YANGA wamebainisha kuwa hesabu kubwa kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ni kupata pointi tatu ndani ya dakika 90 ili kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na utakuwa ni mchezo wa kwanza ugenini 2025

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa kwenye mchezo wake uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika ilivuna pointi tatu ikiwa Uwanja wa Mkapa kwa ushindi wa mabao 3-1 baada ya dakika 90 wakisepa na pointi tatu muhimu.
Ikumbukwe kwamba kwenye kundi A Yanga ni nafasi ya tatu wakiwa wamevuna pointi nne wanakwenda kukutana na vinara kwenye kundi wenye pointi 10 ambao katika mchezo waliokutana nao Uwanja wa Mkapa, Yanga ilipoteza pointi tatu.
MCHEZO KUPIGWA HAPA
Mchezo wao ujao Yanga ikiwa ugenini unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa de la Capitale ambapo Yanga watashuka uwanjani wachezaji kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90 ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.
Ipo wazi kwamba timu hiyo itatumia mbinu za Kocha Mkuu, Sead Ramovic kusaka pointi tatu muhimu wakiwa na kumbukumbu yakupoteza mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Yanga 0-2 Al Hilal.
Al Hilal tayari imeshakata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na pointi 10 katika kundi A inakutana na Yanga yenye pointi nne ikiwa nafasi ya tatu.
HUYU HAPA KOCHA MSAIDIZI

Kocha Msaidizi wa Yanga, Abdihamid Moalin amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Al Hilal utakuwa ni mgumu lakini wapo tayari kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu kutokana na umuhimu wa mchezo huo kwa Yanga.
Ikiwa Yanga itapata pointi tatu kwenye mchezo huo itabakiwa na mchezo mmoja Uwanja wa Mkapa ambao huo utaamua hatima ya timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo huo Yanga inatambua kwamba wapinzani wao wanatumia nguvu nyingi kwenye mipira ya kushtukiza huku ulinzi wao ukiwa imara kwa kuwa nit imu yenye safu imara ya ulinzi.
Kocha huyo amebainisha kwamba wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na wanakwenda wakiwa na ari ya kusaka ushindi ndani ya dakika 90 hivyo wataingia kwa tahadhari kusaka ushindi kwenye mchezo huo mgumu.
“Tunakwenda tukiwa na Imani kwamba tutapata pointi tatu muhimu, tunatambua kwamba hautakuwa mchezo mwepesi lakini tupo tayari na wachezaji wanajua kwamba huu ni mchezo muhimu kwetu kutafuta pointi tatu muhimu.
“Kikubwa ni utayari na mchezo wetu upo wazi kwamba walipata ushindi kwenye mchezo wetu uliopita, tunahitaji kufanya vizuri katika mchezo wetu na tupo tayari mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi na tutapambana kupata matokeo mazuri.”
HUYU HAPA SEMAJI YANGA

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa maandalizi yapo vizuri kuelekea mchezo huo ambapo wapo wachezaji ambao watakosekana kwenye mchezo wetu na malengo ni kuona tunatinga hatua ya robo fainali.
Kikubwa kwenye mchezo wetu ni kupata matokeo na hilo linawezekana kwa kuwa wachezaji wapo tayari kwa mapambano hivyo tunakwenda tukijiamini tunajua kwamba wapo ambao wanafikiria tofauti ila malengo yetu ni kuona tunapata ushindi hilo linawezekana.
“Kuna wachezaji ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa bado hawajawa fiti ambapo ni Aziz Andambwile, Yao na Maxi hawa bado hawajaimarika na ushauri wa madaktari ni kwamba waendelee kuwa chini ya uangalizi maalumu.

“Lakini Clatous Chama yeye yupo tayari na ameanza mazoezi na wachezaji wenzake atakuwa sehemu ya msafara kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Al Hilal.
“Licha ya wachezaji wengine kukosekana bado tunakwenda kwa kujiamini unajua hatua hii kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kila timu ni kubwa kinachotakiwa ni kuheshimiana na kuchukua tahadhari kila kitu kinawezekana hakuna namna.

“Tumepata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu uliopita dhidi ya TP Mazembe hilo linaongeza nguvu kuelekea mchezo wetu ujao na wachezaji wana ari kubwa kuhakikisha kwamba wanapambana na kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua.”

