skip to Main Content
LIGI KUU NBC 2022/23- Umekuwa Msimu Bora Sana Kwa Yanga.
Yanga-bingwa

LIGI KUU NBC 2022/23- Umekuwa msimu bora sana kwa Yanga.

Ligi Kuu Tanzania bara ilikuwa iendelee kesho Jumatano kwa michezo kadhaa kupigwa ikiwa ni mzunguko wa 28, katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya NBC Tanzania, lakini mechi hizo zimeahirishwa ili ziweze kuchezwa zote kwa pamoja.

Yanga ambayo ilikuwa icheze na Mbeya City, mkoani Mbeya wamepewa nafasi ya kujiandaa kwa ajili ya mechi ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Africa, ambapo timu hiyo ya Jangwani inatarajiwa kucheza na timu ya USM alger ya Algeria siku ya Jumapili Tarehe 28, jijini Dar-Es-Salaam.

Tukirudi katika ligi ya NBC, tayari bingwa ameshapatikana ambaye ni Yanga, lakini bado kuna timu zinahitaji kumaliza vyema msimu wakati vita kubwa imesalia kwa timu zinazopigana kujinusuru na kushuka daraja.

Kwa Klabu zilizopo kuanzia nafasi ya 7 ambayo ni Kagera Sugar yenye alama 35 ipo salama ,lakini timu iliyopo kuanzia nafasi ya 8 ambayo ni Tanzania Prisons yenye alama 34 bado haijajihakikishia kukwepa kabisa hekaheka zinazoendelea na timu nyingi ya kusalia Ligi Kuu msimu huu uliopo ukingoni.

Baada ya michezo ya Jumatano hii, kila timu itakuwa imesalia na mchezo mmoja, hivyo ni mechi muhimu kwa kila timu ambayo bado haipo salama na watatakiwa wapate matokeo mazuri ili kujinusuru na kushuka daraja au kucheza mtoano.

Katika dimba la Azam Complex Jijini Dar es salaam, Azam Fc ambao wametoka kupoteza dhidi ya Namungo watawaalika Coastal Union ya Tanga.

Azam waliopo nafasi ya 3 wakiwa na alam 53 wanataka alama 3 ili waendelee kuwakimbia Singida Big Stars walipo nafasi ya 4 wakiwa na alama 51, wakati Coastal Union ambao katika mchezo uliopita waliwanyuka Ihefu bao 1-0, wanahitaji alama 3, ili wafikishe alama 36, zitakazowahakikishia kutokushuka daraja.

Mwenendo wa Coastal Union umekuwa wa kuvutia hivi karibuni kwani katika michezo mitano ya mwisho wameshinda mitatu na sare miwili,wakati Azam wameshinda mitatu na kupoteza miwili.

Coastal Union wanakamata nafasi ya 10 hivi sasa na wakishinda watasogea juu ikitegemea na matokeo ya timu nyingine kwa siku hiyo.

Ihefu vs PolisiPatashika nyingine itashuhudiwa kwenye mashamba ya Mbarali ambapo Ihefu ambayo imepoteza kiwango kwa hivi karibuni watawakaribisha Geita Gold ambayo nayo haijawa na matokeo mazuri.

Ihefu ipo nafasi ya 9 wana alama 33, iwapo watashinda watafikisha alama 36 ambazo zitawaondoa kabisa kwenye hekaheka za kushuka daraja,lakini Geita wao wapo salama katika nafasi yao ya 6 na alama zao 37 ingawa ushindi kwao utaongeza thamani yao na kuwashusha Namungo ambao wana alama 39 na itategemea matokeo ya mchezo wao.

Huko Jamhuri Mkoani Morogoro ndugu wawili wataonyeshana kazi ambapo Mtibwa Sugar watawakaribisha Kagera Sugar.

Mtibwa wanashikilia nafasi ya 14 wakiwa na alama 29, wanazihitaji zaidi alama 3 ili wafikishe alama 32 ambazo pia zitategemea zaidi mechi yao ya mwisho ili wajue nafasi watakayokuwa .

