- Kinawaka leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Metropolitano, ambapo kutapigwa mechi kubwa ya Ligi Kuu Hispania La Liga.
- Ni Atletico Madrid vs Barcelona, mchezo ambao unakwenda kutoa taswira ya vita ya ubingwa.
- Barcelona wapo kwenye nafasi ya 1, huku Atletico Madrid wakiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo, huku timu hizi zikitarajiwa kuvaana mara 3 ndani ya siku 10 tu, katika mashindano ya ligi na UEFA.
Leo Jumamosi usiku kwenye Uwanja wa Metropolitano kutapigwa mechi kubwa ya Ligi Kuu Hispania La Liga. Ni Atletico Madrid vs Barcelona, mchezo ambao unakwenda kutoa taswira ya vita ya ubingwa. Barcelona wapo kwenye nafasi ya 1, huku Atletico Madrid wakiwa nafasi ya 4 kwenye msimamo. Timu hizi zinatarajiwa kuvaana mara 3 ndani ya siku 10 tu, katika mashindano ya ligi na UEFA.
SOMA HII PIA: Atletico Madrid vs Barcelona – A Battle for Supremacy in La Liga
Je, bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Atletico Madrid Vs Barcelona H2H

Timu hizi zimekutana mara 251 katika historia yao, ambapo Barcelona wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 114. Atletico Madrid wao wameshinda mechi 80, huku mechi 57 zikimalizika kwa matokeo ya sare. Mara ya mwisho kukutana ubao wa matokeo ulionyesha, Barcelona 3-0 Atletico Madrid katika nusu fainali ya Copa Del Rey.
Vikosi vinavyotarajiwa
Atletico Madrid

Kipa: Musso
Walinzi: Molina, Le Normand, Hancko, Ruggeri
Viungo: Simeone, Koke, Baena, Lookman
Washambuliaji: Alvarez, Griezmann
Barcelona
Kipa: J Garcia
Walinzi: Araujo, Cubarsi, E Garcia, Cancelo
Viungo: Bernal, Pedri, Yamal, F Lopez, Rashford
Mshambuliaji: Lewandowski
Habari za timu
Atletico Madrid

Atletico Madrid watawakaribisha Barcelona Uwanja wa Metropolitano, katika mchezo wa Ligi Kuu ‘La Liga’. Atletico wanajiandaa kukutana na Barcelona mara tatu, katika mechi nne mfululizo zijazo. Hii ni kutokana na kuwa na michezo miwili ijayo ya robo fainali, ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Camp Nou wiki ijayo.
Tayari kikosi cha, Diego Simeone kipo fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad itakayopigwa tarehe 18 Aprili 2026. Atletico hawapo kwenye mbio za ubingwa wa La Liga msimu huu, ambapo wakiwa nafasi ya 4, wapo nyuma kwa alama 16 dhidi ya vinara Barcelona. Lakini pia wanaongoza kwa alama 13 dhidi ya Real Betis, waliopo nafasi ya tano. Hata hivyo, Atletico wanajua kuwa matokeo mabaya leo Jumamosi, yanaweza kuwaathiri kisaikolojia kabla ya mchezo wao wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona.
SOMA HII ZAIDI: Barcelona FC- Latest news, fixtures, results, table standings, squad players, transfer news and statistics
Barcelona
Barcelona wameshinda mechi nne kati ya tano zilizopita dhidi ya Atletico, ikiwemo ushindi wa 3-1 katika mchezo wa awali msimu huu. Barcelona pia hawajapoteza dhidi ya Atletico ugenini kwenye ligi tangu Oktoba 2021, na wanaingia kwenye mechi hii wakiwa hawajapoteza katika michezo minane mfululizo ya ligi.
Barcelona inaongoza La Liga kwa alama nne juu ya Real Madrid, ingawa pengo linaweza kupungua kabla ya mechi hii iwapo Real Madrid wataifunga Mallorca. Barcelona wamefunga mabao 78 kwenye La Liga msimu huu, na vipigo vyao vyote vinne vimetokea ugenini.
Taarifa za wachezaji wenye majeraha
Atletico Madrid

Atletico wataendelea kumkosa, Marcos Llorente na Johnny Cardoso ambao wanatumikia adhabu. Pablo Barrios (jeraha la paja). Wengine kama Jan Oblak, Marc Pubill, Rodrigo Mendoza na Alexander Sorloth wanamashaka ikiwa watacheza.
Kutokana na hali hiyo, Alex Baena anaweza kucheza nafasi ya ndani zaidi pamoja na Koke. Julian Alvarez anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji dhidi ya Barcelona, ambao inaelezwa wamepanga kumsajili majira ya kiangazi.
Barcelona

Kwa upande wa Barcelona, Raphinha ameumia misuli ya paja akiwa na Brazil, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja hadi mwezi Mei. Andreas Christensen bado yupo nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha la goti, huku Frenkie de Jong akiendelea kuuguza jeraha la misuli. De Jong anatarajiwa kurejea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wiki ijayo.
SOMA HII PIA: Top 5 Dominating Soccer Teams in 2023-2024: Who Will Reign Supreme?
Utabiri wa matokeo na hitimisho
Atletico Madrid vs Barcelona ni mchezo mgumu sana, vijana wa Simeone wamepoteza mechi zao mbili zilizopita dhidi ya Tottenham na Real Madrid. Wanakabiliwa na changamoto eneo la kiungo ambapo kuna pigo kubwa, hata hivyo wanatarajiwa kupambana vya kutosha kupata angalau sare nyumbani. Hii ni katika harakati za kuweka ari, kuelekea makutano ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya Nusu Fainali. Upo uwezekano mkubwa mchezo huu ukamalizika kwa sare

