Ali Shaban KamweAli Shaban Kamwe
  • Mashabiki wanasubiri kwa shauku kubwa tamasha kubwa Afrika linaloashiria kuanza kwa msimu mpya wa 2025/26 katika Ligi Kuu Tanzania ya NBC na mashindano ya kimataifa.
  • Wiki ya Mwananchi zinahesabika siku kabla ya kilele Uwanja wa Mkapa ambapo kutakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Bandari FC ya Kenya.
  • Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amebainisha kuwa tunapiga kichwani tu itakuwa ni slogan.

Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025 tunapiga kichwani tu ni slogan mpya ya Yanga SC msimu wa 2025/26. Msimu wa 2024/25 slogan ilikuwa ni wewe huogopi? Katika Wiki ya Mwananchi, Yanga SC wenye tamasha hilo kubwa ambalo hutumika kutambulisha wachezaji wapya na waliokuwa katika kikosi msimu uliopita wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Bandari FC ya Kenya.

Wikiendi ni muda wakupaisha Kindege cha SportPesa utue na mamilioni

Muda ni sasa kupaisha Kindege cha SportPesa na kuvuna mamilioni. Rahisi sana na ushindi unakusubiri sasa. Unachotakiwa kufanya ni kucheza Aviator upate mgao wako.

SEO Banner LV

Sababu ya Wiki ya Mwananchi Septemba 12 tunapiga kichwani tu

Wiki ya Mwananchi
Israel Mwenda nyota wa Yanga SC kwenye maandalizi kuelekea Wiki ya Mwananchi.

Soma hii: Nyie hamuogopi ilikuwa Uwanja wa Mkapa Agosti 3 2024

Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025, Uwanja wa Mkapa itakuwa ni kilele. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amebainisha kuwa kwa sasa wanaelekea kwenye msimu wa vitendo tu. Aliongeza kwa kubainisha kuwa na dozi kwa wapinzani wao itaongezeka.

 “Wanayanga sasa wamevuka level ya kuwa na Slogan za kupeana matumaini. Tumekubaliana huu ni msimu wa vitendo na tumegundua watu bado wanataka dozi, kuanzia sasa tunaenda kupiga kichwani tu.

“Tunapiga Kichwani tu hiyo ndio slogan yetu. Tukipiga kichwani tunacheza na ufahamu. Mwaka huu ni kichwa tu, tumeweka kabisa nyundo kwa ajili ya wale wanaokaza fuvu.

Kuhusu burudani kilele cha Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025

Kamwe kuhusu burudani na matukio muhimu alisema: -“Kwa sasa Yanga SC tuna ajenda moja tu tamasha bora na kubwa Afrika la Wiki ya Mwananchi.  Kila mwananchi atafurahi. Tukio la msimu huu lazima liwe na huduma rafiki kwa familia na kila mtu. Tunahakikisha tunatoa huduma bora kuwahi kutokea katika historia ya matamasha ya michezo Tanzania.

Ali Kamwe (-)
Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Bandari FC Septemba 12: highlight, vikosi, h2h, utabiri, Kitawaka wiki ya wananchi

“Tunatarajia kuwa na burudani kubwa na ya kipekee kutoka kwa wasanii wakubwa sana. Tumeshaongea na wasanii husika tumewaeleza kuwa wanapaswa kupandisha daraja lao la burudani. Kila mwanayanga atakayefika uwanjani atakutana na burudani ambayo hajawahi kuipata popote.

“Tutakuwa na mchezo wa timu ya Yanga Princess siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi. Yanga Princess msimu huu ni moja kati ya timu ambayo imefanya usajili bora sana. Tumeonesha jeuri ya fedha. Tumemrejesha Precious, Wincate na Mynaco.

“Tumehakikisha wachezaji wetu bora kama akina Aregash wamesalia. Mratibu wa Yanga Princess amesema hakuna tena kisingizio.

“Tutakuwa na mchezo mwingine muhimu sana wa timu ya viongozi wa Yanga na wasanii, huu utakuwa mchezo wa kukata na shoka. Mechi ya mwisho nilitokea benchi ila mchezo huu nitakwenda kuanza na wasipokuwa makini nitachukua na kitambaa kabisa. Kocha wetu Romain Folz na msaidizi wake Rodriguez nao watakuwepo,”.

Tunapiga kichwani tu itaongozwa na wapya hawa

Ecua Elastin

Huyu ni mchezaji mpya alitambulishwa Yanga SC, Agosti Mosi 2025. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote. Yeye ni raia wa Ivory Coast.

Doumbia

Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Nyota huyu ana umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC kutokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Anatajwa kuwa na uwezo kwenye majaribio ya mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine.

Andy Boyeli

 Andy Bobwa Boyeli alitambulishwa Julai 31 ndani ya kikosi cha Yanga SC. Ana miaka 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Anasubiriwa kwa shauku kwenye Wiki ya Mwananchi ikiwa na slogan ya ‘Tunapiga Kichwani Tu’.

Lassine Kouma

Lassine Kouma mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien na amekabidhiwa jezi namba 8.

Balla Conte

Rayon Sports FC 1-3 Yanga SC: Highlights, magoli yote
Balla Conte nyota wa kikosi cha Yanga SC.

Soma hii: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC kabla ya kutambulishwa Yanga SC. Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.

Offen Chikola

Uwezo wake mkubwa ni kwenye kutumia mguu wa kushoto. Akiwa na uzi wa Tabora United msimu wa 2024/25 alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu yake ya zamani.Mashabiki wanasubiri kuona uwezo wake katika matumizi ya mguu wa kulia uwanjani.

Casemiro

 Anaitwa Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Anaingia kwenye orodha ya wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Yanga SC chenye maskani yake Jangwani, Dar.

Zimbwe Jr

Zimbwe Kapten
Zimbwe Jr ingizo jipya Yanga SC 2025/26.

Soma hii: Mohamed Hussen Zimbwe Jr ni Yanga SC

Mohamed Hussen Zimbwe Jr alikuwa Simba SC msimu wa 2024/25. Msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC. Anasubiriwa kwa shauku na mashaki katika Wiki ya Mwananchi.

Hitimisho

Wiki ya Mwananchi Septemba 12 2025 tunapiga kichwani tu inakwenda kujaribiwa kwa mara ya kwanza kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi. Baada ya hapo mchezo unaofuata itakuwa dhidi ya Simba SC. Yanga SC vs Simba SC wanatarajiwa kukutana Septemba 16 2025, Uwanja wa Mkapa.

image

Share this: