- Septemba 5 2025 kulikuwa na mchezo mkali wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa Alphonce Masamba Debat.
- Congo Brazzaville vs Tanzania walikabana koo katika msako wa pointi tatu, mwisho walitsoshana nguvu kwa kugawana pointi mojamoja.
- Seleman Mwalimu alivuruga hesabu za wapinzani wao kupata ushindi katika dakika za jioni akitokea benchi alipofunga goli kwa Tanzania.
Congo Brazzaville vs Tanzania wametoshana nguvu kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 wakifungana bao 1-1. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Alphonce Masamba Debat Septemba 5 2025. Dakika 45 za mwanzo hakukuwa na timu iliyoona lango la mpinzani mpaka kipindi cha pili.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mkwanja
Ni muda wako kuvuna mkwanja bila kuvuja jasho. Ukipaisha Kindege cha SportPesa unavuna mamilioni. Cheza Aviator sasa hivi upate mgao wako.

Congo Brazzaville vs Tanzania wafungaji wa magoli uwanjani

Soma hii: Tanzania vs Burkina Faso na Kenya vs DR Congo: Wenyeji waanza kwa kishindo CHAN 2024.
Ni Dechan Moussavou Lingard alifungua pazia la kufunga dakika ya 69. Mchezaji huyu alifunga goli hilo kwa shuti kali akiwa nje ya 18 akitumia mguu wa kulia. Shuti hilo lilimshinda mlinda mlango Yacoub Suleiman ambaye alianza kikosi cha kwanza.
Ilibidi Tanzania kusubiri zipite dakika 15. Ni mguu wa kushoto wa Seleman Mwalimu Ali ulifunga goli dakika ya 84. Mguu wa kushoto ulitosha kupachika goli hilo ndani ya 18 akitumia pasi ya mshambuliaji Clement Mzize.
Kocha wa Tanzania Hemed Suleiman atoa neno baada ya mchezo

Soma hii: Tanzania vs Morocco robo fainali dume Uwanja wa Mkapa
Hemed Suleiman, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameweka wazi kuwa hawakucheza vizuri. Amebainisha kuwa makosa watayafanyia kazi uwanja wa mazoezi kuwa imara zaidi. Mchezo ujao wa Tanzania watakuwa nyumbani dhidi ya Niger Septemba 9 2025, Uwanja wa New Amaan Complex.
“Tulitarajia kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu lakini mwisho tumepata pointi moja. Hatukucheza vizuri kama ambavyo tulitarajia. Ila matokeo haya tunayachukua na makosa tutafanyia kazi kwenye mchezo wetu ujao,”.
Hiki hapa kikosi cha Tanzania vs Congo Brazzaville
Yakoub Suleiman mlinda mlango anavaa jezi namba 18, Shomari Kapombe beki anavaa jezi namba 22, Pascal Msindo beki anavaa jezi namba 2. Dickson Job beki anavaa jezi namba 5, Ibrahim Bacca anavaa jezi namba 4. Novatus Dismas kiungo anavaa jezi namba 20, Mudathir Yahya kiungo anavaa jezi namba 23.
Feisal Salum kiungo anavaa jezi namba 6, Clement Mzize mshambuliaji anavaa jezi namba 7, Mbwana Samatta mshambuliaji anavaa jezi namba 10 huyu ni nahodha na Saimon Msuva winga anavaa jezi namba 12.
Wachezaji wa akiba ni Hussen Masalanga, Anthony Mpemba, Mohamed Hussen, Wilson Nangu,Lusajo Mwaikenda, Yusuph Kagoma, Yahya Zayd, Idd Suleiman, Edmund John, Seleman Mwalimu na Abdul Hamis.
Hiki hapa kikosi cha Congo Brazzaville vs Tanzania
Fabrizio Cesana, Kocha Mkuu wa Congo Brazzaville katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 kikosi alikuwa kamili. Alitumia mfumo wa 4-2-3-1. Hiki hapa kikosi chake cha kazi:-
Chelcy Bobazebi mwenye miaka 19 alikuwa langoni, C. Atipo, J.Mbembe, B.Itoua ambaye ni nahodha, J. Kapaya, C. Massanga, G.Nongo. D. Moussavou ambaye ni mfungaji wa bao. L.Loemba, M.Koto na D. Bassinga.
Wachezaji wa akiba ni Venold Dzaba, Grace Mavoungou, Christopher Wamba, Simon Samba, Chrislay Pedro, Prince Mouandza, Divin De Nzingoula, Digne Pounga, Chadrac Osseby, Grace Nsemi na Carly Ekongo.
Mabadiliko katika mchezo yalikuwa namna hii:-
G Mavoungou dakika ya 87 alichukua nafasi ya M. Koto, V. Dzaba aliingia dakika ya 41 akichukua nafasi ya G.Nongo dk 41 kwa Congo Brazzaville.
Kwa Tanzania ilikuwa:-Lusajo Mwaikenda aliingia akichukua nafasi ya Shomari Kapombe dakika ya 75, Suleman Mwalimu aliingia akichukua nafasi ya Mudathir Yahya dakika ya 76, Nado aliingia akichukua nafasi ya Mzize dakika ya 89, Mohamed Hussen aliingia dakika ya 60 alichukua nafasi ya Msindo.
Kadi za njano kwa wachezaji
Mchezaji Dechan wa Congo Brazzaville alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 70 kwa kucheza faulo mbaya, Baranger Itoua naye alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 82.
H2H
Katika mashindano haya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 wamekutana mara mbili. 17/03/2025, Tanzania 3-0 Congo Brazzaville na 5/9/2025, Congo Brazzaville 1-1 Tanzania.

Soma hii: Tanzania kuikabili Madagascar CHAN 2024
Msimamo wa Kundi E
Morocco inaongoza kundi ikiwa na pointi 18 imeshinda mechi zote 6, Tanzania namba mbili ikiwa na pointi 10, ushindi mechi 3, sare 1,imepoteza 2, Zambia nafasi ya 3 ina pointi 6, Niger ina pointi 6 nafasi ya 4, Congo Brazzaville nafasi ya 5 pointi 1.
Hitimisho
Congo Brazzaville vs Tanzania ni mchezo uliokusanya magoli mawili ndani ya dakika 90. Katika dakika 45 kila timu ilikuwa inamvutia kasi mwenzake. Mwalimu alikuwa benchi na goli lake na alipoingia alifunga.


