Al Hilal Vs YangaAl Hilal Vs Yanga

Wawakilishi wa Tanzania kimataifa timu za Simba na Yanga leo Jumapili wanashuka Uwanjani kuibeba Tanzania katika vita ya kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya kimataifa, ambapo ikumbukwe Simba ni wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku Yanga wao wakituwakilisha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kumbuka unaweza kujishindia pesa nyingi leo kwa kubashiri matokeo ya michezo hii na mingine mingi kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa yenye odds kubwa kwa kutembelea www.sportpesa.co.tz

SIMBA
Aziz Ki

SIMBA SARE TU, YANGA USHINDI MUHIMU

Simba wao wapo nchini Angola ambapo leo wana kibarua kigumu cha kuwavaa Bravos huku wakiwa wanahitaji angalau matokeo ya sare tu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kufuzu Robo Fainali, huku Yanga wao wakiwa nchini Mauritania ambapo watavaana na mwenyeji wao, Al Hilal ambapo Yanga wanahitaji matokeo ya ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza Robo Fainali.

SIMBA
Mpanzu na Debora-Mastaa wa Simba wakijifua Angola

Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa kundi A la Kombe la Shirikisho Afrika na pointi zao 9 ambazo wamekusanya katika michezo minne ya awali huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wao uliopita dhidi ya CS Sfaxien ugenini nchini Tunisia.

Katika mchezo huo ambao ulipigwa Jumapili iliyopita bao pekee la ushindi kwa Simba lilifungwa na kiungo wao wa kimataifa wa Ivory Coast, Jean Charles Ahoua.

SIMBA WATAMBA KUTINGA ROBO FAINALI KIBABE

Kuelekea mchezo huo wa leo jioni, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa ushindi walioupata ugenini dhidi ya Sfaxien, ulikuwa muhimu lakini amekiri kuwa licha ya kuwa karibu kufanikisha malengo yao bado wana kazi kubwa ya kufanya kutokana na ugumu wa mechi dhidi ya Bravo.

SIMBA
Ahmed Ally

“Kuelekea mchezo huu dhidi ya Bravo kwanza tunajivunia kikosi chetu na kazi kubwa tuliyoifanya kwenye mchezo uliopita nchini Tunisia, tumeshinda ugenini hii ni furaha kwetu lakini bado hatujamaliza tuna kazi nyingine yakufanya kwenye mechi hii ili kujihakikishia nafasi ya Robo fainali kabla ya mchezo wa mwisho nyumbani.

“Kama mmefuatilia mtagundua kuwa mechi yetu dhidi ya Bravos mashabiki walikuja wachache, mechi yetu ya pili dhidi ya SC Sfaxine pia haikuwa na mashabiki wengi, sasa kwenye mechi yetu ya mwisho funga kazi dhidi ya Costantine tunahitaji mashabiki waujaze Uwanja wa Mkapa.”

KIKOSI CHA SIMBA KILICHOTUA ANGOLA KUIVAA BRAVOS

Makipa

Mousa Camara, Hussein Abel na Ally Salim

Mabeki

Karabou Chamou, Che Malone, Abdulazack Hamza, Zimbwe Jr, Shomari Kapombe, Kelvin Kijili

Viungo

Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, Yusuph Kagoma, Elie Mpanzu, Augustine Okejapha, Kibu Dennis, Deborah Mavambo, Ladack Chasambi, Awesu Awesu, Jean Ahoua, Edwin Balua.

Washambuliaji

Valentino Mashak ana Lionel Areba

BRAVO WALIKUFA DAR

Kumbukumbu ya mchezo wa mwisho baina ya timu hizo walipokutana Dar es Salaam Bravos ilipoteza mchezo kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-0 Bravos ambapo bao pekee la Simba lilifungwa na kiungo, Jean Ahoua ambaye mpaka sasa kimataifa kaweka kambani mabao mawili na kuasisti mara mbili.

YANGA KULIPA KISASI KWA IBENGE?

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga nao leo watashuka uwanjani kuvaana na Al Hilal ya kocha, Florent Ibenge. Yanga wanahitaji sana matokeo ya ushindi katika mchezo wa leo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya Robo Fainali katika mchezo ambao unatafsiriwa kuwa ni mchezo wa kisasi kwani Yanga hawajawahi kuifunga Al Hilal ya Ibenge katika michezo mitatu mfululizo waliyokutana katika siku za karibuni.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwenye mchezo wake uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika ilivuna pointi tatu ikiwa Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe.

Ikumbukwe kwamba kwenye kundi A Yanga ipo nafasi ya tatu wakiwa wamevuna pointi nne wanakwenda kukutana na vinara kwenye kundi wenye pointi 10 ambao katika mchezo waliokutana nao Uwanja wa Mkapa, Yanga ilipoteza kwa kipigo cha mabao 2-0.

YANGA WANASEMAJE?

Kocha wa zamani wa Azam na KMC ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Yanga, Abdihamid Moalin amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Al Hilal utakuwa mgumu, lakini wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa Yanga.

“Tunauendea mchezo huu tukiwa na imani kwamba tutapata pointi tatu muhimu, tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari na wachezaji wanajua kwamba huu ni mchezo muhimu kwetu kutafuta pointi tatu, kikubwa ni utayari na mchezo, ipo wazi kwamba walipata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita, tutapambana kupata matokeo mazuri,” amesema Moalin.

SIMBA
Ali Kamwe

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kuelekea mchezo huo: “Maandalizi yetu ni mazuri na kuna wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa bado hawajawa fiti, Clatous Chama yeye yupo tayari kwa ajili ya kutumika, tunakwenda kwa kujiamini kuwa tuna nafasi na inawezekana.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.