- Matokeo ya hivi karibuni Yanga SC, wafungaji msimu huu 2025/26
- Yanga SC imeipiga Tanzania Prisons nje ndani 2025/26
- Allan Okello, Star Boy atwaa tuzo yake ya kwanza ndani ya NBC Premier League
- Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons, kituo kinachofuata ni Pamba Jiji FC
Yanga SC imeipiga Tanzania Prisons nje ndani 2025/26. Yanga SC mechi yao iliyopita ilikuwa dhidi ya wajelajela, Aprili 4, 2026, KMC Complex. Mchezo huo Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons matokeo rasmi. Mzunguko wa kwanza ilikuwa Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC, Uwanja wa Jamhuri.
SOMA HII: Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC NBC Premier League/ Highlights, goal, statics
Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC imeipiga Tanzania Prisons nje ndani, Pamba Jiji FC wanafuata

Yanga SC imeipiga Tanzania Prisons nje ndani katika mechi mbili za ligi. Mabingwa hao watetezi chini ya Kocha Mkuu, Pedro Goncalves hawajapoteza mchezo. Kituo kinachofuata ni dhidi ya Pamba Jiji FC, Aprili 8, 2026.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza Depu alifunga goli pekee la ushindi. Mchezo wa pili alikosekana kutokana na kutokuwa fiti. Ingizo hilo jipya tayari limeanza mazoezi.
Magoli ya Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons

Katika mchezo wa mzunguko wa pili goli la ufunguzi lilifungwa na Allen Okello dakika ya 50. Hili linakuwa goli lake la pili kwenye ligi. Alifungua ukurasa kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars raia huyu wa Uganda.
Kutokana na kiwango alichoonyesha Okello alitwaa tuzo ya mchezaji bora. Inakuwa tuzo yake ya kwanza kwenye ligi 2025/26. Ikumbukwe kwamba kiungo huyu alisajiliwa dirisha dogo akitokea Klabu ya Vipers.
Goli la pili lilifungwa na Mudathir Yayha ambaye ni Mtanzania dakika ya 68. Pacome Zouzoua raia wa Ivory Coast alifunga goli dakika ya 86. Magoli 3 na pointi tatu ilikuwa kwa mabingwa watezi.
SOMA HII: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Msimamo wa NBC Premier League 2025/26
Huu hapa msimamo wa NBC Premier League uliobereshwa hivi punde. Yanga SC wanaongoza ligi na pointi 41. Tanzania Prisons nafasi ya 15.
| POS | MP | W | D | L | PTS |
| Yanga SC | 17 | 12 | 5 | 0 | 41 |
| Simba SC | 16 | 10 | 5 | 1 | 35 |
| 3. Azam FC | 17 | 8 | 9 | 0 | 33 |
| 4. JKT Tanzania | 18 | 7 | 8 | 3 | 29 |
| 5.Pamba Jiji FC | 17 | 6 | 8 | 3 | 26 |
| 6.Singida Black Stars | 17 | 7 | 4 | 6 | 25 |
| 7.Dodoma Jiji FC | 18 | 6 | 6 | 6 | 24 |
| 8. TRA United | 17 | 6 | 5 | 6 | 23 |
| 9.Mtibwa Sugar | 18 | 5 | 8 | 5 | 23 |
| 10.Namungo FC | 18 | 5 | 7 | 6 | 22 |
| 11.Mashujaa FC | 18 | 4 | 8 | 6 | 20 |
| 12.Mbeya City | 17 | 4 | 4 | 9 | 16 |
| 13.Coastal Union | 18 | 3 | 7 | 8 | 16 |
| 14.Fountain Gate | 17 | 4 | 4 | 9 | 16 |
| 15.Tanzania Prisons | 18 | 3 | 4 | 11 | 13 |
| 16. KMC FC | 17 | 2 | 2 | 13 | 8 |
SOMA HII: NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili | Azam FC vs Simba SC | Yanga SC vs Prisons | Msimamo
Hitimisho
Yanga SC imeipiga Tanzania Prisons nje ndani 2025/26 katika mechi za NBC Premier League. Magoli manne na pointi sita wamevuna. Tanzania Prisons ipo katika mstari wa kushuka daraja kutokana na mwendo waliona kwenye mechi za ligi.

