Rushine De Reuck rasmi asaini na atambulishwa Simba SCAhmed Ally
  • Mohamed Hussein aaga rasmi Simba atajwa kusaini Yanga, atoa sababu 3 nzito.
  • Hili ni pigo la pili kubwa kwa Simba katika dirisha hili la usajili baada ya jana Ijumaa kupigwa kikumbo na Yanga kwenye dili la Balla Conte.
  • Licha ya kuwa kwenye presha kubwa na kinachoendelea kwenye dirisha la usajili, Simba wanatajwa kuvizia Saini ya straika kutoka Ivory Coast Dramane Kamagate.

Aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Simba, Mohamed Hussein rasmi amewaandikia ujumbe wa kuwaaga mashabiki, benchi la ufundi, viongozi na waliokuwa wachezaji wenzake ndani ya kikosi cha timu hiyo ambapo anatajwa kutimkia Yanga huku mabosi wa Simba sasa wakigeukia usajili wa straika Kamagate.

Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

SEO Banner LV

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

Hii hapa barua ya Mohamed Hussein kwa Wanasimba (Sababu 3 nzito)

Barua ya MO Hussein Simba
Barua ya MO Hussein Simba

“Takribani miaka 11 ya Furaha, huzuni, Shangwe, vifijo, nderemo na masikitiko ndani ya Mbuga. Kwa uaminifu mkubwa, weledi wa kiwango cha juu, Kuvuja jasho kuipigania nembo ya klabu ndio ulikuwa msingi na malengo. Wahenga walisema kila lenye mwanzo halikosi mwisho na leo nawaaga rasmi.

“Haya ni maamuzi yaliyolenga Maendeleo yangu binafsi, maslahi yangu binafsi na weledi wangu uliotukuka. Nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi, benchi la ufundi na ‘operation staffs’ wote wa klabu ya Simba SC kwa kipindi chote cha kuhudumu ndani ya klabu.

“Kipekee niwashukuru mashabiki kwa kuwa nami kipindi chote, kama mnavyonipenda na mimi nawapenda pia na nina imani mtaendelea kuniunga mkono. Naishukuru Management Yangu ikiongozwa na Carlos Carlos kwa ushirikiano mkubwa wa kipindi chote.”

SOMA HII PIA: Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC

Pigo la pili baada ya kumpoteza Balla Conte

Hili linaonekana kuwa pigo la pili kubwa kwa Simba katika dirisha hili la usajili nah ii ni baada ya Simba hivi karibuni kupigwa kikumbo na Yanga kwenye dili la staa wa kimataifa wa Guinea, Balla Moussa Conte ambaye Yanga walikamilisha usajili wake na kumtambulisha jana Ijumaa.

Kuhusu utambulisho wa Conte na Yanga

Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC
Conte na Kamwe

Balla Conte amesaini rasmi Yanga mkataba wa miaka miwili na kutambulishwa jana Ijumaa, stori ambayo imekuwa gumzo kubwa kwenye dirisha la usajili hasa kwa kuwa staa huyo alihusishwa kuziingiza vitani Yanga SC na Simba SC ambazo zote zilikuwa vitani kusaka Saini ya nyota huyu wa Guinea.

SOMA HII PIA: Baada ya Conte Yanga SC yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Jeuri ya pesa na Umafia watumika

Tajiri wa Simba MO Dewji na GSM wa Yanga
Tajiri wa Simba MO Dewji na GSM wa Yanga

Kutoka kwa mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael ameweka wazi kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.

“Kulikuwepo na makubaliano kati ya klabu na klabu (CS Sfaxien na Yanga), ambapo Yanga walipewa Ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga hayajakamilika ndipo usiku Simba walienda na ofa kubwa.

“Kocha mkuu wa Simba, Fadlu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya Simu. Ofa ya Simba kwenda CS Sfaxien ni kubwa sana kuliko Yanga na Fadlu anawapush viongozi wake kumpata kijana kwani ndio chaguo namba moja sokoni.

“Baada ya vita kubwa kati ya Simba na Yanga, usiku wa jana Rais wa Yanga alituma ofa kubwa zaidi kwenda kwa Conte na CS Sfaxien. Ofa hiyo imekubalika na pande hizo mbili, hivyo asubuhi hii dili limekamilika pande zote. Conte ameahidiwa na Yanga kupewa Gari, Nyumba ya kuishi na mshahara mnono.

“Simba waliweka ofa mezani ila changamoto walitaka kulipa hela hiyo kwa awamu mbili, kitu ambacho CS Sfaxien wamekataa, hivyo Yanga wamekubali kulipa hela zote kwa Awamu moja na CS Sfaxien wamekubali biashara.

Ishu ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Yanga sasa ikoje?

Hivi karibuni hata kabla ya Mohamed Hussein kuaga Simba leo, imekuwa ikielezwa kuwa Yanga rasmi wamefungua mazungumzo na beki na nahodha huyo wa zamani wa Simba taarifa ambazo zimeripotiwa na vyanzo mbalimbali vya Habari.

Kuaga kwa Mohamed Hussein Simba kumetafsiriwa kama hatua muhimu kwake ya kuhamia Yanga timu ambayo imehusishwa sana na kuhitaji Saini yake katika dirisha hili kubwa la usajili ambapo inatajwa kuwa hata taratibu za kusaini mkataba wake zimefanyika akiwa kwenye kambi ya kujiandaa na mashindano ya Chan Misri. Je atatambulishwa Yanga tusubiri na kuona.

Hitimisho Simba sasa wamgeukia Kamagate

Mohamed Hussein aaga rasmi Simba atajwa kusaini Yanga
Kamagate

Licha ya kuwa kwenye presha kubwa kutokana na kinachoendelea kwenye dirisha la usajili, uongozi wa Simba umeendelea kufanya majukumu yake ikiwemo kuachana na wachezaji ambao hawapo kwenye mipango yao akiwemo Debora Fernadez, huku sasa inaelezwa wameweka nguvu kumsajili straika bora wa Ligi Kuu Ivory Coast msimu uliopita Dramane Kamagate.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC yakata tamaa kuhusu Zimbwe Jr | Yanga SC yampa ofa nono | Orodha ya wachezaji walioachwa

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.