ya Yanga SC, akifunga mabao 7 na kuasisti mara 3. Mara ya mwisho Yanga SC na Simba SC walipokutana hakucheza kutokana na majeraha, Simba wanapaswa kuwa makini kwani aliwaliza kwenye ngao ya jamii.

SOMA HII PIA: Kiungo wa Yanga SC Mudathiri Yahya kuikosa mechi ya Simba SC | Afungiwa mechi 3 na TPLB

Laurindo Depu

Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC NBC
Depuu

Amejiunga na Yanga katika dirisha dogo la usajili, lakini Nyota huyu ni moto wa kuotea mbali. Kwa muda mchache tu, straika huyo rai awa Angola ameifungia Yanga SC mabao 6 na kama ataendelea na kasi hiyo anaweza kuwashangaza wengi msiu huu. Aliwapa walinzi wa Simba SC wakati mgumu kwenye mchezo wa kwanza na anatabiriwa kufanYa hivyo tena watakapokutana Mei 3, 2026.

Maxi Nzengeli

Hili ni jina ambalo mashabiki wa Simba SC hawataki kabisa kulisikia, amewafunga Simba SC kwenye michezo 3 mfululizo kati ya mechi 5 zilizopita. Msimu huu naye ni miongoni mwa Nyota wenye takwimu bora, amehusika kwenye mabao 8 akifunga mabao 4 na kuasisti mara 4. Kocha, Steve Barker wa Simba SC ana kazi kubwa kuandaa mpango wa kumzuia.

Allan Okello

Simba SC vs Yanga SC
Allan

‘Star boy’ ndilo jina lake la utani, ni mchezaji wa kimataifa wa Uganda mwenye umri wa miaka 25 tu. Alianza kwa kusasua kiasi cha kuwatisha baadhi ya mashabiki wa Yanga SC, lakini kasi aliyonayo sasa inatishia wengi. Okello amehusika kwenye mabao 8 ya Yanga SC msimu huu akifunga mabao 6 na kuasisti mara 2. Star boy ana moto na Simba wanapaswa kumchunga.

Hitimisho

Simba SC vs Yanga SC ndio mchezo mkubwa kwenye histori ya soka la Tanzania. Hali hii inaufanya mchezo huu kubeba presha kubwa, huku kila hatua ikifuatilliwa kwa karibu. Ni wazi mchezaji yoyote anaweza kuleta tofauti katika mchezo huu, lakini hawa waliotajwa ni hatari zaidi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.