Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27Yanga SC paredi
  • Kumekucha Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27 hesabu za ubingwa zimeanza
  • Simba SC vs Yanga SC ni Agosti 12,2026 Ngao ya Jamii mchezo wa kufungua pazia la ligi
  • Ahmed Ally afungukia suala la kuchimba dawa Jangwani

Watani wa jadi Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27 yanaanza mara baada ya msimu kufika tamati. Juni 30,2026 kila timu ilitambua kile ambacho ilivuna kwenye ligi. Mabingwa walitangazwa kuwa Yanga SC mara baada ya kufikisha pointi 75 huku Simba SC nafasi ya pili na pointi 73. Tofauti ya pointi 2 ziliwatenganisha watoto hawa wa Kariakoo.

Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chin

Usajili wa Simba SC umeshtua: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27 yameanza

Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27
Simba SC Jangwani kwenye paredi la ubingwa wa CRDB Federation

Mwisho wa msimu mmoja ni mwanzo wa msimu mwingine ipo hivyo kwa Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27 yameanza rasmi. Yanga SC mechi ya mwisho ilikuwa Juni 30,2026 wakipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Tanzania. Hapo walipata tiketi ya kutwaa ubingwa na watapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba SC mchezo wa mwisho ilikuwa fainali ya CRDB Federation Cup. Mchezo huu ulichezwa Julai 4,2026 na Simba SC ikashinda bao 1-0. Azam FC ilipoteza taji hilo ikiwa imeandika rekodi ya kumuondoa hatua ya nusu fainali aliyekuwa bingwa mtetezi Yanga SC.

Maandalizi yanaanza mapema kwa timu hizi ambapo hesabu kubwa ni kuhakikisha zinatetea mataji yao msimu ujao. Kwa upande wa kimataifa kila timu ina mpango kufika mbali zaidi. Hivyo msimu mpya utakuwa na ushindani mkubwa zaidi ya uliokwisha sasa.

Yanga SC mwakani tena wanautaka ubingwa

Yanga SC Bingwa
Yanga SC Bingwa 2025/26

Vita nzito Yanga SC vs Simba SC: Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli | Wachezaji kwenye vita nzito Kariakoo Dabi

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Uongozi wa Yanga SC chini ya mdhamini mkuu SportPesa umebainisha kuwa msimu ujao unahitaji kutwaa ubingwa tena. Rekodi imeandikwa kwa timu hiyo kutwaa ubingwa mara 5 mfululizo. Inaongoza kwa kutwaa mataji mengi ambayo ni 32 mpaka sasa ya ligi.

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC amesema wanatambua ushindani utakuwa mkubwa hesabu ni kuendelea kushinda. Kiongozi huyo ameongeza kila kitu kipo kwenye mipango kuhakikisha wanafanya vizuri. Amewaomba mashabiki kuendelea na ushirikiano bila kuchoka.

“Tumekuwa na msimu wenye ushindani mkubwa na mwisho tumefanikiwa kutwaa ubingwa. Haikuwa rahisi kutokana na kila timu kuonyesha ushindani na huu ni mpira. Kwa kilichotokea tumeona na benchi la ufundi linatambua kipi kilikuwa bora na wapi ambapo tulifanya makosa.

“Mwakani tena tunahitaji kuendelea kuwa imara na kutwaa kwa mara nyingine ubingwa.Furaha yetu ni kuona tunaendelea kuwa bora zaidi ya hapa ambapo tumeishia. Kazi ni kubwa tunalitambua hilo hivyo mashabiki wazidi kuwa nasi kila nyakati,”.

Simba SC wachimba dawa ya Yanga SC

Kuelekea msimu mpya wa 2026/26 Simba SC wamechimba dawa ya Yanga SC makao makuu Jangwani. Hiyo ilikuwa ni Julai 5,2026 kwenye paredi la ubingwa wa CRDB Federation Cup. Mashabiki wa Simba SC walifika Jangwani na kuchimba dawa ikiwa ni imani kwamba watafanya vizuri msimu ujao.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kitendo hicho ni nguvu kuelekea msimu mpya. Ameongeza kuwa kila shabiki alifanya kile anachoamini kitawapa nguvu. Amewaomba mashabiki kuendelea na mshikamano huo.

“Kwenye paredi mashabiki walichimba dawa, na hii imetokana na ubora wa Yanga SC. Hivyo kitendo cha mashabiki kufika pale na kutafuta dawa inayowapa mafanikio itakuwa nguvu kwetu kuelekea msimu mpya. Mashabiki tunawaomba waendelee kuwa nasi kuelekea msimu ujao wa 2026/27,”. aliongea Ahmed kwenye mahojiano na Haji Manara mtangazaji wa Crown Media.

Simba SC vs Yanga SC ni Agosti 12,2026

Msimu mpya wa 2026/27 unatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 12,2026. Mchezo wa Ngao ya Jamii utawakutanisha wababe hawa wawili. Mshindi wa taji la NBC Premier League ambaye ni Yanga SC vs mshindi wa CRDB Federation Cup ambaye ni Simba SC.

Simba SC na Yanga SC kambi 2026/27

Maandalizi ya msimu mpya yanaendana na chaguo la kambi kwa timu. Simba SC wanatarajiwa kuwa katika kambi. Simba SC inatarajiwa kuwa ukanda wa Afrika Mashariki kati ya Kenya na Rwanda kwa maandalizi. Yanga SC wao wanatarajiwa kuanza kambi AVIC Town, Kigamboni.

Takwimu za Yanga SC 2025/26

KipengeleTakwimu
Mechi Zilizochezwa30
Ushindi23
Sare6
Vipigo1
Mabao ya Kufunga71
Mabao ya Kufungwa9
Tofauti ya Mabao+62
Pointi75
Nafasi Kwenye Jedwali1

Takwimu za Simba SC 2025/26

KipengeleTakwimu
Mechi Zilizochezwa30
Ushindi22
Sare7
Vipigo1
Mabao ya Kufunga54
Mabao ya Kufungwa11
Tofauti ya Mabao+43
Pointi73
Nafasi Kwenye Jedwali2

Hitimisho

Ni Simba SC na Yanga SC maandalizi msimu mpya 2026/27 yameanza kimyakimya. Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF) Wallace Karia amebainisha kuwa ligi inatarajiwa kuanza rasmi Agosti 14,2026. Msimu mpya unatarajiwa kufunguliwa kwa mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 12 na unatarajiwa kufika tamati Mei 16,2027.

Share this: