Denis Kibu kwenye Msafara wa Simba uliotua DarDenis Kibu kwenye Msafara wa Simba uliotua Dar

Mara baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ugenini, msafara wa kikosi cha Simba leo Ijumaa asubuhi umetua rasmi Tanzania.

n
Yusuph Kagoma; Simba

Simba wamerejea nchini huku wakitangaza wazi kuwa wanaanza maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao unatarajiwa kupigwa Aprili 9, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

TUJIKUMBUSHE MCHEZO WA KWANZA

n
Elie Mpanzu; Source Simba

Simba ilipoteza mchezo wa kwanza ambao ulipigwa katika dimba la Suez Canal huko Isamailia ambapo katika mchezo hu oni nyota, Abderahim Deghmoum aliwapatia Al Masry bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti kali la mguu wa kushoto nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango, Moussa Camara.

Baada ya bao hilo Simba waliongeza utulivu na kucheza kwa ungalifu huku wakihakikisha wanawanyima nafasi wapinzani wao ili wasiweze kuwadhuru na Simba kufanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa ambazo hazikuzaa matunda.

Kipindi cha pili Simba waliongeza kasi na kulifikia zaidi ya lango la Al Masry ingawa walikuwa walinzi wa wenyeji walikuwa imara kuhakikisha hawaruhusu bao.

John Okoye aliwapatia Al Masry bao la pili dakika ya 90 akimalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka upande wa kushoto wa uwanja ambao walinzi wa mnyama walishindwa kuukoa.

NGOMA KURUDIWA JUMATANO KWA MKAPA

n
Uwanja wa Benjamin Mkapa

Mara baada ya mchezo huo, sasa kila timu inaseti mipango yake kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili ambao unatarajiwa kupigwa Jumatano ijayo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mshindi wa jumla atatinga nusu fainali ya mashindano hayo.

Katika mchezo huo wa Jumatano Simba ina mlima mrefu ambapo itahitaji kuhakikisha inapata ushindi wa mabao 3-0 au zaidi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya nusu Fainali ya mashindano hayo.

Ikumbukwe kikosi cha Simba katika mchezo wa kwanza kiliundwa na mastaa hawa; Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu, Ngoma, Ateba (Mukwala 78′), Ahoua, Mpanzu.

ALICHOSEMA KOCHA SIMBA

Fadlu Davids (-)
Fadlu Davids

Kuelekea mchezo huo wa marudiano kocha mkuu wa Simba, Fadlu ameweka wazi kuwa wachezaji wake wanajua kazi iliyo mbele yao na wanaendelea kuandaliwa kimwili na kiakili kuhakikisha wanacheza bila presha ili kufanikisha malengo waliyojiwekea, licha ya kukiri kuwa utakuwa mchezo mgumu lakini wamejiandaa kufanya vizuri.

Fadlu ameongeza kuwa tangu mwanzo walikuwa wakijua mechi ya pili itakayopigwa jijini Dar es Salaam ndio itaamua nani wa kufuzu nusu fainali na wamejipanga kutumia faida ya kucheza nyumbani kufanikisha hilo.

“Itakuwa mechi ngumu, lakini tumejiandaa vizuri. Kikosi chetu kitapata muda mzuri wa maandalizi na kufanya mazoezi kuelekea mchezo huo na naamini tuna nafasi ya kubadilisha matokeo.

“Tunatarajia mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa uzoefu wa wapinzani, lakini tumewaandaa wachezaji vyakutosha kuhakikisha tunapata matokeo chanya. Nilisema Al Masry wana kocha mpya na wana kikosi imara ambacho kinaweza kuleta ushindani mkubwa dhidi ya timu yoyote.”

SIMBA KUVAANA NA MBEYA CITY ROBO FAINALI FA

n
Lionel Ateba akipambana na walinzi wa Al masry

Ukiachana na kibarua hiko kigumu kwa mnyama kuelekea mchezo wa marudiano, pia wana kazi kubwa katika mashindano ya ndani ambapo droo ya robo fainali ya michuano ya CRDB BANK federation cup imekamilika na wao wamepangwa na Mbeya City kutoka Mbeya inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza (Championship)

Katika mchezo huo ambao mnyama ndio anatarajiwa kuwa mwenyeji itapigwa kati ya Aprili 11-13 katika Uwanja wa KMC Complex. Mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Singida Black Star na Kagera Sugar katika mchezo wa nusu fainali ambao nao unatarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 25-27.

Ikumbukwe Simba imepata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Bigman FC 2-1 kwenye mechi ya hatua ya 16 bora iliyopigwa Uwanja wa KMC Complex, Machi 27, mwaka huu. Simba ikiwa ndio timu pekee ya Tanzania ambayo haijatolewa kwenye mashindano yoyote mpaka sasa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.