- FT: Simba 6-1 Mighty Wanderers, Septemba 13, 2026 Uwanja wa Uhuru, Dar mchezo wa hatua ya awali CAF Champions League
- Mabao ya Clatous Chama, Libase Gueye yamefungua njia kwa mnyama kusonga hatua inayofuata
- Simba SC inafuzu kwa jumla ya mabao 7-1 baada ya mchezo wa awali ugenini, Uwanja wa Bingu kushinda 1-0.
Ngoma imeisha Simba SC 6-1 Mighty Wanderers ni matokeo rasmi katika mchezo wa hatua ya awali CAF Champions League. Mabao yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 7 na 34, Libase Gueye dakika ya 26 na 69, Keletso Makgalwa dakika ya 88 na Morice Abraham dakika ya 90. Bao pekee la Mighty Wanderers limefungwa na IIsaac Kaliati kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44 kipindi cha kwanza. Mnyama anafuzu hatua inayofuata ya mashindano ya CAFCL kwa jumla ya mabao 7-1.
Lineups Simba SC vs Mighty Wanderers: Simba SC vs Mighty Wanderers CAF Champions League | Odds | Hiki hapa kikosi cha Simba SC | SportPesa Blog
Bado hujashinda mamilioni ya SportPesa?
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Bashiri na SportPesa uvune mkwanja sasa hivi kwa kubonyeza picha hapo chini.

Taarifa muhimu Simba SC 6-1 Mighty Wanderers

| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | Ligi ya Mabingwa Afrika |
| Hatua | Hatua ya awali |
| Tarehe | Septemba 13, 2026 |
| Uwanja | Uhuru |
| Matokeo | Simba SC 6-1 Mighty Wanderers |
H2H Simba SC vs Mighty Wanderers
| Tarehe | Matokeo | Timu mwenyeji |
| Septemba 6, 2026 | Mighty Wanderers 0-1 Simba SC | Mighty Wanderers |
| Septemba 13, 2026 | Simba SC 6-1 Mighty Wanderers | Simba SC |
Simba SC imeshinda nje ndani
Mnyama amepata matokeo nje ndani dhidi ya Mighty Wanderers kwenye hatua za awali. Jumla ni mabao 7 ameshinda akiruhusu kufungwa moja akiwa nyumbani. Mchezo wa ugenini bao la ushindi lilifungwa na Anicet Oura ambaye katika mchezo wa pili ametoa pasi mbili za mabao. Alianza kwa Clatous Chama dakika ya 7 na Gueye dakika ya 69.
Mzawa Morice Abraham chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker amefunga bao lakufungia hesabu dakika ya 90. Winga huyo alipachika bao akitumia pasi ya Kalesto na wote waliingia kipindi cha pili. Morice aliingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Clatous Chama.
Hitimisho
Simba SC 6-1 Mighty Wanderers ni ushindi mkubwa katika anga za kimataifa. Mnyama ameandika rekodi tamu akiwa nyumbani kwa msimu wa 2026/27. Kazi bado haijaisha kwa mechi zinazofuata ambazo ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa zaidi.

