Ratiba ya nusu fainali FIFA Kombe la Dunia 2026Mbappe (-)
  • Ufaransa vs Hispania FIFA Kombe la Dunia 2026 mchezo wa nusu fainali unaokutanisha mataifa yenye vikosi bora
  • Julai 14,2026 mchezo huu utapigwa saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki
  • Mshindi atakata tiketi ya fainali atakutana na mshindi wa mchezo wa fainali kati ya Argentina vs England utakaopigwa Julai 15,2026

Ufaransa vs Hispania FIFA Kombe la Dunia 2026 zinakutana siku ya Jumanne hatua ya nusu fainali. Mchezo huu mkali utapigwa Uwanja wa Dallas. Julai 14, saa 10:00 usiku saa za Afrika Mashariki wababe hawa watakuwa kazini kusaka tiketi kutinga fainali.

Mabingwa watetezi kazini: Prediction | England vs Argentina FIFA Kombe la Dunia 2026: Nusu fainali, Ratiba, Live score, h2h, odds na habari za timu

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Ufaransa vs Hispania
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

France vs Spain
France vs Spain

Ufaransa vs Hispania taarifa za mechi

KipengeleMaelezo
MashindanoFIFA Kombe la Dunia 2026
MechiUfaransa vs Hispania
HatuaNusu Fainali
SikuJumanne
TareheJulai 14, 2026
MudaSaa 4:00 usiku (Saa za Afrika Mashariki – EAT)
UwanjaDallas Stadium, Arlington, Texas, Marekani

Ufaransa vs Hispania taarifa kuhusu timu

Ufaransa vs Hispania FIFA Kombe la Dunia 2026
France vs Spain FIFA Kombe la Dunia 2026

Ijue ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Les Bleus (jina la utani la timu ya taifa ya Ufaransa) wamekuwa miongoni mwa timu zilizong’ara zaidi kwenye mashindano haya. Walishinda mechi zote tatu za hatua ya makundi kabla ya kuziondoa Uswidi, Paraguay na Morocco katika hatua za mtoano na kufuzu nusu fainali.

Hispania ilianza mashindano kwa kusuasua baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Cabo Verde, lakini baadaye iliongoza kundi lake kabla ya kuziondoa Austria, Ureno na Ubelgiji ili kutinga hatua ya nne bora.

Kikosi cha kocha Didier Deschamps kinawania kuweka historia kwa kuwa taifa la pili la Ulaya kufika fainali tatu za Kombe la Dunia mfululizo, baada ya Ujerumani Magharibi kufanya hivyo hapo awali.

Ufaransa imeonyesha ubora mkubwa katika mashindano haya, ikiwa imefunga mabao 13 na kuruhusu mabao mawili tu. Aidha, bado haijaruhusu bao lolote katika hatua za mtoano, jambo linaloonyesha uimara mkubwa wa safu yake ya ulinzi.

Ufaransa vs Hispania wachezaji wakuchungwa

Kylian Mbappé ameendelea kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Ufaransa kwa kiwango cha juu, akiwa tayari amefunga mabao nane katika mashindano haya. Wakati huo huo, Ousmane Dembélé, Michael Olise, Bradley Barcola na Désiré Doué wamekuwa muhimu kwa kuongeza kasi, ubunifu na nafasi za kufunga katika eneo la mwisho la ushambuliaji.

Katika safu ya ulinzi, William Saliba na Dayot Upamecano wameunda ushirikiano imara katikati ya ulinzi, na kuwa miongoni mwa mabeki bora zaidi katika mashindano haya.

Kwa upande wa Hispania, timu hiyo imeendelea kuimarika kadri mashindano yalivyoendelea baada ya sare ya mechi ya ufunguzi. Baadaye ilitoa maonyesho mazuri na yenye utulivu dhidi ya Saudi Arabia na Uruguay, kabla ya kuziondoa Austria, Ureno na Ubelgiji ili kufuzu nusu fainali.

Kikosi cha kocha Luis de la Fuente kimejenga mafanikio yake kupitia umiliki mzuri wa mpira katikati ya uwanja, ambapo Rodri, Pedri na Dani Olmo wamekuwa wakiongoza mchezo. Pembeni mwa uwanja, chipukizi Lamine Yamal pamoja na Nico Williams wamekuwa tishio kwa kasi yao na uwezo wa kubadili mwelekeo wa mashambulizi.

Hispania pia imeonyesha uimara mkubwa katika safu ya ulinzi, ikiwa imeruhusu bao moja tu katika mashindano yote. Aymeric Laporte na Pau Cubarsí wameongoza vyema safu ya nyuma mbele ya kipa Unai Simón.

Habari za vikosi: Ufaransa dhidi ya Hispania

Ufaransa haina tatizo kubwa la majeraha kuelekea mchezo wa nusu fainali, na inatarajiwa kubaki na kikosi kilekile kilichoiondoa Morocco kwa ushindi wa kishindo katika robo fainali.

Kipa Mike Maignan anatarajiwa kuendelea kuanza langoni, akilindwa na mabeki wa kati William Saliba na Dayot Upamecano. Nafasi za mabeki wa pembeni zinatarajiwa kushikiliwa na Jules Koundé na Lucas Digne.

Katikati ya uwanja, Adrien Rabiot na Manu Koné wanatarajiwa kucheza kama viungo wa ukabaji, huku Michael Olise, Ousmane Dembélé na Désiré Doué wakipewa jukumu la kumsaidia Kylian Mbappé katika safu ya ushambuliaji.

