skip to Main Content
MJASIRIAMALI TABATA ALAMBA 5,615,992 JACKPOT YA SPORTPESA!!
SportPesa Jackpot Bonus Winner

MJASIRIAMALI TABATA ALAMBA 5,615,992 JACKPOT YA SPORTPESA!!

Mkazi wa Tabata Kimanga Deus Isidory Msigwa, amebahatika kushinda kitita cha Sh 5,615,992, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13, kama bonus ya Jackpot ya SportPesa.

Akizungumza katika ofisi za SportPesa, Oyesterbay, Jijini Dar-Es-Salaam, Deus anasema alianza kucheza na SportPesa miaka miwili iliyopita, baada ya mshkaji wake wake wa Karibu Ezra kushinda Mil 31 za Jackpot Bonus.

‘’Mimi nilianza kucheza na SportPesa kama miaka miwili iliyopita. Si kwamba ni mgeni wa michezo hii kabla sijaanza kucheza na SportPesa bali wakati ule nilikuwa nacheza na kampuni nyingine. Sasa kuna mambo hayakwenda sawa, hivyo niliacha kwa muda.

Ilipotokea jamaa yangu Ezra ameshinda Mil 31, nilianza kuifutailia SportPesa kupitia mitandao ya kijaamii na baada ya muda nilipakua app yao na kuanza kujifunza taratibu taratibu namna ya kucheza’’. Alisema Deus.

Deus anaendelea kusema kwamba tangu ameanza kucheza na SportPesa kiwango cha juu kuwahi kula ni Sh 3000 kwenye mechi za kawaida ambazo tayari ameshacheza.

‘’Unajua mimi ninacheza zaidi Multi bet, hivyo nikiwa maeneo ya Tabata kama nina hela huwa najaribu kucheza mechi za multi bet na Jackpot.

Mara nyingi kabla ya ushindi huu wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki nilikuwa nashinda vihela vidogo dogo kama buku moja moja na elfu mbili, mbili.  Vihela hivyo vilinipa moyo.

Anaendelea kwa kusema ushindi huu kwake una umuhimu mkubwa sana, kwani kutoka kiwango cha Sh 1000,2000 na 3000 alichokizoea mpaka Mil 5,615,992 ni bahati kubwa kwake. ‘’Nafikiri huu ni mwanzo wa safari ya ushindi kwangu mimi. Ushindi huu umenipa hamasa ya kucheza Jackpot zote mbili za SportPesa kwa nguvu sana.

Kuhusu mkeka huu wa Jackpot ya kati kati ya wiki ulioshinda, Deus anasema, kwa kawaida yeye huwa anaweka mikeka sita ya Jackpot za SportPesa, kila wiki. Huwa naanza na mikeka 3 ya Jackpot ya kati kati ya wiki na pia pale mikeka ya Supa Jackpot inapotoka huwa naweka mikeka mingine mitatu.

Kwa mkeka huu wa ushindi niliweka mkeka siku ya Jumatatu, ambapo baada ya kuziona mechi nilichukua masaa kadhaa kabla ya kuuweka na kusubiria matokeo. Kwa namna ambavyo niko na presha, nikisha weka mkeka huwa siangalii au sifuatilii matokeo.

‘’Matokeo ya Jackpot bonus hii mimi wala sikuyafuatilia, sasa nilijuaje kama nimeshinda. Nilikuwa zangu kwenye mishe mishe zangu, nakumbuka, ilikuwa majira ya saa 5 asubuhi, nikiwa nafanya mitikasi yangu ikaingia sms ikinipa Hongera.

Nashukuru Mungu juhudi zangu japo kwa kiwango hichi zimefanya kazi na nimeweza kushinda za Jackpot bonus.

Kwa sasa najipanga kuona nitafanyia nini fedha hii, lakini kitu cha kwanza ambacho hakina mjadala ni kupeleka fedha hii kwenye matengenezo ya nyumba yangu ambayo ujenzi bado unaendelea.

Akimalizia Deus anawashukuru SportPesa kwa fursa ya Jackpot bonus kwani ni SportPesa pekee ambapo mchezaji anashinda hela tena nyingi hata kama hakushinda Jackpot yenyewe. ‘’Lazima niwe mkweli katika kutoa shukrani zangu.

Tangu nimeanza kubashiri na makampuni mbali mbali hakuna hata kampuni moja ambayo ina Jackpot inayofanana na hizi mbili za SportPesa. Maana yake ni kwamba SportPesa wametoa fursa kubwa sana kwa  sisi wachezaji.

Jukumu letu ni moja tu, Kuweka pesa nakucheza!

Akimpongeza Deus kwa ushindi wa Jackpot Bonus ya katikati ya wiki, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya aliwataka watanzania kuendelea kuiunga mkono SportPesa, kutokana na fursa ambazo zipo kwa wachezaji.

Nafikiri mtakuwa mnakumbuka wiki iliyopita alipatikana mshindi wa Supa Jackpot bonus wa Mil 56, ambaye anatokea Bagamoyo. Leo nipo hapa kumpongeza Deus kwa ushindi wake alioupata baada ya kupatia mechi 12 kati ya 13 kwa usahihi.

Ni juhudi yako kama mchezaji, kuendelea kucheza kila Jackpot zinapotoka, ili uweze kucheza na kujaribu fursa ya kuwa bilionea au milionea kama Deus alivyojishindia mkwanja huu wa Sh 5,615,992.

Supa Jackpot ya wiki mecho kuanzia 13 hadi 17 imesimamia  shillingi 1,096,041,286 .

Share this:
Back To Top