- SportPesa mshindi mpya wa mid-week jackpot asepa na kitita cha milioni 268.6 za ushindi.
- Latifah Hamisi Mdoka ambaye ni mjasiriamali mwenye umri wa miaka 28 anayeishi Vikindu, Dar es Salaam ndiye amefanikiwa kuondoka na mzigo wa mamilioni.
- Latifah, mzaliwa wa Mchinga mkoani Lindi, ni mshindi wa tano mkubwa wa jackpot mwaka 2026 na mwanamke wa tatu kujishindia jackpot ya mamilioni kupitia SportPesa Tanzania mwaka huu
Dar es Salaam, Kampuni inayoongoza ya michezo ya kubashiri na burudani, SportPesa imeendelea kutoa tabasamu kwa wateja wake. Hii ni baada ya Julai 9, mwaka huu kumtangaza rasmi mshindi wa Mid-Week Jackpot. Mshindi huyo ni Latifa Hamisi Mdoka mwenye umri wa miaka 28 ambaye ni mjasiliamali kutoka Vikindu, Dar es Salaam. Latifa amefanikiwa kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 268,671,530 kupitia ushindi wa mid-week jackpot.
Mshindi anasemaje?

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Latifa amesema: “Nilijiunga na nyumba ya washindi Kampuni ya SportPesa mwezi Juni 2019, hivyo nimekuwa nikicheza na kampuni hii kwa miaka 7 sasa. Sijawahi kupata ushindi mkubwa kama huu, hivyo hii ni mara yangu ya 1 lakini nimewahi kupata ushindi wa bonasi ndogo.
“Ushindi huu niliokuwa naupata ulizidi kunihamasisha kuendelea kubashiri kwa kuwa nafasi ya kushinda ni kubwa. Mara nyingi nimekuwa nikichambua matokeo ya mechi kabla ya kuweka ubashiri wangu. Na kwakuwa nafanya uchambuzi kwa makini, imenisaidia kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushinda.
“Nilipopigiwa simu na kuambiwa nimeshinda, kwa kweli sikutegemea kabisa. Nilidhani ni utani. Nimekuwa nikicheza jackpot kwa matumaini kuwa siku moja na mimi ningekuwa mshindi, na leo ndoto hiyo imetimia. Namshukuru Mungu na SportPesa kwa ushindi huu ambao naamini utabadilisha maisha yangu na ya familia yangu,” alisema Latifah.
Ushindi huu ataufanyia nini?
Ushindi huu utanisaidia kutimiza malengo yangu ya kukuza shughuli zangu za ujasiriamali. Naikubali sana SportPesa kwa kunipa nafasi ya kubadilisha maisha yangu, hii ndiyo kampuni inayoaminika zaidi hapa Tanzania. Mara zote ukishinda unapewa fedha zako.”
SOMA HII PIA: SportPesa mshindi mid-week jackpot milioni 367 huyu hapa
Bosi SportPesa naye afunguka

Kufuatia ushindi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas naye amesema: “Tangu SportPesa ilipoanza shughuli zake nchini Tanzania, tumewatunuku washindi wakubwa 29 wa jackpot wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.8.
“Ushindi wa Latifah unaongeza idadi ya wanawake wanaoendelea kushinda jackpot zetu mwaka huu na unaonesha wazi kuwa washindi wetu wanatoka katika mikoa, taaluma na mazingira mbalimbali nchini.
“Hii ndiyo dhamira yetu ya kuendelea kuwapa Watanzania nafasi ya kubadilisha maisha yao, kupitia jackpot za SportPesa,” alisema Mhe. Tarimba Abbas.
SOMA HII PIA: SPORTPESA MSHINDI MID-WEEK JACKPOT AFUNGA NA KUFUNGUA MWAKA NA MILIONI 253
Mkuu Kitengo cha Masoko ahimiza wengine kushiriki

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, aliongeza: “Ushindi wa Latifah ni miongoni mwa simulizi nyingi za Watanzania, ambao wameendelea kunufaika kupitia jackpot za SportPesa.
“Kinachofurahisha zaidi kuhusu ushindi wa Latifah ni kwamba amekuwa nasi kwa zaidi ya miaka saba. Ameendelea kushiriki kwa uvumilivu na leo ameona matokeo yake. Huu ni uthibitisho kuwa kila anayeshiriki ana nafasi ya kushinda, na tunafurahi kuona ushindi huu ukibadilisha maisha yake,” alisema Tracy.
SOMA HII PIA: SupaJackpot ya SportPesa yaendelea kunufaisha wajasiriamali
Hitimisho
Ushindi wa Latifah unaendelea kuonesha kuwa jackpot za SportPesa zinabadilisha maisha ya Watanzania, kutoka maeneo na makundi mbalimbali nchini. Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa SportPesa, Tracy Humplick aliendelea kueleza, juu ya utaratibu wote wa mshindi kupokea zawadi yake. Hii ni katika kutoa fursa kwa wote wanaotaka kufuatilia mchakato wa makabidhiano, na kujiridhisha kuwa wanaweza kufuatilia kupitia akaunti rasmi za SportPesa.
