- Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12, ni siku ya kihistoria.
- Mashine zote mpya za Yanga kutambulishwa rasmi mbele ya Maelfu ya Wananchi.
- Yanga SC kujaza tena viwanja viwili? Safari ya kusaka makombe msimu mpya wa 2025/26 kuanza rasmi.
Hatimaye uongozi wa Yanga umeitangaza siku ya Ijumaa ya Septemba 12, mwaka huu kuwa siku rasmi ya kilele cha wiki ya Wananchi. Hii ni siku maalum ambayo hutumiwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kikosi kipya mbele ya mashabiki. Pamoja na utambulisho huo matukio kama burudani za muziki na mechi kali ya soka hunogesha. Hili ni miongoni mwa matamasha makubwa ya michezo Afrika.
Paisha ‘Kindege’ cha Sportpesa ushinde mamilioni sasa
Wakati ukiendelea kuhabarika na makala hii, kumbuka unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza sasa mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Historia ya Tamasha la Wananchi

Historia ya tamasha hili haiwezi kuwekwa mbali na ile ya Tamasha la watani zao wa Jadi Simba SC, ambao walianzisha Simba Day zaidi ya miaka 10 iliyopita. Simba SC ilianzisha Tamasha hilo kama sehemu ya malengo ya kupata fedha za usajili na gharama nyingine za uendeshaji wa timu.
Ikumbukwe Muasisi wa tamasha hilo kwa upande wa Simba SC wakati ule alikuwa, Hassan Dalali ambaye alikuwa akihudumu katika nafasi ya mwenyekiti. Siku za awali Tarehe rasmi ya Tamasha ilikuwa ni Agosti 8, ambayo kila mwaka Tanzania pia inaadhimisha sikukuu ya wakulima. Kutokana na mabadiliko ya ratiba kila msimu, siku hiyo nayo imekuwa ikibadilika.
Baada ya timu kuwa a misuli ya uongozi pia, lengo kuu likabadilika kutoka kukusanya fedha mpaka kuwa burudani rasmi. Burudani hii huhusisha utambulisho wa wachezaji na benchi la ufundi. Hii pia inahusisha viongozi kuweka wazi shabaha ya timu kwa msimu husika.
Ili kusherehesha tukio hilo, katika miaka ya karibuni mara nyingi tamasha hilo huhusisha burudani mbalimbali za wasanii. Wasanii hao hutoka katika viwanda mbalimbali ikiwemo muziki, sarakasi n.k.
SOMA HII PIA: Nyie hamuogopi 2024/25? Yanga yaweka rekodi
Mbosso kulibeba tamasha mwaka huu?

Upo uwezekano mkubwa wa msanii wa kizazi kipya Mbosso Khan kulibeba tamasha hili. Hii ni baada ya kuwa na mafanikio makubwa alivyobeba sherehe za ubingwa wa Yanga, mwishoni mwa msimu uliopita. Ikumbukwe Mbosso kupiia ‘Hit Song’ yake ya Aviola alipata heshima kubwa, kutumbuiza katika hafla ya ubingwa wa Yanga. Hii inamuweka kwenye nafasi nzuri ya kupata tenda hii.
SOMA HII PIA: Fei Toto kusaini Simba au Yanga? Tetesi usajili bongo, ulaya
Sura mpya ndani ya Yanga SC msimu wa 2025/26

- Mohamed Doumbia
Yanga SC ilimshusha staa huyu usiku wa Agosti 3, 2025. Doumbia ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga SC 2025/26, ambapo nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 amejiunga na Yanga SC akitokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Anatajwa kuwa na uwezo mkubwa wa majaribio ya mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine.
- Ecua Elastin
1/08/ 2025 uongozi wa Yanga ulimtambulisha Ecua kwa dili la miaka miwili. Ikumbukwe Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC, ambapo alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli.
- Boyeli
MVP wa zamani wa Ligi Kuu ya Zambia, ambaye naye amejiunga na Wananchi kutokea Afrika Kusini. Alitambulishwa Julai 31, 2025. Akiwa na umri wa miaa 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini. Sasa nyota huyo atahudumu kwa mkopo wa angalau nwaka mmoja na Wananchi.
- Paul Mattews
Huyu ni Mkurugenzi mpya wa ufundi wa Yanga ambaye alitambulishwa Yanga SC Julai 29 2025. Yupo Jangwani msimu wa 2025/26. Anakwenda kuwa kiungo muhimu cha wachezaji, viongozi na mashabiki.
- Manu Rodriguez
Kocha msaidizi mpya wa Yanga ni, Manu Rodriguez alitambulishwa Julai 29 2025. Anaingia kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha msaidizi wa Yanga SCakimsaidia mkuu mpya wa benchi la ufundi kocha, Romain Folz ambaye naye ni mrithi mikoba ya Miloud Hamdi. Ikumbukwe Aucho tayari mkataba wake umeisha na hakuna mazungumzo ya mkataba mpya.
- Balla Conte
Huyu usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC na Yanga SC. Julai 18, 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.
SOMA HII ZAIDI: Baada ya Aziz Ki: Mzize na Aucho wanaondoka Yanga? Tetesi usajili bongo
Hitimisho: Hawa pia watarajiwe kutambulishwa kwa mara ya kwanza

Ukiachana na mashabiki wazawa na wa kimataifa, Yanga SC wiki ya wananchi pia itawashuhudia mastaa wapya kama; Offen Chikola, Casemiro, Ninju na kocha wao Roman Folz

