Morocco x World CupMorocco x World Cup

Scotland vs Morocco: Utabiri, muda, vikosi, h2h na odds

  • Scotland vs Morocco ni ratiba ya mechi za mzunguko wa pili wa Kundi C Kombe la Dunia 2026, ambayo inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Gillette, Boston.
  • Mechi hii inatarajiwa kupigwa June 19, 2026 saa 12 jioni kwa saa za Marekanis awa na saa 7 usiku June 20, 2026 kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Kwa kuzingatia uchambuzi wa kina wa Opta Analyst, Morocco wanapewa nafasi kubwa ya asilimia 55.1% kushinda dhidi ya Bosnia and Herzegovina yenye asilimia 11.7
  • Timu hizi zimekutana mara moja tu, ilikuwa mwaka 1998 ambapo matokeo yalikuwa Morocco 3-0 Scotland, nakala hii inakuletea taarifa muhimu za mchezo huu; livescores, h2h, prediction, stats, results.

Scotland vs Morocco, utakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa Kombe la Dunia la FIFA 2026. Mechi hii itapigwaUwanja wa Gillette, Boston tarehe 19 June 2026 saa 12 jioni nchini Marekani sawa na saa 7 usiku 20 June 2026. Baada ya kuonyesha kiwango bora wakiizuia Brazil kwenye mchezo wa kwanza, Morocco wataweza kuvuna ushindi.? Achraf Hakimi na Ayyoub Bouaddi wa Morocco, watavaana uso kwa uso na Scott McTominay na Andy Robertson wa Scotland.

Updated: Scotland vs Morocco, team news, lineups, kick-off time, H2H na odds kabla ya mchezo wa Kundi B Kombe la Dunia 2026.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.

Taarifa muhimu za mechi Scotland vs Morocco

KipengeleMaelezo
MchezoScotland dhidi ya Morocco
MashindanoFainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026
KundiKundi C
Tarehe ya Mechi19 Juni 2026 (kwa saa za Marekani) / 20 Juni 2026 (kwa saa za Afrika Mashariki)
Eneo la MchezoBoston, Massachusetts, Marekani
Uwanja UtakaotumikaGillette Stadium
Jina Maarufu la UwanjaBoston Stadium
Muda wa Afrika Mashariki (EAT)Saa 7:00 usiku
Muda wa Boston (ET)Saa 12:00 jioni kwa muda wa wenyeji
Yatakayopatikana Kwenye MakalaUchambuzi wa mechi na utabiri wa matokeo, taarifa za hivi karibuni za timu, vikosi vinavyotarajiwa kuanza, rekodi za mikutano ya awali (H2H), matokeo mubashara (live score) pamoja na viwango vya ubashiri (odds) vya ushindi.
Jukwaa la UbashiriSportPesa

Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani ya SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026

Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mecchi za Kombe la Dunia 2026. Kwa mechi ya Scotland vs Morocco, angalia odds kwa kubonyeza picha hii chini, fanya uchambuzi wako, kisha weka mkeka wako kupitia SportPesa. Beti kistaarabu.

Scotland vs Morocco
Scotland vs Morocco

Muhtasari wa Utabiri na uchambuzi wa mechi ya Scotland vs Morocco

Kikosi cha Scotland (-)
Kikosi cha Scotland

Mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili katika mbio za kufuzu hatua ya mtoano kutoka Kundi C. Baada ya matokeo mazuri katika michezo yao ya ufunguzi, Scotland na Morocco zinafahamu kuwa makosa madogo yanaweza kugharimu ndoto zao za kusonga mbele. Scotland ilianza kampeni yake kwa ushindi mwembamba wa mabao 1-0, dhidi ya Haiti, huku Morocco ikitoa sare ya kishujaa ya 1-1 dhidi ya Brazil.

Kocha wa Scotland, Steve Clarke atategemea uzoefu wa nahodha, Andy Robertson pamoja na nguvu za kiungo Scott McTominay kudhibiti mchezo katikati ya uwanja. Kwa upande mwingine, Morocco chini ya kocha Mohamed Ouahbi imeonyesha uimara mkubwa wa kiulinzi. Baada ya kuizuia Brazil, Morocco wataingia kusaka ushindi.

Kujua ratiba ya mechi zote 104 za Kombe la Dunia 2026, soma hii pia: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Scotland vs Morocco H2H

Timu hizi zimekutana mara moja tu, na hii ilikuwa Machi 1998, ambapo Morocco walishinda mabao 3-0. Miaka 28 baadae Chochote kinaweza kutokewa watakapokutana. Fomu ya sasa, ubora wa vikosi na nidhamu ya mbinu, vitaamua matokeo.

Table hii inachambua kwa urahisi fomu ya Scotland vs Morocco

Fomu ya Scotland kabla ya mechi

MchezoMashindanoMatokeoTathmini Fupi
Haiti vs ScotlandKombe la Dunia la FIFA 2026Ushindi 1-0Scotland ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa ushindi muhimu, ikionyesha nidhamu na uwezo wa kulinda matokeo hadi mwisho.
Bolivia vs ScotlandMechi ya Kirafiki ya KimataifaUshindi 4-0Kikosi cha Steve Clarke kilitoa onyesho la kuvutia kwa kutumia vyema nafasi za kufunga na kuonyesha makali ya ushambuliaji.
Scotland vs CuracaoMechi ya Kirafiki ya KimataifaUshindi 4-1Ushindi huu ulidhihirisha ubora wa safu ya mbele ya Scotland, iliyokuwa na kasi na ubunifu mkubwa.
Ivory Coast vs ScotlandMechi ya Kirafiki ya KimataifaKipigo cha 1-0Licha ya kupambana kwa juhudi, Scotland ilishindwa kupata jibu dhidi ya uimara wa wapinzani wao.
Scotland vs JapanMechi ya Kirafiki ya KimataifaKipigo cha 1-0Waskoti walikosa ufanisi katika eneo la mwisho, jambo lililowagharimu katika mchezo uliokuwa wa ushindani mkubwa.

Morocco kabla ya mechi

MchezoMashindanoMatokeoTathmini Fupi
Brazil vs MoroccoKombe la Dunia la FIFA 2026Sare 1-1Morocco ilionesha uimara mkubwa wa kiulinzi na kuzuia mabingwa hao wa Amerika Kusini kupata ushindi.
Morocco vs NorwayMechi ya Kirafiki ya KimataifaSare 1-1Pambano la ushindani mkubwa ambapo Morocco ilionyesha uthabiti lakini ikashindwa kupata ushindi mwishoni.
Morocco vs MadagascarMechi ya Kirafiki ya KimataifaUshindi 4-0Ushindi wa kishindo uliodhihirisha ubora wa mashambulizi ya Atlas Lions.
Morocco vs BurundiMechi ya Kirafiki ya KimataifaUshindi 5-0Morocco ilitawala mchezo kwa kiwango kikubwa na kufunga mabao mengi bila kupingwa.
Morocco vs ParaguayMechi ya Kirafiki ya KimataifaUshindi 2-1Ushindi wa ushindani mkubwa ulioonyesha uwezo wa Morocco kushinda mechi ngumu.

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza

Hii hapa listi ya vikosi vinavyotarajiwa kuanza kulingana na fomu ya wachezaji, taarifa za awali za timu na mwenendo wa mechi zilizopita. Vikosi rasmi vitathibitishwa karibu na muda wa mchezo.

Scotland

Scotland vs Morocco
Kikosi cha Scotland
NafasiWachezaji Wanaotarajiwa Kuanza
KipaAngus Gunn
WalinziNathan Patterson, John Souttar, Grant Hanley, Andy Robertson
ViungoJohn McGinn, Scott McTominay, Lewis Ferguson, Ryan Christie, Ben Gannon-Doak
MshambuliajiChé Adams

Morocco

NafasiWachezaji Wanaotarajiwa Kuanza
KipaYassine Bounou
WalinziAchraf Hakimi, Chadi Riad, Issa Diop, Noussair Mazraoui
ViungoSofyan Amrabat, Azzedine Ounahi, Ismael Saibari
WashambuliajiBrahim Díaz, Ayoub El Kaabi, Soufiane Rahimi

Kufahamu mabadiliko ya sheria za Kombe la Dunia 2026, soma hii: Sheria mpya za mechi Kombe la Dunia 2026 zashtua! Nini kimebadilishwa?

Habari za timu na majeruhi

Kwa Scotland kikosi chao kina hali nzuri na hakuna majeruhi makubwa, ya kumtia wasiwasi baada ya ushindi dhidi ya Haiti. Morocco ina changamoto kubwa zaidi ya urejeshaji wa nguvu, baada ya mechi ngumu dhidi ya Brazil. Kiungo, Sofyan Amrabat anafuatiliwa kwa karibu na madaktari kutokana na maumivu madogo aliyoyapata.

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator

Scotland vs Morocco utabiri Kombe la Dunia 2026 (Utabiri wetu: Scotland 0-2 Morocco)

Ayyoub Bouaddi
Ayyoub Bouaddi

Kwa mujibu wa Opta na uchambuzi wa kitaalam kutoka mashirika mbalimbali, inatabiriwa matokeo yatakuwa ya ushindi wa mabao 2-0 kwa Morocco. Kutokana na umuhimu wa mchezo tunatarajia mchezo mgumu sana. Zingatia, huu ni mtazamo wa kiuhariri, si matokeo halisi hivyo Bashiri kistaarabu.

Kufahamu utabiri na uchambuzi wa mechi inayofuata ya Brazili, soma hii: Brazil vs Haiti FIFA Kombe la Dunia 2026: Team news, prediction, h2h

Wachezaji bora

Scotland

MchezajiNafasiMchango Wake kwa Scotland
Andrew RobertsonBekiNahodha wa Scotland na beki wa kushoto wa Liverpool FC. Anajulikana kwa uongozi wake wa kiwango cha juu na uwezo wa kupiga krosi sahihi. Pambano lake la moja kwa moja dhidi ya Achraf Hakimi linatarajiwa kuamua kasi na mwelekeo wa mchezo pembeni.
Scott McTominayKiungoKiungo wa Napoli anayefanya kazi kama injini kuu ya Scotland. Ni mchezaji wa box-to-box mwenye nguvu, anayechangia mabao na kudhibiti mabadiliko ya mchezo kutoka ulinzi kwenda mashambulizi.
John McGinnKiungoNyota wa Aston Villa aliyefunga bao muhimu dhidi ya Haiti. Ni mhimili wa mashambulizi ya kushtukiza na huleta nguvu, kasi na ubunifu katika eneo la kiungo.
Ché AdamsMshambuliajiMshambuliaji wa Torino FC anayetoa nguvu ya kimwili na uwezo wa kushikilia mpira mbele. Anasaidia kuvunja uimara wa safu ya ulinzi ya Morocco kupitia hold-up play na harakati zake za mbele ya lango.

Morocco

MchezajiNafasiMchango Wake kwa Morocco
Achraf HakimiBekiBeki wa kulia wa PSG anayechukuliwa kuwa miongoni mwa bora duniani katika nafasi yake. Uzoefu wake wa karibu mechi 100 za kimataifa pamoja na uwezo wake wa kupanda kushambulia na kufanya overlapping humfanya kuwa silaha muhimu ya Morocco upande wa kulia.
Brahim DíazMshambuliaji / Kiungo mshambuliajiKiungo mshambuliaji wa Real Madrid mwenye ubunifu wa hali ya juu, uwezo wa kiufundi na hatari kubwa mbele ya lango. Anatoa suluhisho la ubunifu katika maeneo ya kati ya uwanja.
Sofyan AmrabatKiungoKiungo wa Real Betis anayefanya kazi kubwa ya kuzuia mashambulizi. Ndiye mhimili wa timu katika kukata mashambulizi ya wapinzani na kudhibiti kasi ya mchezo.
Ismael SaibariKiungoNyota wa PSV Eindhoven aliye katika kiwango bora cha fomu. Alifanikiwa kufunga bao muhimu la kusawazisha dhidi ya Brazil katika mchezo wa ufunguzi wa kundi.
Yassine BounouKipaMlinda mlango wa Al-Hilal mwenye uzoefu mkubwa wa kimataifa. Akiwa na zaidi ya mechi 90 za taifa, anatoa uongozi na uhakika mkubwa langoni.

Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unaipa nafasi kubwa Morocco kuibuka na ushindi dhidi ya Scotland. Hautakuwa mchezo rahisi, kwani timu zote zinahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu mtoano. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Scotland vs Moroccokwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.

Scotland vs Morocco live score na matokeo

John McGinn
John McGinn

Scotland vs Morocco live score na matokeo ya mwisho yataongezwa hapa baada ya mchezo kuanza, na baada ya dakika 90. Fuatilia SportPesa Blog kwa magoli, highlights, mchezaji bora, matokeo ya mwisho na msimamo wa Kundi A baada ya mechi.

Maswali muhimu yanayoulizwa kuhusu mchezo huu

Mechi ya Scotland vs Morocco itachezwa lini?

Mechi hii itapigwa Tarehe 20 June 2026 saa saba usiku kwa saa za Afrika Mashariki, ambayo ni 19 June 2026 saa 12 jioni kwa saa za Marekani.

Scotland vs Morocco ni kundi gani?

Huu ni mchezo wa Kundi C kwenye Kombe la Dunia 2026.

Scotland vs Morocco zimewahi kukutana?

Historia inaeleza timu hizi zimekutana mara moja tu, mwaka 1998 ambapo Morocco walishinda 3-0.

Utabiri wa Scotland vs Morocco ni upi?

Utabiri wetu wa kiuhariri ni Scotland 0-2 Morocco

Scotland vs Morocco itachezwa uwanja gani?

Mechi hii itachezwa Uwanja wa Gillette, Boston

Jinsi ya kuangalia (How to watch) Scotland vs Morocco

Mashabiki wanaweza kufuatilia Scotland vs Moroccokupitia watangazaji rasmi wa FIFA World Cup 2026 katika nchi zao. Kwa Tanzania, angalia ratiba ya matangazo ya washirika rasmi wa FIFA, na fuatilia SportPesa Blog kwa live score, matokeo, highlights na taarifa za mchezo.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.