MSAKO wa pointi tatu haukuwa wa kitoto kwa wababe wawili uwanjani Coastal Union ya Tanga dhidi ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye alishuhudia wachezaji wake wakisepa na pointi tatu muhimu baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma Coastal Union 0-1 Yanga.

Mwamuzi wa kati alikuwa ni Abel William ambaye alikuwa alikuwa akisimamia sheria 17 za mpira kwa timu zote kupambania kusepa na pointi tatu muhimu mwisho Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ilikomba pointi hizo mazima ikiwa ugenini.
Katika dakika 15 za mwanzo Coastal Union walikosa nafasi ya kufunga ambapo kipa namba mbili wa Yanga, Abobhakari Khomeiny alianza langoni ukiwa ni mchezo wake wa kwanza baada ya Djigui Diarra kukosekana katika mchezo huo kutokana na adhabu ya kati za njano.
Hapa tunakuletea rekodi za baadhi ya mastaa kwa timu zote mbili ndani ya uwanja kwenye kuonyeshana balaa uwanjani ilikuwa namna hii:-
COASTAL UNION
RAMADHAN CHUMA
Ramadhan Chuma alianza kikosi cha kwanza na alitunguliwa bao moja ilikuwa dakika ya 24 na Jean Baleke wa Yanga, aliokoa hatari dakika ya 20, 88, 89 alitumia mguu wa kulia dakika ya 20 kupiga pasi ndefu.
JUMA MAABAD
Maabad Juma huyu alianza kikosi cha kwanza kwa Coastal Union, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 23, alicheza faulo dakika ya 61 kwenye mchezo huo ambao walipoteza pointi tatu.
LUKAS KIKOTI
Kiungo wa Coastal Union mwenye jezi namba 8 mgongoni alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika ya 13, 19.
GELAD GWALALA
Alikuwa kwenye ubora wake mwamba huyu alionyesha uwezo wa kukokota mpira dakika ya 55, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 71.
ABDALLAH HASSAN
Nyota huyu alicheza faulo dakika ya 62 na alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi William Abel dakika ya 62, alichezewa faulo dakika ya 73.
HAWA HAPA MASTAA WA YANGA
ABOUBAKAR KHOMEINY
Kipa huyu alikomba dakika 90 kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Yanga ugenini aliokoa hatari dakika ya 12, 23, 44, 63, 75 alipiga pasi ndefu dakika ya 26.
Licha ya kuwa ni kipa alipewa jukumu la kupiga faulo ilikuwa dakika ya 45, 61 kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi msimu wa 2024/25.
KHALID AUCHO
Kiungo huyu wa kazi ngumu alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 59 alicheza faulo nyingine dakika ya 13 kwenye mchezo huo ambapo alichezewa faulo dakika ya 23 wakati akitoa pasi ya bao kwa Jean Baleke.
IBRAHIM BACCA
Alianza kikosi cha kwanza na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 44aliokoa hatari dakika ya 15 kwenye mchezo huo wakiwa ugenini.

JEAN BALEKE
Jean Baleke lifunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Yanga kwenye ligi lifunga dakika ya 24 akiwa ndani ya 18 alicheza faulo dakika ya 22.
BOKA
Beki wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Yanga, Boka alipiga krosi dakika ya 62, alichezewa faulo dakika ya 62.
AZIZ KI
Aziz Ki alichezewa faulo dakika ya 19, 64 alipiga faulo dakika ya 20 kwenye mchezo huo alikomba dakika 65 nafasi yake ilichukuliwa na Prince Dube ambaye alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 66, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 89.

MUDATHIR YAHYA
Alicheza faulo dakika ya 67, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya dakika 90.
BAKARI NONDO
Nyota huyo alianza kikosi cha kwanza alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 44 aliokoa hatari dakika ya 20, 54.
PACOME
Kiungo huyu aliingia dakika ya 65 akichukua nafasi ya Jean Baleke, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 73, alichezewa faulo dakika ya 87 alipiga krosi dakika ya 89 na alipewa jukumu la kupiga kona dakika ya 89.
MAXI NZENGELI

Kiungo wa kazi Max alipiga krosi dakika ya 22 alipiga kona dakika ya 24 na alikomba dakika 65 nafasi yake aliingia Clatous Chama ambaye alichezewa faulo dakika ya 77, alipiga faulo dakika ya 78 ikiwa ni shuti ambalo halikulenga lango, alicheza faulo dakika ya 90.
Kiungo Maxi ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ametupia mabao matatu msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa. Ni yeye alifungua rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, ubao uliposoma Kagera Sugar 0-2 Yanga.