Kagera Sugar wao wapo kwenye nafasi nzuri kwani alama moja pekee itawaondolea kabisa bugdha ya kucheza mtoano kwani wao hivi sasa wana alama 35 kibindoni.

wachezaji wa Azam wakijiandaa na moja ya mechi ya ligi kuuKwa Mkapa kutakuwa na shughuli pevu kwa maafande wa Polisi Tanzania ambao waliweka hai matarajio yao ya kusalia Ligi Kuu baada ya kuwatandika Mtibwa katika mchezo uliopita.

Swali kwa vijana wa Kocha Mwinyi Zahera wataweza kuwazuia Simba ambao wamepoteza mchezo mmoja tu katika Ligi Kuu?Simba ambayo inahitaji kuwafariji mashabiki wao baada ya kutoka patupu msimu huu?

Polisi Tanzania ipo nafasi ya 19, wana alama 25, wanapambana washinde mechi zao zote ili wafikishe alama 30 huku wakisubiria je Mbeya City yenye alama 27, KMC na Mtibwa Sugar zenye alama 29 watamalizaje michezo yao?

Kifupi ni kwamba maisha ya Polisi Tanzania yanategemea zaidi matokeo yao lakini pia matokeo ya Mtibwa Sugar, KMC na Mbeya City.

Shughuli nyingine pevu itakuwa katika dimba la Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya kati ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 8 wakiwa na alama 34 watakipiga dhidi ya KMC iliyo kwenye nafasi ya 13 wakiwa na alama 29.

Iwapo Mbeya City watashinda watafikisha alama 37 na kujiondoa kabisa kwenye mstari wa kushuka daraja,wakati watawaacha KMC wakipiga hesabu za vidole,lakini iwapo KMC watashinda watawaachia majanga Polisi Tanzania,Mbeya City na Mtibwa kupambana kutokushuka daraja moja kwa moja.

Namungo nao watakuwa wenyeji wa Dodoma Jiji katika dimba la Majaliwa mkoani Lindi na vijana wa Kocha Denis Kitambi wapo katika ubora wao kwa kuwasimamisha Simba kabla ya kuwacharaza Azam bao 2-1 .

Ushindi kwa Namungo yenye alama 39 katika nafasi yao ya 5 hakutobadilisha sana mwenendo wao bali utawaimarisha zaidi katika namna ya kuumaliza msimu kwani hawatoweza kuifikia Singida Big Stars iliyo na alama zao 51 ambao walima Alizeth  wao watacheza dhidi ya Ruvu Shooting ambayo imeshuka daraja.

Kwa timu zote zenye alama kuanzia 31 hazitoshuka daraja moja kwa moja kwakuwa Polisi Tanzania ina uwezo wa kusifikisha alama 30 hata ikishinda mechi zake zote zilizobakia,hivyo zilizosalia ni zile ambazo zinapambana kutokucheza mtoano.

Ikumbukwe ni timu mbili pekee zinashuka daraja ambapo tayari Ruvu Shooting imeshatangulia,lakini timu zitakazomaliza kwenye nafasi ya 16 na 17 zitacheza mtoano.

Yote kwa yote kwa namna ambavyo msimu huu umekwenda naweza kusema umekuwa msimu bora zaidi kwa Yanga na pia usiotabirika. Nafahamu timu ya Yanga imeshachukua ubingwa, lakini kila mmoja wetu anakumbuka namna unbeaten ya Yanga ilivyoshangaza wengi kule Ihefu.

Wengine wanakumbuka namna Simba alivyopata shinda kwa Azam katika mechi zake zote walizokutana msimu huu. Kubwa kabisa ni namna baadhi ya timu kama Singida Big stars ilivyokuja msimu huu na usajili wa wa Brazil na Mu Argentina.

Timu ya Geita Gold yenyewe ilisajili Mjapan ambaye hakupata nafasi sana ya kucheza, lakini ilikuwa ni sehemu moja wapo ya usajili ulioongeza ubora na ushindani.

Tunatumai baada ya mechi za kesho na mechi za raundi ya mwisho, timu zilizobakia zitajitahidi kurudi vizuri msimu ujao na kuendeleza ubora na ushindani ambao umeonekana msimu huu.

Tembelea tovuti yetu sportpesa.co.tz au piga *150*87# kubashiri mechi hizi.

 

Share this:
Back To Top