Sillah GibrilSillah Gibril

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imepoteza mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi msimu wa 2024/25 kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Yanga 0-1 Azam FC baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Ipo wazi kwamba Yanga ilicheza mechi 8 mfululizo ambazo ni dakika 720 bila kufungwa ndani ya uwanja, rekodi hiyo imetibuliwa kwenye mchezo wa 9 dhidi ya Azam FC kwa kufungwa na kupoteza pointi tatu muhimu ambazo zimebebwa na Azam FC.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa, licha ya kupoteza mchezo huo imebainisha kuwa mpango kazi ni kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata kwa kuwa mpira una matokeo matatu.

 

 

Kamwe Ali
Kamwe Ali, Ofisa Habari wa Yanga, 2024/25. Source: Yanga.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amebainisha kuwa wapo ambao walikuwa wanasubiria kuona timu hiyo ikifungwa na imetokea hivyo wanapaswa wafurahi kwa kuwa ni maisha ya mpira na kuna mechi zinakuja hawapaswi kuwa wanyonge

“Wapo ambao wamefurahi Yanga kufungwa sio Azam FC pekee ambao wamefurahi hapana wapo wengi, lakini huu ni mpira na haya ni matokeo, kikubwa tunawapongeza Azam FC kwa ushindi huu kwani kwenye ligi kuna mechi nyingi.

“Kwa kilichotokea tunawapongeza wachezaji wetu unaona kwamba tulikuwa pungufu bado walicheza kwa jitihada kutimiza majukumu yao, mechi zijazo tunaamini tutapata matokeo mazuri.”

DIJGUI DIARRA

Alianza langoni aliokoa hatari dakika ya 25, 26, 47 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 79 alifungwa bao moja dakika ya 33 na Giblill Sillah. Alikomba dakika 90.

DICKSON JOB

Beki Dickson Job alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 2, alichezewa faulo dakika ya 32 alicheza faulo dakika ya 79, 90 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.

AUCHO

Khalid Aucho alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya 12, 63.

MAXI NZENGELI

Maxi Nzengeli alianza kikosi cha kwanza dhidi ya Azam FC alichezewa faulo dakika ya 14, 63 alicheza faulo dakika ya 65.

AZIZ KI

Aziz Ki alianza kikosi cha kwanza alipiga kona dakika ya 50, 51 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 52, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 87 alikomba dakika 71 nafasi yake aliingia Pacome.

BACCA

Ibrahim Bacca beki wa kazi alikwama kusepa na dakika 90 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 21 baada ya kumchezea faulo Saadun.

NONDO

Bakari Nondo alianza kikosi cha kwanza na alichezewa faulo dakika ya 60,65 alicheza faulo dakika ya 73, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 73.

MUDATHIR YAHYA

Nyota huyu wa zamani wa Azam FC alianza kikosi cha kwanza na alicheza faulo dakika ya 26, 59 alikomba dakika 85 nafasi yake ilichukuliwa na Kennedy Musonda.

BOKA/KIBABAGE

 

Kibabage
Kibabage beki wa kazi wa Yanga kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Source: Yanga.

Boka alianza kikosi cha kwanza kwenye kumwaga krosi alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 28 alikomba dakika 45 nafasi yake ilichukuliwa na Nickson Kibabage.

 

PRINCE DUBE

Alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 61 alicheza faulo dakika ya 40, 59 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 45. Alikomba dakika 62 nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize.

HAWA HAPA MASTAA WA AZAM FC

MOHAMED MUSTAPHA

Alianza langoni kwa Azam FC aliokoa hatari dakika ya 52, 61, 67, 81 na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90.

FEI TOTO

Toto Fei
Toto Fei kiungo wa Azam FC, 2024/25. Source: Azam FC.

Kiungo Feisal Salum alianza kikosi cha kwanza na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 9, alipiga kona dakika ya 45.

PASCAL MSINDO

Msindo alianza kikosi cha kwanza aliokoa hatari dakika ya alikomba dakika 74 nafasi yake ni Sidibe aliingia.

ADOLF MTASWIGWA

 

Mtasigwa v Kibabage
Mtasigwa v Kibabage kwenye mchezo wa ligi 2024/25. Source: Yanga.

Adolf Mtasigwa alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo alicheza faulo dakika ya 71 aliokoa hatari dakika ya 12.

IDD NADO

Kiungo huyu Idd Nado alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 45, alicheza faulo dakika ya 16, alichezewa faulo dakika ya 65.

NASSORO SAADUN

Nyota huyu alichezewa faulo dakika ya 21 na Bacca, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 62, alicheza faulo dakika ya 67, 85 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 85.

GIBRIL SILLAH

Alianza kikosi cha kwanza anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kuifunga Yanga kwenye ligi dakika ya 33 alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 31 alicheza faulo dakika ya 60.

 

Share this: