SEVILLA vs ROMA-Ni Fainali ya Europa ya kimbinu
Leo usiku kuanzia majira ya Saa 3, kwenye dimba la Puskas Arena Jijini Budapest nchini Romania, itapigwa fainali ya michuano ya Europa ikizikutanisha Sevilla ya Hispania na AS Roma ya Italia ambapo bingwa wa kwanza wa michuano ya Ulaya atapatikana katika mchezo huo.
Mwaka mmoja uliopita bingwa alikuwa ku kuanzia majira ya Saa 3, kwenye dimba la Puskas Arena Jijini Budapest nchini Romania, itapigwa fainali ya michuano ya Europa ikizikutanisha Sevilla ya Hispania na Roma FC ya Italia ambapo bingwa wa kwanza wa michuano ya Ulaya atapatikana katika mchezo huo.ni Eintratcht Frankfurt walioshinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya Rangers ya Scotland.
Sevilla inaonekana kupewa nafasi kubwa dhidi ya AS Roma kutokana na kuwa na rekodi nzuri ya ya kutwaa taji la michuano hiyo mara nyingi Zaidi (6) lakini kikwazo kikubwa ni Kocha Jose Mourinho ambaye amekuwa na wakati mzuri pindi anapotinga hatua ya fainali.
Katika michuano hiyo, Sevilla wanajivunia kutwaa tajio hilo misimu mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2014, 2015 na 2016 ikiwa inanolewa na Unai Emery lakini Jose Mourinho ni kiboko kwani ametwaa mataji matano ya michuano mikubwa ya Klabu barani Ulaya.
Wakati Los Rojiblancos wakiwa ndio wanaonekana wanaimudu michuano hii, upande wa Giallorossi wanaye bosi wao Jose Mourinho ambaye atakuwa anawania rekodi ya kushinda taji la tatu la Europa akiwa na klabu tatu tofauti, baada ya kufanya hivyo na FC Porto na Manchester United.
Mourinho raia wa Ureno pia ni mshindi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya alipokuwa anaifundisha FC Porto ya Ureno na Inter Milan ya Italia na msimu uliopita alifanikiwa kutwaa Uefa Conference League akiwa na Roma FC.
Ingawa katika michuano ya Europa, AS Roma imekuwa na uhaba wa mabao ya kufunga ambapo ina wastani wa kupata mabao chini ya 2.5 ikiwemo suluhu dhidi ya Bayer 04 Leverkusen iliyowapa tiketi ya kucheza fainali.
Mourinho ambaye hafurahishi wengi kwa mfumo wake wa kujilinda kwa muda mrefu, ameiongoza AS Roma kushindwa kufunga bao lolote kwenye mechi nne za mtoano za ugenini ingawa kazi kubwa iliyotukuka waliifanya katika dimba lao la Olimpico ambapo walishinda mechi zote tano ukiwemo wa nusu fainali dhidi ya Feyernoord uliochezwa hadi dakika za ziada.
Sasa AS Roma wanakwenda kucheza katika dimba lisilo na mwenyeji watakuwa mashakani watakapokutana na Sevilla walio katika kiwango bora kwa hivi karibuni kwani katika michezo 12 ya mwisho waliyocheza Sevilla wamepoteza mara mbili tu huku wakishinda mingine na sare iliyosalia.
Katika safari yao kuelekea fainali hii, Sevilla waliitupa nje Juventus baada ya dakika za nyongeza tena wakiwa na wachezaji kumi uwanjani na sasa wapo hapo wakiwania taji la 7 la michuano hiyo.
Rekodi zinaonyesha kwamba Klabu hizi zimekutana mara tatu kwenye historia mara nne na Sevilla imeshinda mara tatu na sare mara moja.
Kabla ya mchezo huo,Sevilla ilikutana na Real Madrid na ikapoteza bao 2-1 katika La Liga wakati AS Roma ilinyukwa bao 2-1 na Fiorentina katika Serie A.
Nyota wa kuchungwa wa Sevilla ni Youssef En Nesyri ambaye amefunga bao 8 na Rafa Mir aliyepachika bao 6 pamoja na Erik Lamela mwenye bao 5 vilevile Lucas Ocampos amefunga bao 4.
Wanao nyota kama Ivan Rakitik mwenye pasi tatu za mabao,Gonzalo Montiel (3),Marcus Acuna na Suso wenye pasi mbili za pasi za mabao.
Upande wa AS Roma kinara wa kupachika mabao ni Paulo Dyabala ambaye amefunga 11 akifuatiwa na Tammy Abraham mwenye mabao 8 na Stephane El Shaarawy mwenye bao 7.
Nyota wengine ni Lollenzo Pellegrini mwenye pasi za bao 4, Leonardo Spinazzola mwenye pasi za mabao 4.
Zipo taarifa za nyota watakaokosekana katika mchezo huo kwa upande wa Sevilla itawakosa Marcao, Tanguy Nianzou, Erik Lamela na Marcus Acuna wanaotumikia adhabu ya kadi, Pape Gueye na Tecatito ambao ni majeraha.
Kwa AS Roma itawakosa Nemanja Matic, Rui Patricio, Marash Kumbulla na Ricky Karsdop ambao wote ni majeruhi.tulivyoeleza kwenye utangulizi mwanzoni kabisa. Mechii inapigwa leo usiku na ipo kwenye tovuti yetu. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga z*150*87#