Washindi Mid-week JackpotWashindi Mid-week Jackpot

SPORTPESA YATOA SHILINGI BILIONI 1,130,403,843 KWA WASHINDI SITA

  • Washindi 6, kila mmoja akiondoka na Sh. 188,403,843.
  • Baada ya kubashiri kwa usahihi mechi zote 13/13 za Mid-week Jackpot.
SPORTPESA
Frank Joseph akipokea hundi yake

Dar es Salaam, Oktoba 30, 2024 – Kampuni inayoongoza kwa ubashiri wa michezo na burudani, SportPesa, leo imetangaza rasmi washindi sita wa Mid-week Jackpot, ambapo jumla ya shilingi bilioni 1,130,423,060 zimelipwa kwa washindi wote, kila mmoja akipokea TZS 188,403,843 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13 kati ya 13.

Kuhusu Washindi wa SportPesa Mid-week Jackpot

SPORTPESA
Washindi wa Mid-week Jackpot

Washindi hawa sita wanatoka katika mikoa tofauti nchini, ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Geita, na Lindi. Hii inaonyesha ushiriki wa kitaifa wa mchezo wa Mid-week Jackpot na ushindi wa kipekee kwa washiriki wa mikoa mbalimbali. Orodha ya washindi ni kama ifuatavyo:

  1. Mwangwa Imori Mwibuli – Mtumishi wa Umma, miaka 35, kutoka Kibiti, Pwani.
  2. Frank Joseph Buchweishaija – Mfanyabiashara, miaka 36, kutoka Dar es Salaam.
  3. Colonel Moses Keyu – Mfanyabiashara, miaka 30, kutoka Geita.
  4. Martin Bruno Bagule – Mfanyakazi wa Sekta Binafsi, miaka 30, kutoka Dar es Salaam.
  5. Daud Leonard Sahani – Mwalimu, miaka 31, kutoka Ruangwa, Lindi.
  6. Mirambo Magesa Mswaga – Mvuvi, miaka 29, kutoka Geita.

Mbali na zawadi kuu, washindi watano kati yao walipokea malipo ya ziada kupitia muundo wa ‘double combinations’ ambao umewapa nyongeza kutokana na kuongeza nafasi za ushindi. Malipo ya ziada kwa kila mshindi ni kama ifuatavyo:

  • Mwangwa, Frank, na Colonel – TZS 2,850,974 kwa double combinations 128.
  • Martin – TZS 2,184,444 kwa double combinations 64.
  • Daud – TZS 1,622,420 kwa double combinations 32.

Katika hafla fupi ya kuwatangaza washindi hao iliyofanyika kwenye Peninsula House, makao makuu ya SportPesa, washindi walikabidhiwa hundi za mfano na kutambulishwa rasmi kwa umma. Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa, Bw. Tarimba Abbas, aliwapongeza washindi hao kwa ushindi huu mkubwa na wa kihistoria.

Tarimba Abbas Awapongeza Washindi

SPORTPESA
Abbas Tarimba (Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa)

“Kwa niaba ya kampuni ya Sportpesa, ni furaha yangu kubwa sana kuwatangaza washindi wetu sita wa Mid-week Jackpot ambao wameshinda jumla ya TZS 1,130,423,060 ambapo kila mmoja amepokea TZS 188,403,843,” alisema Bw. Abbas.

“Hili ni jambo la kihistoria kwa kampuni, hasa kwa kuwa mara ya mwisho tumepata mshindi wa Mid-week Jackpot ilikuwa mwaka 2022.”

Bw. Tarimba Abbas aliwahimiza wateja wa Sportpesa waendelee kuamini kuwa ushindi ni wa kweli na uwezekano upo.

“Katika kipindi cha miaka saba tangu kuanzishwa kwa SportPesa, tumefanikiwa kutangaza maelfu ya washindi wa bonasi na Jackpots. Ushindi ni halisi na unawezekana,” alisema.

Mshindi wa Mid-week Jackpot atoa Maoni yake

SPORTPESA
Daud Sahani (Mshindi wa Mid-week Jackpot)

Daud Leonard Sahani, mmoja wa washindi mwenye umri wa miaka 31 na ambaye ni mwalimu kitaaluma kutoka mkoani Lindi, alielezea furaha yake baada ya kushinda Jackpot. “Nimekuwa nikicheza na SportPesa kwa muda mrefu sasa, baada ya kuifahamu kupitia magazeti na marafiki. Mara kwa mara nimeshiriki katika Jackpot zote – SUPA Jackpot yenye mechi 17 na hii ya katikati ya wiki yenye mechi 13,” alisema Daud.

Aliongeza, “Nilicheza mkeka wangu wa Mid-week Jackpot tarehe 24 Oktoba 2024 na nikafanikiwa kubashiri kwa usahihi mechi zote 13. Kiasi hiki cha pesa kitakwenda kugusa maisha yangu kwa namna nyingi, na itakwenda kubadilisha maisha yangu. Kwa sasa siwezi kusema nitafanyia nini pesa hizi, lakini itoshe kusema zinakwenda kubadili hali yangu ya maisha na kiuchumi.”

Aliendelea kwa kusema: “Baada ya kuweka mkeka wangu wa Mid-week Jackpot nilienda kulala. Taarifa niliipata asubuhi baada ya kuamka ambapo mwanzo sikuamini, lakini baada ya kupigiwa simu na kufika hapa ofisini nikapata uhakika juu ya ushindi wangu. Kwa kweli mambo yanakwenda kuwa vizuri na nina furaha kubwa.”

Tofauti ya SportPesa na Wengine Kwenye Jackpot

Daud alifafanua kuwa, licha ya kuwepo kwa makampuni mengi ya kubashiri, amekuwa akivutiwa na SportPesa kwa sababu ya uaminifu wake, ofa kubwa, na malipo ya haraka.

“Ujumbe wangu kwa Watanzania wote ambao wanatamani kushinda na kutimiza malengo yao ni kuwa waendelee kucheza na SportPesa, hata kama bado hawajashinda waamini kuwa ipo siku watashinda kama mimi nilivyoshinda,” alisema Daud kwa msisitizo.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Asisitiza Ushiriki Zaidi

SPORTPESA
Tracy Humplick (Mkuu wa kitengo cha masoko SportPesa)

Mkuu wa Kitengo cha Masoko, SportPesa, Bi. Tracy Humplick, alitoa pongezi kwa washindi wote na kuwasihi wawe mabalozi wa SportPesa kwa wengine. “Kwanza niwapongeze sana washindi wetu wa Mid-week Jackpot kwa ushindi huu mkubwa. Nyie ni kati ya Watanzania wengi wanaopambana kimaisha na kujaribu njia tofauti za kutafuta pesa,” alisema Bi. Humplick.

Alisisitiza kuwa, “Nawakumbusha wateja wetu wote kwamba Jackpot bado ipo na itaendelea kuwepo. Endeleeni kubashiri na pia wekeni double combinations ili kuongeza nafasi za kushinda. Pia, kuna ‘Quick Pick’ inayopatikana kwenye tovuti www.sportpesa.co.tz na aplikesheni ya SportPesa kwa wale wanaohitaji usaidizi wa kubashiri haraka na kwa urahisi.”

Kwa kuhitimisha, SportPesa inaahidi kuendelea kutoa huduma bora na nafasi zaidi za ushindi kwa wateja wake kote nchini, ikiwapa nafasi ya kutimiza malengo na kubadilisha maisha yao kwa njia ya ubashiri wenye uaminifu.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.