Simba SC vs JKT Tanzania NBCSowah Mnyama
  • Simba SC haitaki utani kutokana na maboresho makubwa kwenye kikosi hicho kilichoweka kambi nchini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
  • Usajili mpya Simba SC 2025/25 gumzo kubwa kutokana na kuimarisha kila idara huku ikiwatambulisha wachezaji wawili tegemeo kutoka JKT Tanzania.
  • Zimebaki siku tatu dirisha la usajili kufungwa ikiwa ni ishara ya kuanza mchakamchaka wa msimu mpya wa ligi ya NBC.

Usajili mpya Simba SC 2025/26 ni gumzo kutokana na kubeba wachezaji wawili nguzo ndani ya JKT Tanzania. Awali ilikuwa ni tetesi na mwisho zimekamilika kwa wachezaji hao tegemeo kutangazwa. Ni Wilson Nangu ambaye ni beki na Yakoub Suleman ambaye ni kipa.

Muda wakuvuna mamilioni na Kindege cha SportPesa

Kila sekunde kuna rubani anavuna mamilioni akipaisha Kindege cha SportPesa. Rahisi sana ukicheza Aviator. Mgao upo kila siku unakusubiri rubani makini.

SEO Banner LV

Usajili mpya Simba SC 2025/26 ulivyokuwa gumzo

Usajili mpya Simba SC 2025/26
Nangu beki alipewa Thank You JKT Tanzania Agosti 28 2025. Source: JKT Tanzania.

Soma hii: Wadi Degla SC 0-2 Simba SC: Magoli yote, vikosi, highlights, h2h

Mara ya dirisha la usajili kufunguliwa Julai Mosi 2025, Simba SC ilikaa kimya kwa muda jambo lililokuwa gumzo kuna nini kilichotokea? Zilipita siku 28 bila Simba SC kutambulisha mchezaji mpya. Mchezaji wa kwanza alitambulishwa Julai 29 ni Rushine De Reuck huyu ni beki raia wa Afrika Kusini.

Usajili wa Wilson Nangu na Yakoub

Wakati zikiwa zimesalia siku tatu usajili kufungwa, kuna wachezaji wawili wametambulishwa. Ni beki Wilson Nangu na Yakoub Suleiman ambaye ni kipa. Hawa wawili walikuwa chaguo la kwanza ndani ya JKT Tanzania.

Utambulisho wao kuwa wachezaji wapya Simba SC 2025/26. Nyota hawa walikuwa katika timu ya taifa ya Tanzania iliyoishia hatua ya robo fainali CHAN 2024 huku Yakoub akiwa ni kipa namba moja. Wote wanatarajiwa kuwa katika changamoto mpya msimu ujao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Majina yao yamejumuishwa katika kikosi cha Tanzania ambacho kinajiandaa na michezo miwili ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Congo Brazzaville na Niger. Tayari wapo kwenye kikosi kilichopo DR Congo kwa mchezo wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Septemba 5 2025. Uwepo wao katika timu ya taifa unamaanisha kuwa walikuwa muhimili ndani ya JKT Tanzania.

Orodha ya usajili mpya Simba SC 2025/26 hii hapa

Sele Mwalimu Gomez
Sele Mwalimu Gomez usajili mpya Simba SC 2025/26.

Soma hii:Simba Day 2025 ni Simba SC vs Gor Mahia FC: highlight, vikosi, h2h, Ubaya Ubwela Part 2 moto utawaka!

Mwalimu

Selemani Mwalimu alitambulishwa Simba SC, Agosti 28 kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja. Alikuwa Wydad Casablanca ya Morocco. Huyu ni mshambuliaji.

Kante

Nyota Alassane Kante ambaye ni kiungo alikuwa anacheza CA Bizertin ya Tunisia. Atakuwa ndani ya Simba SC msimu wa 2025/26. Alitambulishwa Julai 30 2025.

Morice

 Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025. Nyota huyo amesema kuwa kuna kazi kubwa yakufanya katika changamoto mpya. Yupo kambini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya.

Semfuko

 Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga. Atakuwa kwenye changamoto mpya.

Sowah

Jonathan Sowah alitambulishwa Simba SC, Agosti Mosi 2025. Msimu wa 2024/25 alikuwa Singida Black Stars alifunga mabao 13.

Bajaber

Agosti 2 2025 Simba SC ilimtambulisha Mohamed Bajaber. Kiungo mshambuliaji alikuwa anacheza Polisi ya Kenya. Nyota huyu ana uwezo wakufunga na kutengeneza nafasi ndani ya uwanja.

Mligo

Antony Mligo beki wa kushoto alitambulishwa ndani ya Simba SC Agosti 5 2025 alikuwa Namungo FC. Kandarasi ya miaka mitatu. Beki huyo ni mrithi wa mikoba ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr ambaye yupo ndani ya kikosi cha Yanga SC.

Camara

Wadi Degla SC 0-2 Simba SC
Camara Simba SC ingizo jipya Simba SC 2025/26.

Soma hii: Simba SC kufanya usajili mkubwa

Ni Naby Camara alitambulishwa rasmi kuwa nyekundu na nyeupe Agosti 14 2025. Nyota huyo aliwahi kucheza Klabu ya Al Waab ya Qatar na CS Sfaxien.

Camara ana umri wa miaka 23 ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati na beki wa kushoto. Anasajiliwa ili kuongeza nguvu kwenye upande wa kushoto wa ulinzi, nafasi iliyoachwa wazi na Mohammed Hussein Zimbwe Jr, ambaye amejiunga na watani wa jadi, Yanga SC.

Nyota huyo mpya wa Simba SC aliwahi kuichezea klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia na msimu uliopita alikuwa akiitumikia Al-Waab Sporting Club ya nchini Qatar.

Hitimisho

Usajili mpya wa Simba SC 2025/26 utafika tamati rasmi dirisha litakapofungwa. Dirisha la usajili lilifunguliwa Julai Mosi 2025 linatarajiwa kufungwa Septemba 7 2025 saa 5:59 usiku. Simba SC itawatambulisha wachezaji wote Septemba 10 2025 kwenye tamasha la Simba Day 2025.

image
Share this: