Simba vs Wydad CasablancaWydadS

Siku ya kesho katika dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es salaam, kuanzia majira ya saa 10 kamili Jioni, kwa saa za Afrika Mashariki utapigwa mchezo wenye hadhi kubwa, wa hatua ya robo fainali, Ligi ya mabingwa Afrika, ambapo itashuhudia wekundu wa msimbazi Simba wakiwakaribisha mabingwa watetezi wa michuano hiyo Wydad Athletic Club kutoka nchini Morocco.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, Vijana wa Msimbazi, wamepata kibali kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF, kinachowaruhusu mchezo huo kupigwa majira ya saa 10 jioni.

“Tulipeleka maombi ya mashabiki wetu kupitia TFF, tunashukuru Mungu yamekubaliwa. Mashabiki wetu walipendekeza mechi zetu zipigwe muda wa saa kumi alasiri, tofauti na mechi tulizocheza katika hatua ya makundi ambazo tulicheza majira ya saa 1 usiku”

Ripoti nyingine kutoka Simba zinahusu wachezaji waliokuwa majeruhi ambao ni Aishi Manula ambaye amekosekana katika michezo miwili iliyopita ukiwemo ule wa Derby ya Kariakoo, anatarajiwa kuonana na daktari wa timu kuona iwapo upo uwezekano wa kurejea kikosini au atahitaji matibabu zaidi. Vile vile kiungo mkata umeme,Sadio Kanoute naye bado haijathibitishwa kama atakuwemo kikosini.

Ukweli ni kwamba iwapo Simba itakosa nyota hawa wawili ni pigo kwakuwa hakuna asiyefahamu umuhimu wa Manula ambaye ni mzoefu wa mashindano hayo. pia kiungo Kanoute ndiye aliyeunda safu bora ya kiungo akiwa na Muzamiru Yassin na kuifanya timu ya Simba kuwa imara zaidi katika eneo la kujilinda.

Licha ya kuwa na hatihati ya wawili hao bado Simba ina hazina ya wachezaji wazuri kama Beno Kakolanya na Ally Salim katika milingoti mitatu. Erasto Nyoni anaweza kucheza eneo la kati kati ya uwanja, hivyo kumpa Kocha Robertinho na benchi la ufundi sababu ya kumwamini na kuonyesha thamani yake dhidi ya Wydad Athletic Club.

Matokeo ambayo Simba imeyapata katika Dreby ya Kariakoo kwa kuichapa Yanga yamekuwa ni sehemu ya motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi kuelekea mchezo huu ingawa Afisa Habari wa mnyama,Ahmed Ally anasema wapinzani wao wa siku ya Jumamosi ni tofauti kabisa na Wananchi hivyo matokeo waliyoyavuna wiki iliyopita hayana uhusiano wowote na uimara wao kuelekea mchezo wa Klabu bingwa Afrika.

‘’Ukweli ni kwamba matokeo tuliyoyapata dhidi ya Yanga hayatoshi kutupa mwanga kwamba yanatosha kuiandaa timu kucheza mchezo war obo fainali,Wydad na Yanga ni vitu viwili tofauti ni mbingu na ardhi,Wydad wametuzidi kila kitu,na tunatamani siku moja hata sisi kuwa kama wao,lakini kwenye mchezo wa mpira wa miguu tunaweza kufanya lolote kama ambavyo tulifanya dhidi ya Zamaleki ya Misri na tutawashangaza’’Ahmed Ally alisema.

Hii ni msimu wan ne Simba wanacheza hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF na ndipo kikwazo chao kikubwa cha ndoto zao za kufika mbali zaidi huwa zinaishia .

Kwa mara ya kwanza tangu timu hii iwe chini ya Mohamed Dewji ilikuwa ni katika msimu wa 2018/19 Simba ilitupwa nje na TP Mazembe katika Ligi ya mabingwa baada ya kupokea kichap cha bao 4-1 baada ya suluhu ya katika mchezo wa mkondo wa kwanza kwa Mkapa.

Mnyama alipambana msimu wa 2020/21 na katika hatua ya robo fainali wakakwaa kisiki dhidi ya Kaizer Chiefs licha ya ushindi wa bao 3-0 kwenye mchezo wa marejeano uliopigwa hapa nchini lakini walishindwa kusonga mbele baada ya kipigo kizito cha bao 4-0 walichokipata nchini Afrika Kusini.

Msimu wa 2021/22 Simba haikufanya vizuri katika Ligi ya mabingwa na wakajikuta wakiangukia kwenye Kombe la Shirikisho ambapo kwenye hatua ya robo fainali walijikuta wakitupwa nje na wapinzani kutoka Afrika Kusini kwa mara nyingine ambao ni Orlando Pirates na mnyama akashindwa kwenye changamoto ya mikwaju ya penati.

Upande wa wapizani wao,Wydad Casablanca wao ni mabingwa mara tatu wa michuano hii waliyotwaa 1992,2017 na 2022  na wana rekodi nzuri ya ushiriki wao kwa miaka ya hivi karibuni inachagiza juu ya ubora wao kwani katika michuano ya misimu 8 iliyopita,7 kati ya hiyo walifuzu hatua kama hii wakiwa vinara kwenye makundi yao.

Mwaka jana walitwaa ubingwa kwa kuwavua ubingwa Al Ahly na wao ndio wanatetea taji lao la msimu uliopita,ni mechi ngumu lakini Simba wanayo historia ya kuwavua ubingwa Zamaleki mnamo msimu wa 2002/2003 jambo ambalo inaonyesha katika soka mipango ikiwa mizuri na ubora basi inawezekana.

Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa kwenye kiwango bora chenye muendelezo baada ya ushindi katika mechi 4 na sare 1 katika michezo mitano ya mwisho ya Ligi Kuu Tanzania bara,wapo nafasi ya 2 katika msimamo huku wapinzani wao Wydad wameshinda mechi 3 na sare 2 katika mechi 5 za mwisho katika Ligi ya Morocco na wapo nafasi ya 2 kwenye msimamo.

Safari ya Simba katika michuano hii kwa kuiondoa Nyasa Big Bullets walipoiunga nyumbani na ugenini kwa jumla ya bao 4-0 kabla ya kuicharaza Primeiro De Agosto jumla ya bao 4-1 na kutinga makundi.

Katika kundi lake lililokuwa na timu za Raja Casablanca,Vipers ya Uganda na Horoya ya Guinea,Simba ilimaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya Raja Casablanca.

Ikiwa nyumbani Simba ilishinda michezo jumla ya michezo minne huku ikipotea mmoja dhidi ya Raja Casablanca,ikifunga mabao 11 na kuruhusu mabao matatu katika mchezo mmoja dhidi ya Raja Casablanca.

Simba SC vs Wydad CasablancaIkiwa ugenini Simba ilipata ushindi kwenye michezo mitatu dhidi ya Nyasa Big Bullets,Primeiro de Agosto na Vipers lakini ikapoteza miwili dhidi ya Horoya ya Guinea na Raja Casablanca,ilifunga mabao 7 na kuruhusu mabao matano.

Upande wa Raja Casablanca walianzia safari yao dhidi ya Rivers United kwenye hatua ya mtoano raundi ya pili ambapo walishinda jumla ya bao 6-1 na hatua ya makundi walikuwa na Klabu za Petro de Luanda,As Vita ba JS Jabylie.

Wydad walimaliza vinara wa kundi hilo ambapo walishinda mechi zao zote za nyumbani huku wakifunga mabao 11 na kutoruhusu bao lakini wakiwa ugenini walipoteza mechi moja,sare moja na kushinda mechi 2 .

Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Wydad ni hatari zaidi wanapokuwa nyumbani kwao lakini wakiwa ugenini upo uwezekano wa kupoteza hivyo Simba ambayo imejijengea utamaduni wa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani upo uwezekano wa kupata matokeo kwa Mkapa wikiendi hii.

Kwa miaka ya karibuni Simba imepangwa na timu kutoka Morocco ambapo msimu uliopita ilicheza dhidi ya RS Berkane katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na ilipokuwa nyumbani ilishinda bao 1-0 lakini ikapoteza ugenini bao 2-0.

Msimu huu katika Ligi ya mabingwa Simba ilipoteza kwa Mkapa bao 3-0 na kisha ikanyukwa ugenini bao 3-1.

Simba inakutana na Wydad Casablanca kwa mara ya pili kwenye michuano ya Afrika ambapo mara ya mwisho kukutana ilikuwa Mei 21,2011 ambapo mnyama alipoteza kwa bao 3-0 kwenye Ligi ya mabingwa mchezo uliopigwa katika uwanja wa Petro Sport nchini Misri.

Kama kawaida yetu mechi po tayari kwenye tovuti. Tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87# kucheza.

Share this: