skip to Main Content
BARNSLEY Vs SHEFFIELD WEDNESDAY- Ni Dabi Ya Play Offs Wembley
Barnsley

BARNSLEY vs SHEFFIELD WEDNESDAY- Ni Dabi Ya Play Offs Wembley

Patashika ya mchezo wa fainali ya Play Offs ya timu za League One, itafikia tamati usiku wa leo, ambapo timu ya Barnsley watakabiliana na Sheffield Wednesday, katika uwanja wa Wembley jijini London.

Mchezo huu wa fainali ya Paly offs ni mmoja wa michezo unaoingia katika kihistoria ukiwa ni mchezo unaozihusisha timu mbili Jirani ambazo zote zinapatikana katika kitongoji cha Yorkshire Kusini.

Kwa nini unaitwa mchezo wa kihistoria? Hii ni kwa sababu, mara ya mwisho kwa timu Jirani kucheza mechi ya fainali ya Play offs ilikuwa Mwaka 2020 ambapo Fulham walipepetana na Brentford katika uwanja huu huu wa Wembley.

lakini tofauti na mchezo wa leo, mchezo wao haukuwa na mashabiki ndani ya uwanja, hii ni kutokana na janga la ugonjwa wa Covid 19, ambalo lilipelekea matukio mengi ya kimichezo kuahirishwa au mashabiki kutoruhusiwa, ikiwemo mechi hiyo kuchezwa bila mashabiki au watazamaji.

Barnsley wataingia katika mchezo huu wakiwa ni timu isiyopewa nafasi kubwa ingawa wameichapa Sheffield Wednesday mara mbili msimu huu, lakini pia wameshinda mechi 3 za mwisho dhidi ya The Owls.

Klabu ya Barnsley watateremka dimbani wakiwa na motisha ya ushindi walioupata kwa kuwatandika Sheffield bao 4-2 huko Oakwel miezi miwili iliyopita.

Sheffield Wednesday wanatarajiwa kuchagizwa na uwepo wa mashabiki zaidi ya 35,000 katika dimba la Wembley.

Vijana wa Michael Duff, Barnsley walifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya mtoano ya League One baada ya kuicharaza Bolton Wanderers kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali. Barnsley walitoka sare ya 1-1, katika mechi ya kwanza wakiwa ugenini na kisha wakashinda goli moja bila wakiwa nyumbani wiki moja iliyopita.

Msimu uliopita Barnsley walimaliza mkiani mwa Ligi ya Championship na kushushwa daraja. The Tykes hivi sasa wanayo nafasi ya kurejea kwenye Ligi ya daraja la pili la England kama watapata ushindi katika mechi ya leo.

Upande wa Sheffield Wednesday waliushangaza ulimwengu wa soka kwa kuwa klabu ya kwanza kupindua kupigo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Darren Moore kilipata bao dakika ya 99 na kulazimisha mchezo kwenda dakika za nyongeza dhidi ya Peterborough iliyokuwa inaongoza bao 4-0.

 

Wachezaji wa Sheffield Wednesday.The Owls ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 na sasa wanayo nafasi ya kurejea katika Ligi ya Championship baada ya kuporomoka mwaka 2021.

Kwa mara ya mwisho Sheffield Wednesday kucheza katika dimba la Wembley ni miaka 7 iliyopita ambapo walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Hull City.

Sheffield Wednesday wamefunga wastani wa bao 2.5 katika mechi 7 kati ya 8 za mwisho walizocheza katika League One lakini The Owls wameshinda mechi 5 kati ya 6 za mwisho katika Ligi hiyo.

Upande wa Barnsley wamefunga mabao chini ya 2.5 katika mechi tatu za mwisho walizocheza katika League one.

Wachezaji wa kuchungwa zaidi upande wa Barnsley ni Devance Cole aliyefunga bao 15, James Norwood mwenye bao 11, Adam Phillips kapachika bao 9, Nicky Garden mwenye bao 6 na Jordan Williams amefunga mabao 5.

Upande wa Sheffield nyota wa kuwachunga ni Michael Smith aliyecheka na nyavu mara 1, Lee Gregory kafunga bao Lee Gregory aliyefunga bao 11, Josh Windass naye amefunga bao 11, Barry Bannan aliyefunga magoli 11.

Katika mechi 6 za mwisho wababe hawa kukutana Barnsley imeshinda mara 4, Sheffield Wednesday imeshinda mara moja na sare moja.

Pamoja na takwimu hizi ambazo tumeziainisha hapo juu, ushindi kwa moja wapo kati ya timu hizi utategemea zaidi mbinu, maarifa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja ambao ndio itakuwa silaha ya ushindi.

Kubwa kuliko zote mchezo huu unakuja na presha ya ushindi na mategemeo ya kufuzu. Hayo yote yanachagiza kuifanya mechi hii kuwa ya kipekee kwa sababu timu hizi zinatoka eneo moja kwa hiyo upinzani upo kuanzia kwenye ngazi ya mtaa mpaka uwanjani.

SportPesa imekuwekea mechi hii. Kubashiri tembelea Sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

 

 

 

Share this:
Back To Top