- Ni Yanga SC vs Simba SC, Ngao ya Jamii Agosti 12, 2026 mechi ya ufunguzi msimu mpya 2026/27
- H2H wababe hawa wawili matokeo ya mwisho ilikuwa Yanga SC 1-0 Simba SC, Uwanja wa Benjamini Mkapa
- Pacome kuikosa Kariakoo Dabi, huyu ni mfungaji wa bao la ushindi fainali ya mwisho
- Rais wa TFF Wallace Karia ataja sababu ya mabingwa kukutana
Ni Yanga SC vs Simba SC, Ngao ya Jamii Agosti 12, 2026 wababe hawa watakutana ikiwa ni Kariakoo Dabi. Mchezo huu ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu mpya wa 2026/27. Mabingwa wa NBC Premier League 2025/26 Yanga SC watamenyana na mabingwa wa CRDB Federation Cup Simba SC. Ligi inatarajiwa kuanza rasmi Agosti 14,2026.
Aziz Ki kurudi Yanga? Aziz Ki kurudi Yanga SC | Tetesi usajili Ligi Kuu NBC
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Kwa nini Yanga SC vs Simba SC, Ngao ya Jamii Agosti 12, 2026?

Yanga SC vs Simba SC Ngao ya Jamii Agosti 12, 2026 kupigwa mapema ni Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON. Mpango mkubwa wa mechi za Ngao ya Jamii ulikuwa unahusisha timua ambazo zinamaliza nafasi nne kwenye msimamo. Ni Yanga SC, Simba SC, Azam FC na Singida Black Stars hizi zilipaswa kucheza Ngao ya Jamii kwa mfumo wa mechi za mtoano.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema mfumo wa Ngao ya Jamii kuwa na timu nne haujabadilika.Yote haya yalifanyika kwenye uzinduzi wa mfumo wa Kidigitali wa kusimamia ligi. Aliongeza kuwa ligi inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
“Mfumo wa Ngao ya Jamii kuwa na timu 4 haujabadilika lakini kutokana na wenyeji wa AFCON tunalazimika kufanya mambo kwa haraka. Tutakuwa na timu 2 tu, bingwa wa ligi ambaye ni Yanga SC na bingwa wa CRDB ambaye ni Simba SC. Mechi hii itachezwa Agosti 12,”.
h2h Yanga SC vs Simba SC Ngao ya Jamii
| Tarehe | Mechi | Matokeo | Hatua |
|---|---|---|---|
| 16 Septemba 2025 | Yanga SC vs Simba SC | Yanga SC 1–0 Simba SC | Fainali |
| 13 Agosti 2023 | Simba SC vs Yanga SC | Simba SC 3–1 Yanga SC | Baada ya sare ya 0–0 ndani ya dakika 90, mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penalti |
| 13 Agosti 2022 | Yanga SC vs Simba SC | Yanga SC 2–1 Simba SC | Fainali |
| 25 Septemba 2021 | Yanga SC vs Simba SC | Yanga SC 1–0 Simba SC | Fainali |

Yanga SC vs Simba SC takwimu muhimu za Ngao ya Jamii
Kwenye mchezo wa ufunguzi 2025, Yanga SC waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Pacome Zouzoua. Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Benjamini Mkapa. Ilikuwa ni rekodi ya Yanga SC kuendelea kupata ushindi mbele ya mnyama kwenye jumla ya mechi 6.
Rekodi zinaonyesha kuwa Yanga SC imetwaa Ngao ya Jamii mara 9 ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo zimetwaa taji hilo mara nyingi zaidi. Wanatarajiwa kufungua msimu kwa kuanza na mtani kwenye mchezo wa kwanza Agosti 12,2026.
Mfungaji Pacome kuikosa Kariakoo Dabi
Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Pacome ambaye alikuwa mfungaji wa bao la ushindi atakosekana kwenye mchezo wa ufunguzi. Hii inatokana na maumivu ya mguu aliyopata kwenye mchezo wa kufunga msimu 2025/26. Kiungo huyo alipata maumivu Juni 30,2026 mechi vs JKT Tanzania. Kwa sasa anaendelea na matibabu ili kurejea kwenye ubora.
Hitimisho
Yanga SC vs Simba SC, Ngao ya Jamii Agosti 12,2026 ni mchezo unaoashiria kuanza kwa msimu mpya 2026/27. Timu hizi zote mbili zimefunga msimu zikiwa na mataji kabatini. Yanga SC walitwaa taji la ligi huku Simba SC wakitwaa taji la CRDB Federation Cup.

