Simba SC vs Yanga SC kupigwa Uwanja wa Meja IsamuhyoMeja
  • Dabi ya Kariakoo kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, Mei 3, 2026
  • Uwanja una uwezo wa kuchukua mashabiki 15,000
  • TPLB yataja sababu Uwanja wa Benjemin Mkapa kutotumika

Dabi ya Kariako kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, Mei 3, 2026. Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Taarifa rasmi iliyotolewa leo Aprili 24,2026 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imethibitisha.

SOMA HII: Simba SC kuigomea Kariakoo Dabi? Kisa Uwanja wa New Amaan Complex, barua yajibiwa

Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Challenge

Dabi ya Kariakoo kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo

Simba SC vs Yanga SC kupigwa Uwanja wa Meja Isamuhyo
Simba SC vs Yanga SC.

Dabi ya Kariakoo kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo kwa wababe Simba SC vs Yanga SC kusaka pointi tatu. Mzunguko wa kwanza ilichezwa Uwanja wa New Amaan Zanzibar. Ubao ulisoma Yanga SC 0-0 Simba SC na mchezaji bora alikuwa Djigui Diarra. Huu unakuwa mchezo wa kwanza kuchezwa katika kambi ya jeshi Meja Jeneral Isamuhyo.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ukafanyiwa mabadiliko. Mechi ikapelekwa Zanzibar na hii ilitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa mabadiliko yamefanyika. 2025/26 wababe hawa kwenye NBC Premier League hawajakutana katika uwanja uliopangwa mwanzo.

SOMA HII: Fulltime: Yanga SC 0-0 Simba SC NBC Premier League/Highlights, stats, standings

SportPesa Aviator Challenge

Taarifa kutoka TPLB hii hapa

Zimbwe Jr vs Simba
Zimbwe Jr vs Simba NBC Premier League.

Taarifa kutoka TPLB imeeleza namna huu: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) inatangaza mabadiliko ya uwanja wa mchezo namba 169 wa Ligi Kuu ya NBC 2025/26 Simba SC vs Yanga SC maarufu kama Kariakoo Derby.

Mchezo huo hapo awali ulipangwa kufanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, sasa utachezwa Uwanja wa Mej. Jeneral Isamuhyo, Dar Mei 3, 2026 kuanzia saa 12:00 jioni.

Sababu ya mabadiliko hayo ni Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa kwenye matengenezo. Klabu za Simba SC na Yanga SC na wadau wengine wa Ligi Kuu ya NBC wamepatiwa taarifa zote kuhusiana na mabadiliko ya uwanja wa mchezo huo na maandalizi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mikubwa ya ligi ya 6 kwa ubora barani Afrika. Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inawatakia maandalizi mema wadau wote wa michezo.

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali

Uwezo wa Uwanja wa Meja Isahmuyo

Uwanja wa Meja Isamuhyo una uwezo wa kuchukua mashabiki 15,000. Uwezo wake ni mdogo kulingana na ukubwa wa mechi ya Kariakoo Dabi ambayo hubeba mashabiki wengi. Mnyama amekuwa akitumia uwanja huo kwa mechi za nyumbani hivyo kazi inaendelea kwa mechi zinazofuata wakiwa nyumbani.

Kwenye msimamo Simba SC ipo nafasi ya pili na pointi 42 inakutana na Yanga SC inayoongoza ligi ikiwa na pointi 47. Katika mechi 5 zilizopita Yanga SC imeshinda 4 na sare moja kwenye Kariakoo Dabi.

Hitimisho

Dabi ya Kariakoo kupigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo TPLB wapo kazini kuhakikisha mazingira yanakuwa bora. Ikumbukwe kwamba timu hizi ni kongwe Afrika zina mashabiki zaidi ya 15,000 kwa Dar kila timu. Je mnyama atapata matokeo akiwa nyumbani ama Yanga SC wataendeleza ubabe? Majibu Mei 3, 2026 baada ya dakika 90.

Share this: