England vs ArgentinaEngland vs Argentina
  • England vs Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026, ni ratiba ya mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya mashindano haya itakayopigwa 15 July 2026.
  • Mchezo huu unaotarajiwa kupigwa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, utafanyika katika Uwanja wa Atlanta, USA
  • Staa wa Argentina, Lionel Messi pamoja na Julian Alvarez wanatarajiwa kuiongoza timu hiyo kuvaana na timu ngumu ya England chini ya mastaa, Jude Belingham na Harry Kane.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

England chini ya kocha, Thomas Tuchel baada ya kuifungashia virago Norway Jumatano 15 July 2026 watashuka uwanjani kuvaana na Argentina ya Lionel Messi.  Mchezo huu ni wa Nusu Fainali, ambao unatarajiwa kupigwa saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Staa wa Argentina na mfungaji bora wa mashindano haya mpaka sasa, Lionel Messi ataiongoza tena Argentina kusaka ushindi muhimu na tiketi ya kwenda Fainali. Hapa tunachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya England vs Argentina

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

England vs Argentina
England vs Argentina

Maelezo ya Mechi

KipengeleMaelezo
MashindanoMchezo huu ni wa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. Timu itakayoshinda itafuzu moja kwa moja kwenda Fainali, huku timu itakayopoteza ikicheza mechi ya kuwania nafasi ya tatu.
Tarehe na MudaMechi itachezwa Jumatano, 15 Julai 2026, kuanzia saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
UwanjaPambano litafanyika katika Atlanta Stadium, jijini Atlanta, Marekani. Uwanja huu ni miongoni mwa viwanja vinavyotumika kuandaa mechi za Kombe la Dunia la FIFA 2026 na una miundombinu ya kisasa inayokidhi viwango vya juu vya mashindano ya kimataifa.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104 ZA KOMBE LA DUNIA 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa England vs Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026

Baada ya kuwa na mechi mbili ngumu za hatua ya mtoano dhidi ya timu kutoka bara la Afrika; Cape Verde na Egypt, mabingwa watetezi Argentina walipata ahueni katika Robo Fainali ya ushindi wa mabao 3-1. Mchezo huo ulilazimika Kwenda hatua ya muda wa nyongeza, baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1. England nao walionyesha kuwa wanazidi kuwa timu bora kila hatua, hii ni baada ya kuiangamiza Norway kwa kuifunga mabao 2-1. Mshindi wa mechi hii atavaana na mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Spain vs France.

England na Argentina zitakutana kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia tangu mwaka 2002, zikisaka nafasi ya kucheza fainali. Wakati Lionel Messi akiwania taji lingine la dunia, England wana Jude Bellingham aliye katika kiwango bora. Ni zaidi ya miaka 20 imepita tangu mataifa haya mawili yakutane kwenye Kombe la Dunia, lakini ni mechi chache zinazobeba historia nzito kama hii.

England ilianza mashindano kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia kabla ya kutoka sare tasa dhidi ya Ghana. Baadaye iliifunga Panama mabao 2-0 na kumaliza kileleni mwa kundi lake. Katika hatua ya mtoano, England ililazimika kupambana kwa nguvu zaidi, Ilitoka nyuma na kuifunga DR Congo katika hatua ya 32 Bora, kisha ikaiondoa wenyeji wenza Mexico licha ya kucheza na wachezaji 10 kwa zaidi ya dakika 30. Katika robo fainali dhidi ya Norway, England ilijikuta nyuma baada ya Andreas Schjelderup kufunga bao la kuongoza, lakini ilirejea na kushinda mabao 2-1.

KUJUA KILA KITU KUHUSU KOMBE LA DUNIA 2026, SOMA HII: Kombe la Dunia 2026 |Linaanza lini? Timu ngapi? Kuchezwa wapi? Kuna Sheria mpya? Ronaldo au Messi? Haya hapa majibu ya maswali yote muhimu unayojiuliza

Habari za timu na majeruhi

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, anatarajiwa kuwa fiti kuikabili England katika nusu fainali ya Kombe la Dunia licha ya kupata jeraha dogo juu ya jicho lake. Messi alipata jeraha hilo kwenye mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Switzerland. Messi mwenye umri wa miaka 39 ameonyesha kiwango cha juu katika mashindano haya, akifunga mabao nane na kutoa asisti mbili katika mechi sita alizocheza hadi sasa.

Kulikuwa pia na hofu kuhusu beki wa kati wa Argentina, Cristian Romero, baada ya kutolewa uwanjani katikati ya muda wa nyongeza. Romero alikuwa amekabiliwa na jeraha la goti kabla ya kuanza kwa mashindano, jambo lililozua wasiwasi mpya alipofanyiwa mabadiliko. Hata hivyo, baada ya mchezo alieleza kuwa hakupata jeraha jipya bali alichoka kutokana na hali ya mchezo.

Kiungo wa Leandro Paredes pia alitolewa katika muda wa nyongeza na nafasi yake kuchukuliwa na José López, jambo lililoibua hofu ya kuumia. Hata hivyo, mabadiliko hayo yalikuwa ya kimkakati pekee na si kutokana na jeraha. Paredes anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Argentina kitakachokabiliana na England. Kwa upande wa Simba watatu, bado hakuna taarifa mpya za majeraha, hivyo hakutarajiwi mabadiliko makubwa ya kikosi.

Rekodi ya H2H England vs Argentina

England vs Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026
England vs Argentina H-2-H

Imepita miaka 21 tangu England na Argentina zilipokutana mara ya mwisho, ambapo England ilishinda mabao 3-2 katika mechi ya kirafiki. Mechi hiyo ilipigwa Geneva Switzerland, huku Michael Owen akifunga mabao mawili. Kwa ujumla huu utakuwa mkutano wa sita kati ya mataifa haya kwenye Kombe la Dunia, ambapo England imeshinda mara 3 (1962, 1966 na 2002) na Argentina imeshinda mara 2 (1986 na 1998).

Vikosi Vinavyotarajiwa

England:

Na.MchezajiNafasi
1Jordan PickfordKipa
2Ezri KonsaBeki wa Kulia
5John StonesBeki wa Kati
6Marc GuéhiBeki wa Kati
3Nico O’ReillyBeki wa Kushoto
4Declan RiceKiungo wa Ulinzi
8Elliot AndersonKiungo wa Kati
20Noni MaduekeWinga wa Kulia
10Jude BellinghamKiungo wa Ushambuliaji
18Anthony GordonWinga wa Kushoto
9Harry KaneMshambuliaji

Argentina:

Na.MchezajiNafasi
23Emiliano MartínezKipa
26Nahuel MolinaBeki wa Kulia
13Cristian RomeroBeki wa Kati
6Lisandro MartínezBeki wa Kati
3Nicolás TagliaficoBeki wa Kushoto
5Leandro ParedesKiungo wa Ulinzi
7Rodrigo De PaulKiungo wa Kati
20Alexis Mac AllisterKiungo wa Kati
24Enzo FernándezKiungo wa Ushambuliaji
10Lionel MessiMshambuliaji Msaidizi
9Julián ÁlvarezMshambuliaji

Utabiri Wetu (kupatikana mabao mawili au zaidi yaani over 1.5)

Argentina imepitia mechi ngumu katika hatua za mtoano, lakini imeonyesha tabia ya mabingwa kwa uwezo wake wa kurejea mchezoni na kushinda hata katika mazingira magumu. Hali hii pia tumeishuhudia kwa England, lakini timu zote mbili zina safu kali za ushambuliaji ambazo zinaweza kufunga bao wakati wowote. Kwa uchambuzi wetu wa kitaalamu, upo uwezekano mkubwa wa kupatikana mabao angalau mawili au zaidi, ikumbukwe utabiri huu unatokana na maoni ya kiuhariri na si matokeo halisi, hivyo chambua mkeka wako na Bashiri kistaarabu.

KUFAHAMU TAARIFA MUHIMU ZA KOMBE LA DUNIA 2026, SOMA HII: World Cup 2026 Group D Fixtures, Standings & Table | Full Schedule, Teams and Latest Rankings

Hitimisho

Nukuu ya kocha wa Argentina kuhusu mechi hiyo
Nukuu ya kocha wa Argentina kuhusu mechi hiyo

Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaonyesha tunatarajia mchezo mgumu sana, England imepewa nafasi kubwa kidogo ya kushinda kutokana na kutopoteza mechi yoyote katika hatua za mtoano pamoja na kiwango bora kinachoonyeshwa na Jude Bellingham. Hata hivyo, Argentina imeendelea kuthibitisha uwezo wake wa kushinda mechi ngumu za mtoano chini ya kocha Lionel Scaloni, jambo linalowafanya kuwa chaguo zuri kwa wanaotafuta odds zenye thamani. Fuatilia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.