Patashika nguo kuchanika ya michezo ya robo fainali, michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, itaunguruma hapo kesho, ambapo wawakilishi wa Tanzania Klabu ya Yanga itakuwa na kibarua kizito katika Jimbo la Akwa Ibom Kusini mwa Nigeria kesho, April 23,2023 watakapokabiliana na Rivers United.
Mchezo wa Rivers United dhidi ya Yanga, unaturejesha nyuma katika msimu wa 2020/21 ambao Yanga walipangwa na wakali hawa kutoka Nigeria, kuwania nafasi ya kucheza makundi Klabu bingwa Afrika,na Wananchi waliokuwa wakijenga timu kwa wakati huo walitupwa nje ya mashindano kwa kipigo cha mabao 2-0 baada ya mechi mbili.
Mtanange wa marudiano uliopigwa huko Nigeria, uligubikwa na sekeseke la fitina za wenyeji dhidi ya Yanga.
Kisa kikubwa cha vurugu walizokutana nazo Yanga ni kufuatia Rivers United kutaka kujaribu kuwazuia baadhi ya wachezaji muhimu wa Yanga, kwa madai kuwa walifeli vipimo vya Corona, jambo ambalo liliwafanya Wananchi kutishia kugomea mchezo, lakini baadae waliruhusiwa ingawa vurumai hizo zilichagiza kuwaondoa Wananchi mchezoni na kupelekea kupoteza mchezo.
Katika mchezo huo alisikika aliyewahi kuwa Afisa Habari wa Yanga, Haji Manara akisema ”Hatuchezi hatuchezi” ikiwa ni sehemu ya kuonyesha walikuwa wakifanyiwa mizengwe nje ya Uwanja.
Vurumai hizo ndizo zilizosababisha viongozi wa Yanga kufurahia droo hii, iliyowarejesha dhidi ya Rivers wakiamini ni muda sahihi wao kulipa kisasi kwa kuwaondosha Rivers United, katika michuano ya Kombe la Shirikisho, ikizingatiwa Wananchi wataanzia ugenini na kumalizia Jijini Dar es salaam.
Kwa uchache tuiangazie safari ya Wananchi ambao wao walianzia hatua ya awali walipowacharaza Zalan jumla ya mabao 9-0 na kusogea hatua ya mwisho wa mtoano Klabu bingwa Afrika na ndipo walipokwaa kisiki mbele vijana wa Florent Ibenge, Al Hilal Ormduman waliowatupa nje Wananchi kwa jumla ya bao 2-1 na kuwaacha kwenye michuano ya Shirikisho Afrika.
Katika hatua ya mtoano Yanga walikabidhiwa mikononi mwa Club Africain na walianzia kwa Mkapa wakatoka suluhu kabla ya kuwashangaza wengi kwa ushindi wa bao 1-0 nchini Tunisia,bao maridhawa la Aziz Stephane Ki lililowapeleka Yanga hatua ya makundi.
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Nassredine Nabi kilipangwa kundi moja na Klabu za US Monastir ya Tunisia, Real Bamako ya Mali na TP Mazembe ya DR Congo.
Katika kundi hilo Yanga ambayo haikupewa nafasi kubwa walimaliza vinara wa kundi lao wakiwa na alama 13, wakishinda mechi zote tatu za nyumbani na moja ugenini,sare moja ugenini na wakapoteza mechi moja nchini Tunisia. Kwa kifupi wananchi walikuwa na ushindi wa asilimia 100, walipocheza nyumbani kwenye hatua ya makundi na walipoteza mechi moja pekee.
Kwa ujumla kuanzia kwenye mchakato wa awali, Yanga ilicheza mechi 6 nyumbani na kushinda mechi 4 na sare 2 wakati ugenini ilicheza mechi 6, ilishinda mechi 3 ,sare 2 na 1 imepoteza.
Ikiwa nyumbani Yanga wameruhusu mabao 2 tu, dhidi ya Al Hilal na Tp Mazembe huku wakifunga mabao 13 lakini ikiwa ugenini Yanga imeruhusu bao 4 na yenyewe ikifunga bao 3.
Tuigeukie safari ya Rivers United ambao nao walianzia kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kwenye hatua ya awali waliwatandika Watanga FC jumla ya bao 4-0 lakini wakakutana na kizingiti kwenye hatua ya mwisho walipokutana na Wydad Athletic Club ambao waliwanyoosha kwa bao 7-2.
Baada ya kutupwa nje ya Wydad, Rivers walipangiwa Al Nasr ambao waliwanyuka jumla ya bao 6-0 na kutinga makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika na wakachuana na Klabu za Asec Mimosas ya Ivory Coast, DC Motemba Pembe ya DR Congo na Diables United.
Katika kundi lao Rivers ilimaliza kama mshindi wa pili nyuma ya vinara Asec Mimosas na ndipo walipopangwa na Yanga kwenye hatua ya robo fainali.
Wakiwa nyumbani Rivers wanaonekana ni bora zaidi kwani tangu kwenye hatua za awali wamecheza jumla ya michezo 6,wameshinda 5 na sare 1 tu wakati wakiwa ugenini wamepoteza mechi 4,sare 1 na ushindi 1 pekee.
Hivyo Yanga wanakwenda nchini Nigeria wakiwa na tahadhari kubwa kwakuwa Rivers wanajua kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kupata matokeo na katika mechi hizo sita nyumbani wamefunga jumla ya mabao 18 na kuruhusu bao 4.
Wakiwa ugenini wameruhusu mabao 9 na wao wakifunga bao 1 pekee wakiwa ugenini,ukilinganisha takwimu hizo unapata taswira kwamba upo uwezekano mkubwa wa kuwafunga nyumbani kwako lakini historia inatukumbusha kuwa mara ya mwisho walipokanyaga ardhi ya Tanzania waliwafunga Yanga bao 1-0.
Nyota wa kuchungwa kwa Rivers United ni Paul Acquah ambaye katika michuano ya Kombe la Shirikisho amepachika mabao manne katika mechi 6 alizocheza, huku akitoa pasi ya bao moja,lakini amewahi kuadhibiwa kwa kadi nyekundu.
Mchezaji mwingine katika timu ya Rivers United anayemfuatia Paul Acquah katika magoli ya kufunga ni Nwangwa Nyima aliyefunga mabao mawili.
Upande wa Yanga nguvu yao kubwa ipo kwa Fiston Mayele mwenye mabao 3 katika michuano hiyo, bila kumsahau Kenedy Musonda ambaye amehusika katika mabao matano ya Yanga hadi walipofikia. Pia mchezaji Aziz Ki pamoja na Mudathir Yahya, Jesus Moloko, Khalid Aucho wanategemewa kuwa nguzo imara katikati ya uwanja.
Hakuna taarifa mpya ya majeraha zaidi kwenye kikosi cha Yanga zaidi ya mlinda mlango Abdultwalib Mshery huku beki Mahmadou Doumbia akitarajiwa kuungana na wenzake nchini Nigeria baada ya kumaliza matatizo ya kifamilia.
SportPesa tukiwa wadhamini wakuu wa Yanga na pia kampuni inayoongoza ya ubashiri Tanzania tumekuwekea mechi hii katika tovuti yetu.
Kubashiria mechi hii tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

