UKIZUBAA ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara unaachwa mazima ambapo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamid inapambania kutetea taji la ligi msimu wa 2024/25 kuna suala la tuzo za wachezaji nalo linavita kubwa.
Ipo wazi kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kete yake ijayo ni dhidi ya Coastal Union, Aprili 7 Uwanja wa KMC ambapo wakiwa uwanjani unanafasi yakuvuna mkwanja ukibashiri na SportPesa.
KESI ILIANZIA HUKU

Ikumbukwe kwamba kwa msimu wa 2023/24 tuzo ya mfungaji bora ilikwenda kwa Aziz Ki ambaye alitupia jumla ya mabao 21 na alikuwa kwenye vita kali na kiungo mzawa Feisal Salum wa Azam FC aliyefunga msimu akiwa katupia mabao 19.
Katika mabao hayo 21 ya Ki wa Yanga alifunga jumla ya mabao 17 akitumia mguu wa kushoto na Feisal aligotea kufunga mabao 4, Feisal alikuwa namba moja kwa kutumia mguu wa kulia alipofunga mabao 13 na Ki alifunga matatu pekee.
Nyota hawa wawili walikuwa wakali wakiwa ndani ya 18 ila Feisal alikuwa na hatari zaidi ambapo alifunga jumla ya mabao 17 akiwa kwenye eneo hilo, Aziz Ki alifunga jumla ya mabao 15 akiwa ndani ya 18. Hivyo alizidiwa mabao mawili pekee kwenye ukali wa kutupia mabao ndani ya 18.
Nje ya 18 Aziz Ki alitupia mabao sita akiwa nje ya 18. Miongoni mwa timu aliyofunga akiwa nje ya 18 ilikuwa dhidi ya Tabora United alipofunga bao lake la 10 ndani ya ligi ilikuwa kwa pigo huru akitumia mguu wake wa kushoto.

Feisal alitupia mabao mawili akiwa nje ya 18. Bao lake la19 la kufungia msimu alipachika akiwa nje ya 18 dhidi ya Geita Gold walipokomba pointi tatu mazima ugenini.
MABAO WALIYOHUSIKA
Aziz Ki alihusika kwenye mabao 29 kati ya 71 yaliyofungwa na Yanga ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24. Ipo wazi kwamba Yanga ilikuwa ni namba moja kwa timu ambazo zilifunga mabao mengi na safu yao ya ulinzi iliruhusu mabao machache ambayo ni 14.
Feisal alihusika kwenye mabao 26 kati ya 63 yaliyofungwa na Azam FC timu hiyo ikiwa ni namba mbili kwa timu zilizofunga mabao mengi. Ukiweka kando kuwa namba mbili kwa safu kali ya ushambuliaji na ile ya ulinzi ni namba mbili ikiwa iliruhusu mabao 21.
MADENI YAO KWA SASA
Mastaa hao wawili ndani ya ligi upepo umebadilika ambapo kiungo Feisal msimu wa 2024/25 katupia mabao manne akiwa namba moja kwa wakali wakutengeneza pasi za mwisho ambazo ni 12 kahusika kwenye mabao 16 kati ya 38 yaliyofungwa na Azam FC ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo. Fei ni deni la mabao 15 anadaiwa kuvunja rekodi yake.
AZIZ KI
Kiungo bora wa msimu wa 2023/24 Aziz Ki ni mabao 7 kafunga na kutengeneza pasi 7 za mabao kahusika kwenye mabao 14 kati ya 61 yaliyofungwa na timu hiyo ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 61. Ki ni deni la mabao 14 anadaiwa kufikia rekodi yake msimu uliopita.
Mbali na kuongoza ligi, Yanga safu yake ya ushambuliaji baada ya mechi 23 ambazo ni dakika 2,070 ni namba moja kwenye utupiaji ikiwa na mabao 61 wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 33.
VITA IMEANZA UPYA SASA
Imeanza upya kwa sasa vita ya ufungaji bora msimu wa 2024/25 kukiwa na balaa zito kutokana na kila mchezaji kuwa na nyota kweye kucheka na nyavu ndani ya ligi kuu bara ambayo ni namba nne kwa ubora.

Clement Mzize nyota anayetimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga huyu ni mzawa pekee mwenye mabao mengi ndani ya chati ya wafungaji bora akiwa katupia mabao 11 kibindoni sawa na Prince Dube raia wa Zimbabwe.
Ukiweka kando nyota hao wawili wa Yanga wenye mabao 11 kinara kwa wakati huu mzunguko wa pili ni Jean Ahoua kiungo wa Simba ana mabao 12 yeye ni raia wa Ivory Coast. Hivyo kwenye chati ya utupiaji wageni wamekuwa na zali lakucheka na nyavu zaidi.

Steven Mukwala raia wa Uganda ni mali ya Simba huyu ni mabao 9 katupia, Elvis Rupia raia wa Kenya yupo Singida Black Stars mabao 9, Gibrill Sillah wa Azam FC huyu ni Mgambia, Jonathan Sowa mali ya Singida Black Stars ni Mghana, Peter Lwasa raia wa Uganda yupo Kagera Sugar na Leonel Ateba wa Simba raia wa Cameroon hawa wote wana mabao 8.
Ligi namba nne kwa ubora Afrka kwa sasa ni mzunguko wa pili kila timu inapambana kutimiza malengo yake na msako ni mkali kwa timu ambazo zinapambania kutwaa ubingwa na zile ambazo zinapambania kutoshuka daraja.