Kwa upande wa Hispania, pia inatarajiwa kushuka uwanjani ikiwa na karibu kikosi chake kamili baada ya kufanikiwa kuiondoa Ubelgiji na kutinga hatua ya nusu fainali.

Habari za Kikosi: Ufaransa dhidi ya Hispania

Kwa upande wa Hispania, kipa Unai Simón anatarajiwa kuanza langoni nyuma ya safu ya ulinzi itakayoundwa na Pedro Porro, Pau Cubarsí, Aymeric Laporte na Marc Cucurella.

Katikati ya uwanja, Rodri na Pedri wanatarajiwa kuendelea kuiongoza timu katika umiliki wa mpira, huku Dani Olmo akicheza nyuma ya nahodha Mikel Oyarzabal. Kwenye winga, Lamine Yamal anatarajiwa kuanza upande wa kulia, wakati Álex Baena atacheza upande wa kushoto.

Vikosi Vinavyotarajiwa Kuanza

UfaransaHispania
Kipa: Mike MaignanKipa: Unai Simón
Mabeki: Jules Koundé, Dayot Upamecano, William Saliba, Lucas DigneMabeki: Pedro Porro, Pau Cubarsí, Aymeric Laporte, Marc Cucurella
Viungo: Manu Koné, Adrien RabiotViungo: Rodri, Pedri
Washambuliaji wa nyuma: Michael Olise, Ousmane Dembélé, Désiré DouéWashambuliaji wa nyuma: Lamine Yamal, Dani Olmo, Álex Baena
Mshambuliaji: Kylian MbappéMshambuliaji: Mikel Oyarzabal

Rekodi ya Mechi na Kiwango cha Sasa: Ufaransa dhidi ya Hispania

Licha ya kwamba Ufaransa na Hispania ni miongoni mwa mataifa yenye historia kubwa katika Kombe la Dunia, hii itakuwa mara ya pili pekee kwa timu hizo kukutana katika michuano hiyo.

Mara yao ya kwanza kukutana ilikuwa katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2006, ambapo Ufaransa ilitoka nyuma kwa bao moja na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, katika mchezo uliobaki kuwa mmoja wa kumbukumbu muhimu kwa Les Bleus.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, Hispania imekuwa na rekodi nzuri zaidi dhidi ya Ufaransa. La Roja iliifunga Ufaransa katika nusu fainali ya UEFA EURO 2024, na baadaye ikaibuka tena na ushindi katika nusu fainali ya UEFA Nations League 2024/25.

Kwa hiyo, mchezo wa Jumanne unatarajiwa kuwa wa ushindani mkubwa, huku Ufaransa ikisaka kulipiza kisasi kwa vipigo hivyo vya karibuni, na Hispania ikitaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya wapinzani hao.

Kiwango cha sasa cha timu

Ufaransa inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kiwango bora kabisa. Imeshinda mechi zote tano ilizocheza kwenye Kombe la Dunia 2026, ikifunga mabao 13 na kuruhusu mabao mawili tu. Uwezo wao mkubwa wa kushambulia pamoja na uimara wa safu ya ulinzi umeifanya kuwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kwa upande wa Hispania, nayo haijapoteza mechi yoyote tangu ilipotoa sare katika mchezo wake wa kwanza. Timu hiyo imeendelea kuonyesha soka lake la umiliki wa mpira, huku ikitumia vizuri nafasi za kufunga katika hatua za mtoano. Ulinzi wake wenye nidhamu na uwezo wa kutawala mchezo kupitia safu ya kiungo vimekuwa nguzo muhimu za mafanikio yao.

Prediction Ufaransa vs Hispania

Nusu fainali hii inatarajiwa kuwa moja ya michezo mikubwa na yenye ushindani mkali kati ya mataifa mawili makubwa ya soka barani Ulaya. Ufaransa ina nguvu kubwa katika mashambulizi ya kushtukiza, ikiwa na kasi ya wachezaji wake wa mbele na safu ya ushambuliaji inayotajwa kuwa miongoni mwa bora zaidi katika mashindano haya. Kwa upande mwingine, Hispania inategemea ubora wa kiufundi na uwezo wa viungo wake kutawala umiliki wa mpira na kudhibiti kasi ya mchezo.

Mapambano kati ya safu ya ushambuliaji ya Ufaransa na ulinzi imara wa Hispania yanaweza kuwa jambo litakaloamua mshindi wa mchezo huu. Kwa kuwa timu zote mbili ziko kwenye kiwango cha juu, makosa madogo yanaweza kuamua matokeo.Ufaransa inaonekana kuwa na makali zaidi katika eneo la ushambuliaji, jambo ambalo linaweza kuipa faida ya kufuzu fainali.

Utabiri: Ufaransa 2-1 Hispania. Haya ni maoni ya mhariri sio matokeo kamili.

France vs Spain
France vs Spain

Namna ya kubashiri kupitia SportPesa

Fungua ukurasa wa tukio la Ufaransa vs Hispania kwenye SportPesa.
Chagua soko lako Single Bet (SB), Multi-Bet (MB), au Live Bet (LB) mara tu mechi itakapoanza.
Weka dau lako na thibitisha ubashiri.

Hitimisho

Ufaransa vs Hispania FIFA Kombe la Dunia 2026 ni mchezo wa maamuzi unazikutanisha timu bora. Hii ni kama fainali kutokana na ubora wa mataifa yote. Mshindi wa mchezo anakwenda fainali atakutana na mshindi wa mchezo kati ya mabingwa watetezi Argentina vs England unaotarajiwa kuchezwa Julai 15,2026.

Share this: