Patashika ya Ligi Kuu ya England inaendelea leo hii, ikiwa inajulikana zaidi kama mechi za ligi ya EPL za lala salama, kwa mchezo mkali unaobeba maamuzi mazito ya timu mbili ambazo ni Newcastle United na Leicester City.
Timu hizi zitaumana kuanzia majira ya saa nne usiku, katika dimba la St James Park huku kila mmoja akiwa na lengo lake la namna ya kuumaliza msimu.
Upande wa wenyeji, The Magpies wao wanawania alama moja tu itakayowahakikishia kumaliza ndani ya nne bora ambapo watakuwa na tiketi ya moja kwa moja ya kucheza michuano ya Klabu bingwa Ulaya msimu ujao.
Malengo ya Newcastle ni tofauti kabisa na Leicester City ambao wanataka kuendelea kufukuza upepo hadi dakika ya mwisho ili kufahamu nafasi yao ya kusalia Ligi Kuu na iwapo watapoteana basi wanaweza kushuka daraja.
Newcastle United wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama 69 kibindoni na wanahitaji sare ya aina yoyote ili wafikishe alama 70 ambazo hazitofikiwa na Liverpool ambayo ndiyo iliyokuwa inazipa shinikizo The Magpies na Manchester United.
Liverpool ilishikiliwa na Aston Villa kwa kutoka sare ya bao moja jambo ambalo limewafanya wafikishe alama 66 na wamebaki na mchezo mmoja ambao hata kama watashinda watafikisha alama 69 ambazo wanazo Newcastle United na Manchester United zenye michezo miwili kibindoni.
Tafsiri yake ni kwamba Newcastle watautolea macho mchezo wao dhidi ya Leicester City ili wakamilishe biashara yao mapema na kujitambulisha rasmi kwenye ulimwengu wa soka la Ulaya baada ya uwekezaji uliofanyika na Mohammed Bin Salman kutoka Saud Arabia mwaka 2021.
Wakati stori ikiwa nzuri kwa Newcastle,upande wa pili wa Leicester waliopo kwenye nafasi ya 19 wakiwa na alama 30,wao ni kama wamepoteza dira tangu aliyekuwa tajiri wa timu hiyo Vichai Srivaddhanaprapha afariki dunia mwaka 2018.
Katika misimu miwili iliyopita hawajawa na timu shindani ingawa inao wachezaji waliotikisa kama James Maddison,Jammie Vardy ambaye umri unamtupa mkono,Youri TielemansPatson Daka,Kelechi Iheanacho,ni kama wamepoteza morali ya kupambana uwanjani.
Leicester City imeshinda mechi 8 tu kati ya 36 walizochezawametoka sare 6,wamepoteza mechi 2 2 wamefunga bao 49 na wameruhusu bao 67 ,hizo ni takwimu ambazo haziridhishi ,Kocha Dean Smith ana kazi kubwa ya kufanya kuinusuru timu hiyo ambayo kwa kusuasua kwao wakalazimika kumtimua kazi Brendan Rodgers lakini haionyeshi kufufuka.
Iwapo watashinda mchezo dhidi ya Newcastle United The Foxes watafikisha alama 33 na watachupa hadi nafasi ya 17 ambayo wapo Everton ambao wikiendi hii walitoka sare ya bao moja dhidi ya Wolves.
Vilevile juu ya Leicester City wapo Leeds United wenye alama 31,na waowana michezo miwili hivyo vita ya kujinusuru kuporomoka daraja.
Kocha wa Newcastle,Eddie Howe mwenye umri wa miaka 45 amesema mechi ya kesho ni muhimu zaidi na iwapo watafuzu UCL atachukua muda wa kupumzika kwa kazi kubwa ambayo watakuwa wameikamilisha.
Kuelekea mchezo huo nyota wa kuchungwa au kutazamwa zaidi upande wa Newcastle United ni mshambuliaji wao kinara Callum Willson ambaye yupo katika kilele cha ubora wake akiwa na bao 18na ndiye aliyepiga mashuti mengi(45), Alexander Isak mwenye bao 10 na amepiga mashuti 23, Miguel Almiron mwenye bao 11 na amepiga mashuti 19.
Upande wa Leicester City kinara wa kucheka na nyavu ni Harve Barners amefunga bao 12 na amepiga mashuti yaliyolenga lango 32,James Maddison mwenye mabao 10 na amepiga mashuti yaliyolenga lango 29.
Katika michezo mitano ya mwisho katika EPL, Newcastle United imepoteza mara moja na sare moja huku wakishinda mitatu,wakati Leicester City wao wameshinda mechi moja pekee kati ya mitano ya mwisho ya EPL, wakitoka sare miwili na kupoteza miwili.
Rekodi inaonyesha tangu msimu wa 2021/22 timu hizi zimekutana mara 5 katika Ligi Kuu ya England. Leicester City imeshinda mara 2, wakati Newcastle United imeshinda mara 3 na katika mchezo wa mwisho The Magpies waliitandika bila huruma The Foxes bao 3-0 .
Tabiri mchezo huu kupitia Sportpesa kwani odds zake ni nono na unaweza kujivunia ushindi mwingi, kazi kwako kuweka dau uli upate ushindi wa kutosha.
Kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

