ANKARAGUCU vs GALATASARAY- Ni Utamu Kunoga Uturuki
Patashika ya kuusaka Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki itaendelea Jumanne hii ya Mei 30,2023 kwa mechi kati ya timu ya Ankaragucu watakapowakaribisha timu ya Galatasaray.
Vita kubwa kwa sasa ni kati ya vinara Galatasaray yenye alama 79, Fernebance iliyo katika nafasi ya pili ikiwa na alama 74 nayo Besiktas inazo alama 74 wapo kwenye nafasi ya tatu.
Mei 30, Ankaragucu watakuwa wenyeji wa Galatasaray, ambao wapo katika kiwango kizuri kabisa kwa sasa. Katika mechi 5 za hivi karibuni za msimu wa ligi Galatasaray wameshinda mechi 3, toa sare moja na kufungwa moja.
Hii inaonyesha ni kwa namna gani Galatasaray wana kiwango kinachoridhisha.
Wenyeji wa mchezo wa leo Ankaragucu wao hawana mwenendo mzuri. Katika mechi tano za hivi karibuni ambazo wameshacheza, Ankaragucu wameshinda mchezo mmoja pekee, wakipoteza mitatu na kutoa sare mmoja.
Pia Ankaraguku hawana rekodi nzuri dhidi ya wageni, pindi walipokutana na Galatasaray. Rekodi zinaonyesha wamepoteza mara 4 na sare moja katika michezo mitano ya mwisho waliyokutana, hivyo wageni wanaonekana wana nafasi kubwa ya kupata matokeo chanya ya mchezo huu wa leo.
Galatasaray wamekuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa kwenye soka la Ulaya kama Mauro Icard ambaye amecheka na nyavu mara 19 akifuatiwa na Kerem Akturkoglu aliyefunga baoa 9.
Mkongwe Bafetimbi Gomis ana magoli 8, akifuatiwa na Dries Mertens mwenye magoli 5.
Licha ya kufunga magoli hayo, Mshambuliaji Mauro Icardi anamchango mkubwa kwa kutoa pasi za mwisho za mabao (assist) (7), hivyo anakuwa ni mshambuliaji ambaye anatarajiwa kuwa mwimba kwa wenyeji katika mchezo wa leo.
Upande wa Ankaragucu wao wanao mastaa kadhaa ambao si haba katika kufunga mabao kwani wanaye Ali Sowe, Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Gambia ambaye ameshafunga mabao 12.
Vile Vile yupo Felicio Milson mshambuliaji wa kimataifa anayecheza winga ya kushoto kutoka Angola. Mshambuliaji huyu ana magoli 3, baada ya kucheza mechi 7. Kinda huyu mwenye umri wa miaka 23, ameaminiwa na kocha Tolunay Kafkas kwenye mchezo wa leo, kwa kuwa watamkosa mshambuliaji Giorgi Beridze, ambaye amefunga magoli manne.
Ushindi kwa Galatasaray utawafanya wafikishe alama 83 na kuwatoroka Fenerbance ambayo ina kibarua siku hiyo dhidi ya Antalyaspor.
Ankaragucu wao wapo nafasi ya 12 wakiwa na alama 39, ushindi kwao utawanyanyua hadi nafasi ya 10 na kuwashusha Alanyaspor wenye alama 44 lakini pia watawakimbia Antalyaspor ambao wapo nafasi ya 13 wakiwa na alama 38 ambao watakuwa na kibarua dhidi ya Fenerbance.
Fernebance walio kwenye nafasi ya pili katika msimamo wanapewa nafasi zaidi kushindi katika mchezo wao dhidi ya Antalyaspor kulingana na rekodi ya mechi za nyuma dhidi ya wapinzani wao kwani katika michezo mitano ya mwisho wameshinda mitatu na sare miwili.
Wenyeji wa mchezo huo iwapo watashinda wataendelea kutoa shinikizo kwa Galatasaray ambao nao watakuwa dimbani kama ratiba ilivyoonyesha hapo juu.
Klabu ya Fernabance nayo imekuwa ikisuwasuwa kwa mechi za karibuni, wamecheza mechi tano za mwisho na wameshinda michezo mitatu na kutoa sare miwili.
Wapinzani wa Fenerbance wao hali yao sio nzuri kwakuwa katika mechi tano za mwisho wameshinda mmoja pekee, wamepoteza michezo miwili na kutoa sare michezo miwili.
Antalyaspor wanajivunia uwepo wa mshambuliaji wao kinara Haji Wright aliyepachika mabao 15 hadi sasa wakati Fenerbance wana mastaa hatari kama Ener Valencia mwenye bao 28 wakati Michy Batshuay amefunga mabao 12.
Timu inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo ni Besiktas ambayo itateremka dimbani Juni 3,2023 ikiwa ugenini kukipiga dhidi ya Kasimpasa.
Kasimpasa wanashikilia nafasi ya 11 wakiwa na alama 40 wanahitaji alama 3 ili wajiimarishe nafasi yao ya katikati ya msimamo wakati iwapo Besiktas watashinda watategemea matokeo ya Fenerbance ambao watakuwa wamecheza Mei 30,2023.
Kocha wa Ankaragucu amesema Pamoja na kutokuwa na matokeo mazuri ya kuridhisha katika mechi za hivi karibuni, watajitahidi kupambana na kupata matokeo ili wasogee japo kwa nafasi moja juu ya Kasimpasa.
Naye kocha wa Galatasaray amesema ana imani wa kuondoka na ushindi hata kama mechi wanachezea ugenini kwa kuwa takwimu zao dhidi ya wapinzani wao zinawapa ari ya kutopoteza mechi hiyo.
Kama utapendelea kubashiri mechi hii basi tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#