
Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania NBC Premier League | Highlights | Msimamo
- Dodoma Jiji FC imekutana mara moja na JKT Tanzania ndani ya NBC Premier League, Oktoba 27,2026 wakitoshana nguvu.
- Kwenye msimamo JKT Tanzania ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 17,Dodoma Jiji FC nafasi ya 5 ina pointi 15.
- Uwanja wa Jamhuri,Dodoma wababe hawa walikutana katika pambano kali 2026/27.
Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa NBC Premier League uliochezwa Oktoba 27,2026. Pambano hili lilipigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.Bikoko Andy wa Dodoma Jiji alichaguliwa kuwa mchezaji bora wakati wakigawana pointi mojamoja.
SOMA HII PIA:JKT Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege
Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.
Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania taarifa muhimu
Kwenye pambano la Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania wababe hawa walitoshana nguvu ndani ya dakika 90.Timu hizi zote zimekuwa zinaonyesha ushindani mkubwa ndani ya uwanja.
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Matokeo | Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania |
| Uwanja | Jamhuri,Dodoma |
| Tarehe | 27/10/2026 |
| Timu mwenyeji | Dodoma Jiji FC |
Takwimu muhimu Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania
| Kipengele | Dodoma Jiji FC | JKT Tanzania |
| Mabao | 0 | 0 |
| Mashuti | 11 | 11 |
| Umiliki | 49% | 51% |
| Pasi | 315 | 386 |
| Kona | 2 | 5 |
| Nafasi zilizotengenezwa | 11 | 10 |
Dodoma Jiji FC walitumia mbinu yakujilinda mara licha ya kuwa walikuwa nyumbani.JKT Tanzania waliongoza kwa kufanya mashambulizi zaidi wakipata kona 5.Mashuti ambayo yalilenga lango wenyeji walipiga 1 huku wageni wakipiga 5.Ni kwa mujibu wa Sokametrics.
Athari za matokeo kwenye msimamo wa ligi
Matokeo haya yana athari katika msimamo wa Ligi Kuu Bara. Kila pointi ni muhimu katika mbio za ubingwa au kuepuka kushuka daraja. Timu zote mbili zitahitaji kurekebisha mikakati yao katika michezo ijayo ili kupata matokeo bora.Ligi Kuu Bara inaendelea kuwa na ushindani mkali, ambapo kila mchezo unatoa changamoto mpya. Timu zinajitahidi kuhakikisha zinapata pointi tatu ili kujiweka katika nafasi nzuri.
Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 15 ikiwa nafasi ya 5 imecheza mechi 9. JKT Tanzania nafasi ya 4 pointi 17 baada ya mechi 10. Vinara ni Simba SC wakiwa na pointi 24 baada ya mechi 8 wanafuatiwa na mabingwa watetezi Yanga SC nafasi ya pili na pointi 22 baada ya mechi 9.
SOMA HII PIA:JKT Tanzania yaingia 4 bora baada ya ushindi wa bao 1-0 Kagera Sugar NBC Premier League
Hitimisho
Matokeo ya Dodoma Jiji FC 0-0 JKT Tanzania matokeo ya mzunguko wa kwanza. Januari 15,2027 wababe hawa wanatarajiwa kukutana mzunguko wa pili.Dodoma Jiji FC imeshinda mechi 4 huku JKT Tanzania ikishinda mechi 5 kwenye ligi msimu wa 2026/27.


